Mbwana Samatta atajwa kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika 2016

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,399
Shirikisho la Soka barani Africa (CAF) kimetoa orodha ya majina ya wachezaji ambao watawania Tuzo ya Mchezaji Bora 2016 na Tuzo ya Mchezaji Bora 2016 kwa wanaocheza ndani ya bara la Afrika.

Moja ya majina ambayo yametajwa kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora 2016 ni pamoja na mtanzania Mbwana Samatta anayekipiga Genk ya Ubelgiji, akiwa katika orodha ya wachezaji 30 akiwemo Riyad Mahrez, Pierre-Emerick Aubameyang na Kelechi Iheanacho.

Kwa Afrika Mashariki wachezaji ambao wamepata nafasi ya kuwania tuzo hiyo ni Mbwana Samata – Tanzania, Victor Wanyama – Kenya na Dennis Onyango – Uganda.

Orodha ya wachezaji wanaowania Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika 2016

Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika 2016 kwa wachezaji wanaocheza ndani ya bara la Afrika.
 
Hii anaichukua Aubameyang tu

Hamna cha samata, Mahrez wala nan...
Kwq wanaofuatilia ligi za ulaya nadhani wanaelewa nini namaanisha
 
Samatta ni mtanzania mwenzangu na nakubali anavyoipeperusha bendera ya Taifa tunamuombea Mungu aweze kushinda (kwa Mahrez na Aubameyang ni ushindani mkubwa sana kwa Samatta wetu)

Anyways weka link ya kupiga kura kama ipo tumpigie samatta.
 
Kama ni inshu ya kura inakuwa sio uchezaji bora
 
huyo kichuya mnavomkuza,kisa kamfunga yanga..acheni ujinga,ajibu mchezaj,ila umri umeenda,mvivu na anaonekana mtu wa kilevi
Ushaleta akili zako za babu yako mzee akilimali sasa Ajibu umri umeeenda kivipi?,weka cheti chake cha kuzaliwa twende sawa.
 
huyo kichuya mnavomkuza,kisa kamfunga yanga..acheni ujinga,ajibu mchezaj,ila umri umeenda,mvivu na anaonekana mtu wa kilevi
Mkuu.. Ingekua hivyo Kichuya angekua na goli moja tu.. Lakini mpaka sasa jamaa ana goli za kutosha.. Na anaongoza chati ya wafungaji bora.. Ajibu hiyo ni habari nyingine.

Ila kila la heri Mbwana Samata.
 
Back
Top Bottom