Mbunge wa Bahi (CCM) ashikiliwa na polisi kwa kuomba rushwa

Naam,

Nimeiboresha title na content naona mwenzetu amesahau kama hii ni JF.

Lakini, kiasi chenyewe inadaiwa hakifikii hata 5mil, achilia mbali 7mil. What a shame?
we unaona kidogo hicho, piga msahesabu akikusanya kila halmashauri anaondoka na ngapi?
 
Hebu nisaidie mtoa taarifa huyu bwana aliomba rushwa ili amfeve nini mtoa rushwa mwongozo tafadhali...........? au ili aifanyie nini halmashauri husika? kwani milioni saba si haba naamini mtoa rushwa hii alitegemie fever flani ambayo ni nini...? na mpokeaji naye anacapacity gani kutimiza hilo?
 
Majasho na wafanyakazi wa TAKUKURU: alafu unaanza kwa kusema posho za wabunge hazitoshi???kweli???we TAKUKURU walipwa bei gani??zinakutosha(mpaka uone za wabunge hazitoshi)??..boss wenu TAKUKURU ..Dr.Hosea aliwahi kunukuliwa kwenye zile dossier za wikileaks kuwa aliwahi kulalamika kutishiwa maisha na ma boss wake ktk utendaji wake...hili wala si siri...linajulikana kabisa kuwa Hosea anaingiliwa katika utendaji wake na boss wake..

.Angalizo kwenu kina Majasho et al (wafanyakazi wa TAKUKURU):Kwanini mnakubali kufanya kazi kwa maslahi ya ma boss wenu??????...kwani nyie mmeajiriwa ili kuwafurahisha ma boss wenu????sheria za kazi zinamlinda kila mtu anaeonewa kutokana na utendaji wake....kama unaona unasumbuliwa kwasababu ya kuwakamata wakubwa si unasema!!!sheria za kazi ziko wazi kabisa kwa wanaoonewa hata na wakubwa zao...sema tatizo la TZ ni uoga wa kuchukua maamuzi...na hili ndio limetufikisha hapa tuiko kama nchi...Kama nyie mliopewa dhamana ya kuwakamata hawa wala rushwa mnakuwa na woga wa namna hiyo sasa nani ataifanya hiyo kazi????....

NI lini tutaona TZ angalau mmemkamata for real mla rushwa mkubwa na TZ tukaona amefungwa jela????..hawa wanasiasa kila leo wanakula rushwa.....kwenye chaguzi za ubunge wanakula rushwa...kila leo wanakula rushwa hawa....lakini kamwe hatuoni mnawakamata...kumbe nyie mmekuwa mnafanya kazi kwa maslahi ya ma boss wenu????..kweli inasikitisha sana......kumbe sasa rushwa itaishaje TZ???yaani mpaka wakubwa wakosane ndio nyie mfanye kazi mliopewa na watanzania???..kweli???....

Sources(for your reading):
 
Aibu kwake huyo mheshimiwa! Ameshajiweka pabaya kisiasa, lakini tusishangae tukisikia akiambiwa na magamba wenzie kuwa hiyo ni ajali ya kisiasa tu au upepo ambao utavuma kisha utapoa hivyo asiwe na wasiwasi.
 
mbna TRA wana mshahara mkubwa lkn wanakula rushwa. kula rushwa ni hulka/tabia ya mtu na si vinginevyo
 
we unaona kidogo hicho, piga msahesabu akikusanya kila halmashauri anaondoka na ngapi?
Huyo badwell alishachukua rushwa halmashauri ya rufiji na mafia
Halmashauri hizo kwenye kikao cha kamati yao alhamis hii wamerudishwa inaonekana badwel hakuwapa wenzie wakurugenzi hao wanalalamikia sana
 
hakuna msafi ndani ya ccm

nimeipenda hii, hawa ccm wameingia kwa rushwa madarakani tangu raisi wao mpaka mtendaji wao wa kijiji, hakuna msafi ccm, msekwa alliba twiga akawapeleka ulaya mpaka leo kimya, jk na best ake el walicheza dili la richmond mpaka leo kimya, zambi alitajwa na kafulila wakapotezea, leo omar badwel tap kanasa wasivokuwa na aibu ataachiwa huru.
Jamani tuikatae ccm, shime watanzania huu mfumo fisadi uloasisiwa na ccm lazima tuukatae, tuwa[ige chini hawa wezi
 
badwel-omary_thumb.jpg
Hebu mwanangalieni huyu mla rushwa macho yake yalivyokaa kiwizi
 
  • Thanks
Reactions: ADK
''Rushwa ni adui wa haki ,sitatoa wala kupokea rushwa".
Ahadi ya mwana TANU isiyo na uzito tena kwa wengi wa wana CCM wa zama hizi..
 
Kumbe ni tuhuma..! Nilidhani kashikwa nazo mkononi....du.!???
Mkuu Negembo hata ukikamatwa unakata kichwa cha mtu inakuwa ni tuhuma hadi utakapohukumiwa na mahakama! Hivyo hata kama amekamatwa red handed akichukuwa bulungutu la mihela inakuwa ni tuhuma hadi mahakama itakapomtia hatiani. Mkuu ndio utawala wa kisheria huo vinginevyo angekamatwa moja kwa moja akapelkwa segerea kutumikia kifungo lakini tunasema lazima apate haki na haki inapatikana mahakamani.
 
Last edited by a moderator:
Wabunge wetu wanatutia mashaka makubwa. Ikifikia oversight institutions zinachukua rushwa basi ujue nchi imeoza. Kama mbunge anayetumwa na wananchi kwenda kuisimamia serikali anatuhumiwa kuwageuka wananchi na kujichukulia rushwa basi hiyo ni hatari kubwa.

Sijui kanuni za bunge zinasemaje lakini ningefurahi kama zingekuwa kama sheria za utumishi kwamba ukiwa na kesi ya jinai basi usiwe kazini hadi kesi yako itakapoisha. Basi huyu muungwana naye angesimama kuhudhuria shughuli za bunge hadi atakapopata haki yake mahakamani.
 
Mkuu Negembo hata ukikamatwa unakata kichwa cha mtu inakuwa ni tuhuma hadi utakapohukumiwa na mahakama! Hivyo hata kama amekamatwa red handed akichukuwa bulungutu la mihela inakuwa ni tuhuma hadi mahakama itakapomtia hatiani. Mkuu ndio utawala wa kisheria huo vinginevyo angekamatwa moja kwa moja akapelkwa segerea kutumikia kifungo lakini tunasema lazima apate haki na haki inapatikana mahakamani.

Kimbunga nashukuru kwa shule ulonipa; kazi njema eeh...!
 
Last edited by a moderator:
Watu wanapopotosha ukweli, nilivyosikia mimi ni kuwa Badwel ndiye aliyewajulisha TAKUKURU kuwa kuna watu wanataka kumhonga na akawapa saa na mahala walipoahidiana kukutana. Sasa vipi tena kibao kigeuzwe kwake?
 
Watu wanapopotosha ukweli, nilivyosikia mimi ni kuwa Badwel ndiye aliyewajulisha TAKUKURU kuwa kuna watu wanataka kumhonga na akawapa saa na mahala walipoahidiana kukutana. Sasa vipi tena kibao kigeuzwe kwake?

Itajulikana mahakamani. Hivyo unataka kutuambia kwamba TAKUKURU wamemgeuka Mbunge?
 
Back
Top Bottom