Mbunge: Wafanyakazi EWURA wanalipiwa gym USD 200 kwa mwezi

Kwa nini wasiende MAWAZO MAWILI CAMP Tandale kwa MTOGOLE buree kabisa. Ila vyuma vina tofautiaana uzito upande mmoja na mwingine.
 
...hivi kufanya mazoezi kwa faida ya afya ya mwili wako ulipiwe na ofisi? where else this happens??? may be only in Tanzania??? In Tanzania, everything fishy is possible!!

Taasisi nyingi tuu zinawalipia wafanyakazi wao ada za GYMKANA. What is the difference? Hawa badala ya kucheza gofu mchezo ambao hatuna asili nao wamechagua mazoezi ya viuongo.
 
Sidhani km ni tatizo kubwa km wengi tunavyojiaminisha. Suala ni kupima utendaji. Bara la Afrika linakabiliwa na tatizo la kukimbiwa na wataalamu, sasa km tukiendelea kuwapa malipo madogo huenda tukakosa watu wa kusimamia shughuli zetu. Imagine mtu analipwa labda dollar 5000, hiyo 200 ni allowance fulani tu. Kwani mnataka wakurugenzi walipwe kiasi gani? Au vinginevyo wote watakuwa wanasiasa.

...George Kichaka alisema:Either you are with Us or You are With them.
...Hakika naona wewe uko upande wa mafisadi.
 
mkuu ..... nadhani hautambui uwepo wa priority .... je gharama za gym ni muhimu kuliko mahitaji mengine ya umma .... je hao staff wa EWURA hawawezi kuamka asubuhi wakakimbia mchaka mchaka na kuruka kichura chura ili kuokoa gharama hizi kubwa na pesa hizi zikawa allocated kwenye vipaumbele vingine...? think twice

hahaha mkuu LAT hapo kwenye bold umesomeka...au wafanye style ya ULTIMATE au KK Security....wajikusanye uwanjani wapige gwaride!
hivi watumishi wa TISS na wao wanalipiwa GYM manake wamejaa vitambi kwa kwenda mbele!!
 
Taasisi nyingi tuu zinawalipia wafanyakazi wao ada za GYMKANA. What is the difference? Hawa badala ya kucheza gofu mchezo ambao hatuna asili nao wamechagua mazoezi ya viuongo.

MKUU Sijaona faida yake bado, EWURA pamejaa vitambi kibao! bora hiyo hela ingekuwa channeled sehemu nyingine ambayo ni more productive.
 
Wakuu: Jioni hii bungeni; Kuna Mbunge wa Nkasi (CCM). Mh. Kesy amesisitiza kuwa nchi yetu si masikini na kusema kuwa EWURA ( Mamlaka ya kudhibiti nishati na madini) kila mfanyakazi (management) analipwa dolla 200 (zaidi ya sh.300,000/=) kwa mwezi, kwa ajili ya kulipia Gym Ostabey. (tofauti na mshahara) Pesa hiyo hulipwa kwenye hiyo gym. (MD wa pale ni Haruna Massebu)
TBC bungeni. Wanajamvi imekaaje hii?

Yani kama matokeo ya hayo mazoezi ni kuja na 'banning za vidumu katika petrol stations' basi ni upuzi mtupu.. Afadhali wangekua wana tija katika sekta ya nishati/madini tungesamehe matumizi tapanyatapanya kama hayo.
 
Unajua EWURA wanakusanya fedha nyingi sana! Hizi hela wala kazi ya kufanyia hawana na ndiyo maana wanajitahidi kubuni namna ya kuzitumia. Wanakwenda safari za nje sana lakini bado fedha ni nyingi!!! Ingetakiwa hizo fedha ziende serikali kuu itumike kuwalipa mishahara walimu na wafanyakazi wa idara za afya, kilimo, nk.
 
Kuna shule hapo Dsm watoto wanaenda na viroba chuleni kwa ajili ya kukalia dalasani,cha kuchangaza kuna watu wanalipiwa fedha ya Gym. Inasikitisha sanaaaaa,tena inauma mno.
 
Wonders shall never cease! EWURA si mamlaka inayookoteza fedha toka Tanesco (miongoni mwa maeneo mengine)? Nini maana ya jeuri na ufujaji huu? WaTz jiulizeni kama hiyo EWURA ni kwa faida ya nani? Scrap and send it to hell
 
Wakuu: Jioni hii bungeni; Kuna Mbunge wa Nkasi (CCM). Mh. Kesy amesisitiza kuwa nchi yetu si masikini na kusema kuwa EWURA ( Mamlaka ya kudhibiti nishati na madini) kila mfanyakazi (management) analipwa dolla 200 (zaidi ya sh.300,000/=) kwa mwezi, kwa ajili ya kulipia Gym Ostabey. (tofauti na mshahara) Pesa hiyo hulipwa kwenye hiyo gym. (MD wa pale ni Haruna Massebu)
TBC bungeni. Wanajamvi imekaaje hii?

Kulipiwa Gym sio mbaya swala hapa hiyo Gym ni bei mbaya kwa nini wao EWURA pamoja na mashirika mengine wasijenge ya kwao kukidhi mahitaji ya wafanya kazi wao? Huu ni ufisadi na huo ni mradi wa Ufisadi ukiangalia sana utawakuta wakina RA, Chenge, EL et al
 
Watumishi wenyewe hata vijana wadogo wamejaa vitambi tu. Tatizo la ewura ni uwepo wa fedha nyingi. Wanakusanya asilimia 1 ya mauzo ya mafuta, gas, umeme na maji. Wameelemewa na hela nyingi na ndiyo maana wamekuwa wakisafiri sana nje ya nchi lakini bado haziishi. Kilichobaki sasa ni kutafuta namna nyingine ya kutumia hela. Serikali ingekuwa inawajali wananchi wake ingepunguza asilimia ya makato ili kuwapunguzia mzigo wananchi lakini wao wapo kimya tu.
 
Sidhani km ni tatizo kubwa km wengi tunavyojiaminisha. Suala ni kupima utendaji. Bara la Afrika linakabiliwa na tatizo la kukimbiwa na wataalamu, sasa km tukiendelea kuwapa malipo madogo huenda tukakosa watu wa kusimamia shughuli zetu. Imagine mtu analipwa labda dollar 5000, hiyo 200 ni allowance fulani tu. Kwani mnataka wakurugenzi walipwe kiasi gani? Au vinginevyo wote watakuwa wanasiasa.
Wataalam wanakimbia Afrika mara nyingi ni kwa sababu ya nchi kutoendelea - yaani kua na maisha ya kijima. Mimi naona bora kufanya kazi mjini Dar kwa mshahara wa milioni 3 kuliko kijijini mfano Newala kwa milioni 5. Bora nilipwe milioni 3 na kuishi Mikocheni kuliko milioni 4 na kuishi Manzese nk. Fikiria huduma- barabara, usafi wa mazingira, matibabu, shule, internet, etc etc, pia fikiria watu wanaokuzunguka kule Newala kijijini.
Vema mikanda ikakazwa na hiyo pesa ikatumika vema ili kuinua uchumi wetu na hali ya maisha kwa ujumla - tukifikia huko hamna atayekimbia hii nchi. Kutoa mapesa ovyo eti kuwavutia, ndiyo hivyo baadaye watu kama Mkapa nk wanaenda kujenga mahoteli SA ambako wanaona watakua na maisha ya hali ya juu. EWURA sio private co.
 
Back
Top Bottom