Mch. Fernandez amlaumu Nyerere kwa kutaifisha mali za wahindi!

Mtego wa Noti

JF-Expert Member
Nov 27, 2010
2,591
1,599
Mch Fernandez wa Agape Ministries kupitia ATN anasema mambo yanayoendelea hapa Tanzania hasa wezi unaofanywa na wawekezaji inatokana na dhambi aliyoifanya Nyerere ya kutaifisha mali za wahindi na watu wengine miaka iliyopita. anasema walichukua mali za watu bila bila ridhaa yao na bila ya kuvuja jasho, ndio maana laana ya alichofanya nyerere ndiyo inayorudi sasa kwa watu kuja kuiba raslimali zetu.

anaunganisha na maneno ya kwenye bible kuwa kama mkuu mmoja wa familia akifanya kosa, laana hiyo inaweza kusambaa na kuwafuata wazaliwa wa mbeleni.

Source ni ATN live boadcasting!
 
Mbona waumini wake wengi siyo wahindi? Mbona anauza TING? Mbona kifamilia zaidi? Mbona anahukumu? Mbona kimtindo flani? Haya taja akaunti tutoe tulichonacho...
 
Hivi ujumbe huo una uhusiano gani na neno la Mungu kama si maslahi tu huyu?

Mambo ya Kaisari amwachie kaisari...
 
Anatumia maandiko isivyo sahihi. Anatakiwa kwenda kurudia kuusoma ushauri wa Paulo kwa Timotheo
"Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli"

Asidanganye watu, tumwuulize kabla ya 1967 wahindi na wagoha walikuwa wamewaibia na kuwadharumu watanganyika kwa kiwango gani?

Awe na kawaida ya kutumia andiko kwa halali siyo kulilazimisha andiko likubaliane na anacho kiwaza.
 
Kuna watu wanajaribu kuisahihisha mapungufu yao kwa kumtwisha 'lawama' Nyerere. Wanaiandika tena historia. Natamani nyerere mpya aje achukue kilicho chetu toka kwa baadhi ya corrupt indians
 
Mtume wa Kiindi Yupo Sahihi Kabisa!Viwanda na Mashirika vilitahifishwa wakapewa watu wasiokuwa na Uwezo wala ujuzi wa Kuviendesha!Matokeo vikafisadiwa kisha vikayumba hatimae nchi ikafilisika kama Zimbabwe ya mugabe leo!
Nadharia za Azimio la AR nazikubali hasa Miiko ya Uongozi IPO SAFI MNO,Kipengee cha Serikali Kumiliki njia kuu za Uchumi ndio kosa na alikosea kabisa kutaifisha mali za watu!Yeye angejenga vya umma na wale kuwakaba kodi
madhara ya kutaifisha ndio yaliyomkuta hata Mugabae nchi yake sasa hivi tee
 
Huyo jamaa ni msanii mbona anajidai ni mchungaji lakini sasa amefungua kapuni ya Agape Associate ianjishugulisha na mabo mengi sana ya kibiashara.

sasa TV yake ya Agape ni mpaka ulipie TIN ndio unapata matangazo,na tukumbuka katika mkutano wa Mh Pinda na waekezaji wa Sumbawanga na maeneo ya kusini alialikwa kama mmoja wa wafanya biashara wakubwa.sasa yeey anausafi gani mpaka amseme Nyerere?

sasa hivi tunapata faida gani kwa mali wanazomiliki wahidi? kama wahindi kuachiwa mali zote za nchi ndio kigezo cha sisi kuwa na mafanikio??
 
Aseme tu kuwa wahindi huwa wanakaa mguu mmoja ndani mwingine nje, ndo ukweli, wako hapo kuchuma tu,basi.
 
Jiulize kwanini wahindi huwa wanaenda ku retire either Canada ama UK?

Na wakifika huko zile pesa walizochuma bongo walizoweka huko, wanafungua duka or some sort of a business ie gas station, wana retire, vijana waliobaki bongo wanaendelea kusuguana na mafisadi wetu huku wanawazungusha akili,na wakiendelea kuchuma hadi zamu yao ya ku retire ifike.

Wahindi kwa utajiri walio nao kama wangekuwa wanaipenda nchi all the way, ama kukawa na system inayowabana ili at least wajenge makazi/nyumba nk, basi mambo yangekuwa better na pengine tungekuwa mbali sana, mwalimu kutaifisha inawezekana alikuwa wrong lakini madhumuni ndo hayo ya kutaka kuona manufaa kwa wananchi.
 
