Mbunge wa Ludewa (Filikunjombe) ana ushahidi wa Barua ya Jairo kusimamisha mradi wa umeme Liganga!

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,674
Kituko kingine cha Jairo akiwa Katibu wa Madini aliandika barua kipindi cha mwezi wa tatu [3] mwaka huu kusimamisha mradi wa umeme wa Liganga. Anasema sababu za kusimamishwa kwa mradi huo wa Umeme ni mambo binafsi na faida binafsi za bwana David Jairo.

Bwana Filikunjombe alikuwa akichangia hoja ya Wizara ya Viwanda na biashara. Anasema bila umeme wananchi wa Ludewa wataendesha vipi shughuri zao huku vijana wao wamefunga saloon zao kwa kukosa umeme.

Kawasilisha mchango wake kwa kupigilia msumari kuhusu bwana David Jairo akiwa na barua hiyo ya kukatisha kuendelea kwa mradi huo wa umeme kwa sababu zake binafsi.

Kwa mtindo huo kweli wametufikisha pabaya

Nawasilisha
 
kama ushahidi anao kwa nini asifikishwe mahakamani?na cag akamilishe uchunguzi haraka tumechoka na viongozi wabovu,kaza buti Fikikunjombe kwa manufaa ya wananchi wako.
 
kumbe naye huwa anaona mbali vipi kuhusu madini kijijini mwake? nasikia wananchi wako, wako hoi sana, nia madini yamewazunguka kila upande, sijui wanasubiri yakue
 
Inawezekana vipi katibu mkuu kusimamisha mradi bila waziri wake kujua?
Kama kweli Mi naona wizara nzima imeoza.

Na vipi huo ushahidi ameshakabidhi kwa spika au kwenye vyombo husika kwa ajili ya uchunguzi zaidi na uthibitisho wa kauli yake.
 
swala hapa ni ni mkuu wa kaya ndio tatizo....anawakumbatia sana......
 
Issue hapo si Jairo pekee kuanzia juu mpaka chini waondoke madarakani jairo angetoa wapi ujasiri kama hayuko pamoja na waziri wake na waziri hasingeacha upupu uwepo kwenye wizara yake kama hayuko pamoja na mkuu wao wote tumewachoka watuiachie nchi yetu jamani
 
Jairo, Ngeleja na Naibu wake lao moja tu tena wakitekeleza magizo ya mkubwa wao...JK alitembelea kila wizara sasa inakuaje haya mambo yatokee sasa?

Hivi ile semina elekezi ilikuwa na lengo gani? Tunataka maamuzi magumu kama ya CHEDEMA yatekelezwe kama haya mambo vinginevyo CHADEMA ndio chama pekee kitakacholeta mapinduzi ya kweli hapa Tanzania..
 
Nimemsikia mwishoni akiongelea hili...ngoja tuone danadana za JK na serikali yake.
 
Inawezekana vipi katibu mkuu kusimamisha mradi bila waziri wake kujua?
Kama kweli Mi naona wizara nzima imeoza.

Na vipi huo ushahidi ameshakabidhi kwa spika au kwenye vyombo husika kwa ajili ya uchunguzi zaidi na uthibitisho wa kauli yake.
Ni pamoja na rais...
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Ni faraja kuona hata wabunge wa ccm wameacha utoto na ushabiki a kikada na sio maslahi ya taifa!hakika nao wameanza kuibua hoja nzito zenye mashiko na maslahi ya taifa na wanaungana na wenzao pasipo kujali itikadi ila wanajali utaifa na maendeleo ya wengi!bravoo bravoo
 
Inawezekana vipi katibu mkuu kusimamisha mradi bila waziri wake kujua?
Kama kweli Mi naona wizara nzima imeoza.

Na vipi huo ushahidi ameshakabidhi kwa spika au kwenye vyombo husika kwa ajili ya uchunguzi zaidi na uthibitisho wa kauli yake.

Chama lekeleke huzaa serekali lekeleke!
 
Inawezekana vipi katibu mkuu kusimamisha mradi bila waziri wake kujua?<br>

Back
Top Bottom