Mbunge wa CUF Mama Mwatuka pokea pongezi zangu!

Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,813
11,126
MBUNGE wa Viti Maalumu wa CUF, Clara Mwatuka, amejitolea kusomesha kidato cha kwanza hadi cha nne watoto 20 kutoka kata 34 za wilayani hapa kuanzia mwaka huu.

Kwa kata hizo 34 za wilaya ya Masasi, inamaanisha kwamba, mbunge huyo atasomesha wanafunzi 680.

Ada ya kila mtoto kwa shule ya Serikali ni Sh 20,000, hali ambayo itamfanya mbunge huyo kulipa zaidi ya Sh milioni 13.6 kwa mwaka.

Mbunge huyo aliyewania ubunge wa Masasi, lakini kura zake hazikutosha mbele ya Mariam Kasembe wa CCM, ameingia bungeni baada ya CUF kumteua, akiwa mbunge pekee wa kuteuliwa kutoka Kanda ya Kusini.

Akizungumza na HABARILEO Jumapili kijijini kwake Nanganga, wilayani hapa jana, alisema dhamira yake ni kuziba pengo baina ya matajiri na masikini na hilo litawezekana iwapo watoto wa masikini watawezeshwa kupata elimu na kwa kuanzia atasomesha watoto 680 kwa wilaya nzima.

“Nimetoa maelekezo kwa watendaji wa kata kuleta majina ya watoto 20 waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwakani, ambao wazazi wao hawana uwezo … katika wilaya yetu kuna kata 34, hivyo jumla ya wanafunzi wote watakuwa 680,” alisema Mwatuka.

Aliongeza “hapa naomba nieleweke, si kuwalipia ada bali nitawasomesha kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne kwa kuwatimizia mahitaji yao yote ya shule ikiwa ni pamoja na sare, kalamu na madaftari, wazazi au walezi watanisaidia chakula, malazi na mavazi ya nyumbani,” alisema.

Alisema uzoefu unaonesha watoa misaada wengi kwa watoto wa masikini, husaidia mwaka wa kwanza na kisha huwatelekeza hali inayosababisha watoto hao kukatisha masomo yao, kitendo ambacho amekilaani.

“Unapoamua kuwasaidia, basi wasaidie kwa miaka yote na kwa mahitaji yao yote ya shule, ukisema umsaidie mwaka huu basi mwaka kesho ataacha shule na hivyo msaada wako utakuwa hauna maana,” alifafanua Mwatuka.

Alibainisha kuwa iwapo watoto wa masikini hawatawezeshwa kupata elimu, ndoto za kuleta usawa katika kumiliki rasilimali za nchi haziwezi kufikiwa na kwamba mizizi ya ubepari itazidi kunawiri na kuhatarisha amani ya Taifa na kwamba hatua hiyo ni mwanzo kutokana na kuwa mwakilishi wa mikoa ya Lindi, Mtwara na wilaya ya Tunduru na Namtumbo mkoani Ruvuma.

Alisema ameamua kuanza na wilaya ya Masasi, kutokana na yeye mwenyewe kuwa mkazi wa wilaya hiyo hata hivyo jitihada zake za kuwakomboa wananchi wa eneo lake la kuongoza zitaenea wilaya zote 14, huku akiahidi kila mwezi kutembelea wilaya moja.

Kwa nyakati tofauti baadhi ya wanafunzi, wazazi na wananchi wa wilaya ya Masasi wameelezea uamuzi wa mbunge huyo kuwa ni wa aina yake, kwani wabunge wa majimbo, viti maalumu waliopita, wameshindwa kufanya hivyo.
 
Msaada wa elimu kwa watoto 680 kwa mwaka si mdogo.

Tungefurahi kusikia anatoa msaada wa elimu ya juu pia japo kwa mwanafunzi mmoja kutoka jimboni kwake.
 
hili pia kulitekeleza si dogo

nnangoja kama kweli ataweza kulifanikisha maana mmmh
 
Msaada wa elimu kwa watoto 680 kwa mwaka si mdogo. Tungefurahi kusikia anatoa msaada wa elimu ya juu pia japo kwa mwanafunzi mmoja kutoka jimboni kwake.
Lakini yeye kaanza na hao na level inayofuata inaweza kufanywa na mtu mwingine
 
Hongera Mama Mwatuka,wajenga nchi ni wananchi na wafuja nchi ni wananchi.
 
Tatizo hawa walengwa watajitokeza? Nasikia wakati akiwa rais, Mkapa alikuwa na kitu kama hicho lakini hakuna mtu aliyejitokeza.
 
Mungu akulipe mama kwa imani yako hiyo, kwani ndo mjuzi wa kulipa zaidi kuliko chochote.
Hila humu jf panatia kinyaa, angekuwa ni mwanaChadema ndo kafanya hivyo ungeona jinsi ambavyo angemwagiwa sifa, SHAME ON YOU.
 
