Mbunge wa Ushetu Emmanuel Cherehani aipongeza Serikali kufuta Hifadhi ya Taifa ya Kigosi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani ameipongeza serikali kufuatia juhudi za kutatua changamoto za migogoro ya ardhi baada ya kufutwa kwa Hifadhi ya Taifa ya Kigosi ambayo ilizuia kufanyika kwa shughuli za kibinadamu ikiwemo ufugaji na kuwakosesha wananchi wa maeneo jirani kufanya shughuli endelevu za kiuchumi ndani ya hifadhi hiyo.

Mheshimiwa Cherehani ameiomba serikali kuwasajili wananchi ambao watafanya shughuli endelevu katika eneo hilo husasan wafugaji wa nyuki pamoja na wavuvi ili waweze kutambulika na kurahisisha usimamizi mzuri wa shughuli hizo.

Itakumbukwa Hifadhi hiyo imesababisha kukosekana kwa fursa hizo kwa wananchi ambapo Serikali imeona ni vyema kufuta Hifadhi ya Taifa Kigosi ili kuruhusu kuanzishwa kwa Hifadhi ya Msitu Kigosi ambao utasimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

Sheria ya misitu sura 323 ina ruhusu kufanyika kwa shughuli za kiuchumi ndani ya Hifadhi za Misitu kwa kuzingatia matakwa ya uhifadhi na utaratibu maalum.

Untitledqaswq.jpg
 
Back
Top Bottom