Mbunge: Wafanyakazi EWURA wanalipiwa gym USD 200 kwa mwezi

POMPO

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
6,690
2,400
Wakuu: Jioni hii bungeni; Kuna Mbunge wa Nkasi (CCM). Mh. Kesy amesisitiza kuwa nchi yetu si masikini na kusema kuwa EWURA ( Mamlaka ya kudhibiti nishati na madini) kila mfanyakazi (management) analipwa dolla 200 (zaidi ya sh.300,000/=) kwa mwezi, kwa ajili ya kulipia Gym Ostabey. (tofauti na mshahara) Pesa hiyo hulipwa kwenye hiyo gym. (MD wa pale ni Haruna Massebu)
TBC bungeni. Wanajamvi imekaaje hii?
 
Wakuu: Jioni hii bungeni; Kuna Mbunge wa Nkasi (CCM). Mh. Kesy amesisitiza kuwa nchi yetu si masikini na kusema kuwa EWURA ( Mamlaka ya kudhibiti nishati na madini) kila mfanyakazi (management) analipwa dolla 200 (zaidi ya sh.300,000/=) kwa mwezi, kwa ajili ya kulipia Gym Ostabey. (tofauti na mshahara) Pesa hiyo hulipwa kwenye hiyo gym. (MD wa pale ni Massabo)
TBC bungeni. Wanajamvi imekaaje hii?

Haruna Masebu ....
 
Amejaribu kuashiria tatizo lipo wapi? Ni amount inayolipwa au ni huko kulipiwa gym?
 
Amejaribu kuashiria tatizo lipo wapi? Ni amount inayolipwa au ni huko kulipiwa gym?

Mkuu SMU ina maana wewe huoni tatizo hapo? Yule ****** alisema mbayumbayu hawezi kuwalipa minimum wage ya laki 3 kumbe kuna wengine kati ya hao hao mbayumbayu kutokana na kodi hizo hizo na huyo huyo ****** anawalipia gym peke yake amount hiyo hiyo. Kweli jamani hapo huoni tatizo? You cant be serious!
 
Sikuwa na maana hakuna tatizo au sioni tatizo. Inawezekana tatizo ninaloliona mimi ni tofauti na alilokuwa analilalamikia mbunge....ndio maana nilikuwa nauliza huyo mbunge amehoji nini hasa?
 
Sioni ubaya wowote kama mmekubaliana na mwajiri wako kabla ya kuajiriwa. Gym siyo starehe na ni nzuri kwa afya! Hiki ni kitu cha kawaida je wabunge wanapewa mangapi kama haya???????
 
Kuwalipia GYM sio kitu kibaya, inasaidia kuboresha afya na kuongeza ufanisi, ili mradi wawe wanalipa kwa ajili ya wale wanaoenda kweli. Lakini ni GYM ipi hiyo $200? Colosseum GYM ni $125 kuna zaidi ya ile kweli?
 
Mkuu SMU ina maana wewe huoni tatizo hapo? Yule ****** alisema mbayumbayu hawezi kuwalipa minimum wage ya laki 3 kumbe kuna wengine kati ya hao hao mbayumbayu kutokana na kodi hizo hizo na huyo huyo ****** anawalipia gym peke yake amount hiyo hiyo. Kweli jamani hapo huoni tatizo? You cant be serious!

Kwamimi tatizo kubwa ni amount! Jimu Elfu hamsini kwa mwezi ingekuwa si mbaya!! Mazoezi yanaweza kusaidia watu wafanye kazi kwa nguvu/akili zaidi.....boresha afya ya wafanyakazi!1
 
Sioni ubaya wowote kama mmekubaliana na mwajiri wako kabla ya kuajiriwa. Gym siyo starehe na ni nzuri kwa afya! Hiki ni kitu cha kawaida je wabunge wanapewa mangapi kama haya???????

Sijajua kama wabunge wana posho ya gym. Duu, kwanza mbunge wa kwetu hata gym hakuna teh teh kazi kweli kweli
 
Wakuu: Jioni hii bungeni; Kuna Mbunge wa Nkasi (CCM). Mh. Kesy amesisitiza kuwa nchi yetu si masikini na kusema kuwa EWURA ( Mamlaka ya kudhibiti nishati na madini) kila mfanyakazi (management) analipwa dolla 200 (zaidi ya sh.300,000/=) kwa mwezi, kwa ajili ya kulipia Gym Ostabey. (tofauti na mshahara) Pesa hiyo hulipwa kwenye hiyo gym. (MD wa pale ni Massabo)
TBC bungeni. Wanajamvi imekaaje hii?