Nampa hongera sana bila ya kujali itikadi za Chama kwani kuna wabunge wengi tu kutoka CUF na walioshinda kwa kura za wananchi lakini hawajaaliwa kufanya ibada hiyo,Ila aliefanya hivyo ajue tu Mwenyezi Mungu hakopeshwi atakulipa tu kwa wema wako huo.
 
Wabongo bwana, mtu at least kajitolea kwa kuanzia, then ntu anasema aongeze at least mmoja for higher education !!

Mimi pia nampongeza, ni mwanzo mzuri na I wish wabunge wote wangewekeza ktk elimu kwa style hii. Ni sawa na yule mbunge aliyejitolea siku moja ktk mwaka kufanya usafi jijini Mwanza. Ni mwanzo mzuri, na hope utaweza kufungua milango kwa wengine kuendeleza hapo- maybe a week, and later one day a week ktk kila mtaa, kata, tarafa ect...

Kwa karne hii, ningependa kuona more creativity hasa hawa wabunge vijana, ambao wengi naamini wamepata exposure ya kutosha. Sisi wenye kuwajua hawa, tuwasaidie. Mambo ya kujionyesha na kuwa kimbelembele na mbio za mwenge, au ugeni wa viongozi wa kitaifa majimboni yamepitwa na wakati. Na sisi humu, tuwatafute wabunge ktk majimbo yetu, au wale ma-mate wetu ambao ni wabunge sasa na tuwa-challenge na kuwapa ideas, including source za info na resource mbalimbali badala ya kila siku kulalama humu na netini weee...
 
hilo si la kupongeza bali ni inputs za kutayarishia sera na ni kielelezo tosha kuwa mtu akiwa mbunge basi si mwenzako! wakati kuna watu hata mtoto mmoja kusmesha ni mshikemshike, yeye anawasomesha wote hao! so sio yeye bali ni siasa ndiyo inayowasomesha kama angekuwa ni yeye basi angefanya hivyo hata kabla hjawa mbunge
 
Piganieni kutengeneza uwezo kwa kila mwananchi kusomesha mtoto wake, siyo kugeuka wafadhili ok?

Haya mambo ya kutoa ufadhili ni kuendekeza tabia inayokua sana hapa nchini ya kuomba msaada kwa kila jambo ok?

Hongera kwa moyo wako wa upendo lakini tupiganie zaidi kuwezesha watu na si kuwapa misaada
 
Mbunge wa cuf ameonyesha njia na mfano mzuri wa kuigwa! Sasa tunangoja kusikia na wabunge wa cdm nao wajitokeze kusaidia watoto masikini wasio na uwezo! Au na hili pia mtagoma? Ktk sera yenu cdm ni kutoa elimu bure! Sasa anzeni kwanza ktk serikali zenu za mitaa mnazoongoza kwa kutoa elimu bure! Au mpaka rais atoke chadema ndio mtasomesha watoto bure!!!

Siasa za bla bla zimepitwa na wakati sasa ni vitendo hongera cuf kwa kuonyesha mfano! Kwanza kwa maandamano ya katiba na sasa wabunge wenu kujitolea kusomesha watoto masikini!
 
nijuavyo CUF mara nyingi huanza mambo mazuri halafu huwashinda nnjiani

kuna mwaka walianzisha shirika la kununua nafaka za wakulima kwa bei ya angalau kuliko ya walanguzi lkn ule mpango haukuwa endelevu kulikoni sijui
 
hongera sana mama. ni moyo mzuri. bernad Membe wa mtama ye anachonga macheni tu? uku akisema of kozi thisi kantri is very pua!
 
Mungu akulipe mama kwa imani yako hiyo, kwani ndo mjuzi wa kulipa zaidi kuliko chochote.
Hila humu jf panatia kinyaa, angekuwa ni mwanaChadema ndo kafanya hivyo ungeona jinsi ambavyo angemwagiwa sifa, SHAME ON YOU.

Jina lenyewe Ngwendu? Ngwendulile
 
hilo si la kupongeza bali ni inputs za kutayarishia sera na ni kielelezo tosha kuwa mtu akiwa mbunge basi si mwenzako! wakati kuna watu hata mtoto mmoja kusmesha ni mshikemshike, yeye anawasomesha wote hao! so sio yeye bali ni siasa ndiyo inayowasomesha kama angekuwa ni yeye basi angefanya hivyo hata kabla hjawa mbunge

Sasa ameonyesha tofauti yake,kabla alikuwa hana kitu,amejaaliwa kuukwaa ubunge japo wa kuteuliwa ,ameweza na ndio hio tofauti na akina Slaa ,sidhani kama Slaa amewea kumgaia mtu japo shilingi ,ingawa aliitetea hoja ya kutaka kupunguziwa mishahara kwa wabunge,angefanya kama huyu basi ingekuwa asavali.
 
Back
Top Bottom