figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,895
Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari afikishwa Mahakamani.
Taarifa kutoka Arusha zilizotufikia hivi karibuni ni kuhusu Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru.
Habari ambazo hazijathibitika zinadai kuwa, Nassari anakabiliwa na tuhuma za shambulio analodaiwa kulifanya kwa aliyekuwa Mtendaji wa Kata ya Makiba mwaka 2014. Mtendaji huyo bado hajatajwa jina lake.
========
Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru akisubiri kusomewa shitaka linalomkabili.
Akizungumza na MCL Digital leo Jumanne Februari 6,2018, Nasari amesema jana alikwenda Kituo cha Polisi Usa River kufuatilia silaha yake iliyochukuliwa na askari wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014.
Nassari amesema alipofika polisi alielezwa kuwa ana kesi ya kumshambulia mtendaji kosa analodaiwa kutenda mwaka 2014 .
Sheki Mfinanga ambaye ni wakili wa Nassari amesema hajui mteja wake anakabiliwa na shtaka gani.
"Jana walisema alishambulia lakini hatujui leo anashitakiwa kwa kosa gani ndiyo tunasubiri," amesema.
Chanzo: Mwananchi