EWURA ( Mamlaka ya kudhibiti nishati na madini) wanatumia nguvu za mwili nini kudhibiti? Kwa hiyo kuanzia secretary mpaka mkurungenzi wanajaza miili kwa kazi ya kudhibiti. Nafikiri hiyo mamlaka imekosa kazi na ndo maana wanamua kwenda Gym wote na familia zao. Halafu Tanzania nchi masikini! No, watanzania wengi ndo masikini. Lakini yana mwisho yote haya. Sisi tunahagaika pesa ya kununulia dawati kwa ajili ya watoto wetu wa shule za kata, nyie mnagawana hela za madini yetu kwa ajili kujaza misuli, ili mtutishi?
 
Sioni ubaya wowote kama mmekubaliana na mwajiri wako kabla ya kuajiriwa. Gym siyo starehe na ni nzuri kwa afya! Hiki ni kitu cha kawaida je wabunge wanapewa mangapi kama haya???????

mkuu ..... nadhani hautambui uwepo wa priority .... je gharama za gym ni muhimu kuliko mahitaji mengine ya umma .... je hao staff wa EWURA hawawezi kuamka asubuhi wakakimbia mchaka mchaka na kuruka kichura chura ili kuokoa gharama hizi kubwa na pesa hizi zikawa allocated kwenye vipaumbele vingine...? think twice
 
  • Thanks
Reactions: Obe
Kwamimi tatizo kubwa ni amount! Jimu Elfu hamsini kwa mwezi ingekuwa si mbaya!! Mazoezi yanaweza kusaidia watu wafanye kazi kwa nguvu/akili zaidi.....boresha afya ya wafanyakazi!1
Jimu siyo baya lakini chanzo cha pesa hicho. Pesa za madini yetu hizo ndo zinatumika hivyo. Na nafikiri hawa watu wanamishahara mikubwa. Hebu mwenye data aziupload hapa tuwajue zaidi hawa wabinfsi na wezi wa madini yetu kwa kushirikiana na America
 
mazoezi ni muhimu lakini sio mpaka uende GYM bwana unaweza kufanya mwenye nyumbani, wawanunulie DVD si wana majumba makubwa wafanye ndani mwao, uwezi kutumia pesa ya nchi kama tanzania kumlipia mtu GYM, kwanza mbona hao wakurugenzi wenyewe hawaendani na kusema wanafanya mazoezi, wanamatumbo na miili ya ovyo kuliko sisi tunaolipia kodi, mbona wenzitu wanafanya mazoezi ya kukimbia na kutembea na mbwa. hawa ni wezi tu wanalipata mishahara mikubwa kijanja, wala hiyo hela haiendi kokote, au hiyo GYM ni yao vigogo na hiyo ni njia ya kupata wateja wa uhakika
 
Kuwalipia GYM sio kitu kibaya, inasaidia kuboresha afya na kuongeza ufanisi, ili mradi wawe wanalipa kwa ajili ya wale wanaoenda kweli. Lakini ni GYM ipi hiyo $200? Colosseum GYM ni $125 kuna zaidi ya ile kweli?

Ningemuona mbunge yupo makini sana kama hoja yake ingeanzia na malipo yao wao kama wabunge. Pili angekemea huu mchezo wa kutumia forex kulipia local services, huu ni wizi wa wazi na uharibifu na uhujumu uchumi wetu. Kwa nini local services ziwe charged on foreign currencies while we have our our currency Tshs?. This is nothing but transfering the foreign translation risks to the consumers. Where is BoT on this illegal and unethical hedging practices?.
 
walazimishwe kuzirudisha wanaruhusu watu wachakachue mafuta magari yanaharibika umeme haushikiki wao wanatumia mshahara wa mwalimu wa zaidi ya miaka kumi kazini kwa mwezi kucheza kwenye vyuma kwa nini wasitembee kama wanataka kufanya mazoezi kodi zetu haziwezi kuwapunguza vitambi na ****** yao
 
Back
Top Bottom