Mbunge: Vibaka walinikaba hivi...... Apigwa Salender Bridge; Nilidhaini kulikuwa na CAMERA POLICE

Nakubaliana na wewe kwamba hao ni ma agent wa polisi. Haiingii akilini inakuwaje uhalifu ufanyike hapo just few meters kutoka kito cha polisi?

Tiba
huo ndio ukweli wenyewe my dear! hakuna polisi pale salenda asiyefahamu adha ya wale agents wao, ila wanafanikisha sana kuwapa chochote kitu, hawawezi kuwafukuza pale! yaani ni ujinga usioelezeka kwa mtu yeyote, kuwa kituo kikubwa kama salenda kipo pale, na watu wanalizwa mali zao, tena kudhurika kabisa, without them taking any action! ni aibu mno kwa serikali dhaifu ya ccm!
 
dawa ya vibaka ni kuwa na hii kitu tu. maana ukitegemea polisi wakupe ulinzi umekwisha.


glock17m.JPG
 
Hahahahahaaaa Pole kamanda wetu!!hao ni kitu kimoja na polisi wa hapo!NINA USHAHIDI-rafiki yangu aliwahi kuibiwa simu zake mbili BB moja na tecno moja,alikuwa akifanya kazi fulani nyumbani kwa askari mmoja aliyeitwa muddy(kifupi)aliyekuwa kwenye kituo kilicho hapo jirani,baada ya kuibiwa hakuleta jeuri yoyote kutokana na mazingira na ugeni wake hapo dar,alienda kituoni hapo na hakumkuta mwenyeji wake ila alitoa taarifa pale counter,askari aliyeandika maelezo yake alimkumbuka kwani jana yake walikuwa naye kwenye baa moja jirani na duka la tbc/startimes,yule askari alicheka sana kisha akamtaka rafiki yangu asubiri kidogo mwenyeji wake(muddy)atarejea punde,kweli mudy hakuchelewa sana na yule askari mwingine akamweleza mudy kilichomkuta mgeni wake huyo,mudy akakunja uso kidogo na kumwuliza yule askari mwingine alichukua hatua gani,akamwambia kuwa alikuwa anasubiri yeye(mudy)aje kwanza,basi mudy akampa rafiki yangu hela za kazi na kumwomba aende kazini asubuhi then aende pale kituoni mida ya mchana,kesho yake rafiki yangu alifanya kama alivyoagizwa na mchana alienda pale kituoni ila hakumkuta mudy,baada ya kujieleza askari mwingine(siyo yule wa jana)alimpigia simu mudy kisha akamwita jamaa yangu nyuma ya kaunta na kumwambia aangalie kama ataweza kuikumbuka simu yake,jamaa akamweleza kuwa zilikuwa simu mbili,yule askari akaja juu,"jana ulisema simu moja leo unasema mbili"jamaa akamtaka aangalie tena kitabu cha maelezo,askari akagoma na kumpa ile tecno,akamwambia kama kuna la zaidi amsubiri mudy,jamaa akauliza mudy ni nani kwenye kituo hicho?au anahusikaje na kilichopotea?akajibiwa ovyoovyo na kuamua kumpigia mudy aliyemtaka wakutane baadaye hapo kwenye ile baa,alipofika mudy alimwambia asubiri kidogo,baadaye kijana mmoja aliingia na kuelekea moja kwa moja kwenye meza waliyokaa,na baada ya mazungumzo kidogo kijana yule alimwita mudy pembeni!!mudy aliporudi alimkabidhi jamaa yangu blackberry ile bila maelezo yoyote na kumtaka kuwa makini siku nyingine iwapo atapita maeneo yale ni bora achukue tax au bajaj,siku hiyo jamaa yangu huyo alikuja kisukulu na kunihadithia story nzima,usiku nilimwambia jamaa yangu huyo ajaribu kumpigia huyo mudy simu na amdanganye kuwa ameibiwa tena huku maeneo ya mwenge lakini huyo mudy alimjibu kuwa kama ataibiwa tena maeneo yale ya salender amshtue ila huko mwenge shauri yake!!hapo nikagundua kitu!!
 
Juzi Jumamosi, nimeshuhudia 'live' kibaka akimuibia mama mmoja hapo hapo Selandar Bridge.

Ni hivi, kulikuwa na foleni, na mama wa watu akiwa peke yake kwenye gari alikuwa anaendesha toka mjini kuja upande wa ubalozi wa ufaransa. Alikuwa kwenye lane ya kushoto. Kwenye hako ka-msitu, ukishavuka daraja (toka mjini) kuna kijana anapenda kutembeatembea huku akiwa mchafu utadhani ni kichaa. Ukimuona tia lock milango ya gari maana huyu ndiyo kibaka-kiongozi.

