Mbunge wa Ludewa (Filikunjombe) ana ushahidi wa Barua ya Jairo kusimamisha mradi wa umeme Liganga!

Afu jambo la ajabu mtu kama huyo anapewa likizo ya malipo...duh! Kweli nchi inaliwa na wachache!!
 
JAIRO ALIKUWA MSAAIDIZI KIPENZI WA JK..

Mh Filikunjombe aksante kwa kuonyesha Utaifa mbele zaidi ya UCCM.... endelea kulitetea Taifa, history itakuenzi.

Kama tunavyofahamu jamaa alikuwa msaidizi kipenzi wa JK, haya yaliyotokea na hatua hakuna zinazochukuliwa..., sasa tutegemee nn? hapa tutaendelea kupata newz zake tuu.., inavyoelekea yatakuja mambo mengi tuu yaliyotendeka chini yake....,
haingii akilini kama JK alikuwa hafahamu nn Jairo anafanya pale wizara ya madini na nishati kama katibu mkuu.

Wizara ya Madini na Nishati ni Wizara nyeti hapa Bongo...!, JK kusema hana ukaribu nao haingii akilini hata kidogo...!, ni wizara inayosimamia utajiri wa nchi yetu!

 
Maamuzi ya nchi yetu yanaamuliwa na wachache wasio na akili
kaza buti mh. Tetea jimbo lako la rudewa bila kujali uozo wa chama
chako wachome waelewe
 
Inawezekana vipi katibu mkuu kusimamisha mradi bila waziri wake kujua?
Kama kweli Mi naona wizara nzima imeoza.

Na vipi huo ushahidi ameshakabidhi kwa spika au kwenye vyombo husika kwa ajili ya uchunguzi zaidi na uthibitisho wa kauli yake.

Wewe vipi? Unaambiwa katekeleza agizo la rais!!!!!!
 
Maamuzi ya nchi yetu yanaamuliwa na wachache wasio na akilikaza buti mh. Tetea jimbo lako la rudewa bila kujali uozo wa chamachako wachome waelewe
Mbona chuma inaondoka kule liganga kila kukicha na yeye yupo kimya! Na ndo kinala wa kutetea uozo wa chama!
 
Inabidi utokwe na chozi kama vile umefiwa, wakati mwingine hata kusikia hizi habari sitaki maana nitapandwa na hasira na kujikuta nikiishia selo..
 
Ana bahati mbaya au wenzake wamemtega?maana nasikia alikuwa mteule wa nafasi katibu mkuu kiongozi!!!!analia kwa mengi bana pole sana Jairo
 
Jairo alikuwa anatekeleza sera za CCM ambayo ndiyo imepewa mamlaka ya kuongoza dola. Maamuzi yote aliyofanya Jairo yalikuwa ni utekelezaji wa sera za chama tawala. Msimtoe akawa mbuzi wa kafara.

So turudi tukae na tujadili - je ni nani aliyeiweka CCM madarakani - ni sisi. kwa hiyo ni sisi wenyewe tujilaumu kwa kufanya hivyo. Hata ukimfunga Jairo, Mwingine atakayekuja naye atafanya hayo hayo sababu ni MFUMO.
 
Hapa sijapata picha vizuriii. Kwamba mradi ulikuwa utekelezwe na pengine mchuzi ulitengwa DJ akau cancel.
 
Rip filikunjombe....daima tutakumbuka juhudi zako baba...umetuacha umeenda peke yako...
 
Back
Top Bottom