Huyo jamaa ni msanii mbona anajidai ni mchungaji lakini sasa amefungua kapuni ya Agape Associate ianjishugulisha na mabo mengi sana ya kibiashara,sasa TV yake ya Agape ni mpaka ulipie TIN ndio unapata matangazo,na tukumbuka katika mkutano wa Mh Pinda na waekezaji wa Sumbawanga na maeneo ya kusini alialikwa kama mmoja wa wafanya biashara wakubwa.sasa yeey anausafi gani mpaka amseme Nyerere? sasa hivi tunapata faida gani kwa mali wanazomiliki wahidi? kama wahindi kuachiwa mali zote za nchi ndio kigezo cha sisi kuwa na mafanikio??

Naikumbuka ile miaka ya '90 mwanzani alikuwaje, alisemaje na leo anasemaje? ....NATAFAKARI...
 
Ndo shida yao wahindi wasio na adabu, kesha chota pesa ya wabongo na sasa anataka kuhalalisha wizi wa wahindi wa toka enzi. Mbona tunajua kuwa wahindi hawajaanza leo kuwaibia wabongo na kwenda kuzitumia mali hizo Canada na Ulaya. Kaniudhi huyu! Siku moja kwenye hiyo tv yake walikuwa wanasherehe za kutimiza mwaka, kuna mtu akapiga simu na kumpongeza kwa maneno huku akiahidi kuendelea kuwaombea. Akawaka ajabu eti "hongera hongera nini, hongera bila pesa! sema unatuma shilingi ngapi, utaendelea kutuombea kwani sisi hatujui kuomba?". Mjinga huyu halafu anamtuhumu Nyerere eti alifanya dhambi, na yeye dhambi za hao mababu zake walowaibia mababu zetu. Huyu! we ngoja.
 
Mch Fernandez wa Agape Ministries kupitia ATN anasema mambo yanayoendelea hapa Tanzania hasa wezi unaofanywa na wawekezaji inatokana na dhambi aliyoifanya Nyerere ya kutaifisha mali za wahindi na watu wengine miaka iliyopita. anasema walichukua mali za watu bila bila ridhaa yao na bila ya kuvuja jasho, ndio maana laana ya alichofanya nyerere ndiyo inayorudi sasa kwa watu kuja kuiba raslimali zetu.

anaunganisha na maneno ya kwenye bible kuwa kama mkuu mmoja wa familia akifanya kosa, laana hiyo inaweza kusambaa na kuwafuata wazaliwa wa mbeleni.

Source ni ATN live boadcasting!

Hawa ndio wale wakoloni wanaorudi kwa mlango wa nyuma, hakuna mhindi aliyekuja na mali zake kutoka india wamezipata kiujanja ujanja hapa mjini, waTZ tuungane tuwatimue hawa jamaa tena kwa mara nyingine.
 
I had the very similar opinions.

Umaskini tunaoupata nchini ni laana juu ya ukwapuaji wa mali za watu. Alichokifanya Nyerere ni wizi tu. Huwezi kuchukua mali za watu kwa dhulma halafu utegemee neema.

Mchungaji umenena kweli na kwa hili mimi nakuunga mkoni 100%. Utaacha nihamie kwenye channel station yako.

Kikwebo.
 
Jiulize kwanini wahindi huwa wanaenda ku retire either Canada ama UK?

Na wakifika huko zile pesa walizochuma bongo walizoweka huko, wanafungua duka or some sort of a business ie gas station, wana retire, vijana waliobaki bongo wanaendelea kusuguana na mafisadi wetu huku wanawazungusha akili,na wakiendelea kuchuma hadi zamu yao ya ku retire ifike.

Wahindi kwa utajiri walio nao kama wangekuwa wanaipenda nchi all the way, ama kukawa na system inayowabana ili at least wajenge makazi/nyumba nk, basi mambo yangekuwa better na pengine tungekuwa mbali sana, mwalimu kutaifisha inawezekana alikuwa wrong lakini madhumuni ndo hayo ya kutaka kuona manufaa kwa wananchi.

Jmushi.
99% viwanda vya Tanzania ni vya wahindi...
 
Hawa ndio wale wakoloni wanaorudi kwa mlango wa nyuma, hakuna mhindi aliyekuja na mali zake kutoka india wamezipata kiujanja ujanja hapa mjini, waTZ tuungane tuwatimue hawa jamaa tena kwa mara nyingine.

Si kweli kama walizipata kwa kuiba. Wahindi wanajulikana kwa utafutaji wao na umahiri katika kufanya biashara.
 
Waswahili husema ukimzoea sana Mbwa atakufuata hadi msikitini! Huyu Mhindi amefika hatua ya kuwa analyst wa siasa zetu sasa! Yaani keshawanyonya waumini wake maskini hajatosheka, kajifanya mtume na nabii hatujasema, mkewe ndo mchungaji kiongozi hatujasema, kabadilika kutoka uhubiri mpaka uwekezaji hatujasema sasa anaanza kupekuwa siasa zetu! Shame on him. Anatutafuta I promise him atatupata tu.
 
Back
Top Bottom