Alichokifanya juzi baada ya kuona magari yanatembea taratibu kwa sababu ya foleni, alianza kusogelea magari na kuchungulia ndani kuna nini. Kwenye gari ya huyo mama aliona mkoba (handbag), ghafla tukaona kafungua mlango wa gari na kuchuku mkoba kisha akatomea kwenye hicho ki-msitu. Nadhani kuna wenzake humo porini. Pilice walikuwepo na watu wengi walijitahidi kumkimbiza lakini kwa bahati mbaya kuna tope na yeye mwenyewe (mwizi) alishafanya 'training' ya kukimbia kwenye tope.

Nadhani kuna haja ya kuongeza doria eneo hilo. Hata ombaomba wa hapo si wa kuamini tena. Ukimuona huyo kibaka hutashtuka hata kidogo maana anaonekana kama kichaa kumbe yuko kikazi zaidi.

Tumefika hapa tulipo kwa sababu tumeruhusu akili ndogo zitawale akili kubwa (Anonymous, 2012)
 
Hii nchi ina matabaka mkuu, miraji kikwete aliwahi kuibiwA simu airport polisi walichachamaa palepale uwanjani mpaka simu ikapatikana.
Naombea mke wa said mwema apate itilafu hapo salenda ili naye aporwe huenda ndio wataona ukubwa wa tatizo.
 
Jamani jamani kweli hii nchi imeoza kila kona sasa pale darajani jamani mbona pako wazi sana tu na hii tabia ya hawa vibaka kutokuogopa wanaipata wapi nani anawapa jeuri hawa washenzi aisee mie kama siku nafanikiwa kupita hapo then kibaka ati anafungua mlango wa gari yangu/ya mtu wa pembeni yangu ni kwamba badala ya kukimbilia huko porini itabidi gari mbli zije yaani moja ya kunichukua mie kwa kuwa nimeshamuuwa kibaka na gari lingine ni Ambulance kuja kuchukua maiti ya kibaka kwani nafahamu kuchukua sheria mkononi si sawa hata kidogo lakini kutokana na hawa mbwa wanavyotanua pale no no no men its to much i cant ole wao bora nikaozee jela lakini nijue nimeuwa kibaka sitajutia.
Kama vipi watu wawe na virungu ndani ya magari yao kama si bastola kama watu tukikomaa na hawa panya wataacha hata kama kuna wengine wenye mpango huo wa kujiunga.
Pole sana Mh Mchungaji Msigwa,Mungu akupe nguvu zaidi na uugue pole
 
Kumbe hata Shimbo amewai kukabwa hapo, híi ni aibu kwa JWT...hana silaha.? Hana mlinzi? Sio komando.?
 
yaani nipo radhi nitembelee rim pale salenda kama gari ikipata pancha, kuliko kukutana na ma-agent wa polisi! haiwezekani washindwe kudhibiti kikundi kidogo cha wezi, sasa hao ni polisi au ni sungu sungu??? pathetic, pole mchungaji! mjini mipango baba!

Umeona eeeeh ipo siku JK atasachiwa hapo ndo labda watawadhibiti hao wezi wenzao
 
yaani nipo radhi nitembelee rim pale salenda kama gari ikipata pancha, kuliko kukutana na ma-agent wa polisi! haiwezekani washindwe kudhibiti kikundi kidogo cha wezi, sasa hao ni polisi au ni sungu sungu??? pathetic, pole mchungaji! mjini mipango baba!

Huo ndo mpango mzima otehrwise unakula hasara mara tatu zaidi,bora ule hasara ya tairi na rim tu. Kuna hapo na eneo lile la darajani baada ya kupita Mtongani hadi uibukie Mission, na eneo la jangwani kutoka fire mpaka magomeni,,ukisimama tu umeliwa
 
Nngu007 na Wana JF,
Kwanza nampa Pole Mchungaji na Mbunge Msigwa,
Kikubwa nilichokielewa kutokana na Habari hii ni kuwa Mchungaji alijisahau na kujiamini.
Alijisahau kuwa alijua na kuambiwa kama sio kuona maeneo hayo ya Salenda wimbi la vibaka limeongezeka, angeweza kutembelea rim mpaka sehemu salama.
Kujiamini, Mpo watu wawili, na wenzako wapo nane, na hakuna msaada wa kupiga makelele ya wezi na kuomba msaada.
Anyway tunajifunza kutokana na Makosa.
Nawakilisha.




JUMATATU, OCTOBA 29, 2012 05:23 NA GABRIEL MUSHI, DAR ES SALAAM

mchungaji-peter-msigwa.jpg


Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa


MBUNGE wa Iringa Mjini, (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa, ameeleza namna alivyovamiwa, kupigwa na kuporwa na vibaka maeneo ya Daraja la Salenda, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akisimulia mkasa huo jana, Mchungaji Msigwa alisema, alikabwa na vibaka juzi, saa moja usiku wakati akitokea katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

“Siku hiyo Kamati yetu ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira, tulikuwa tumekwenda kutembelea Msitu wa Ruvu Kusini na wakati narudi nilipitia ile Barabara ya Ali Hassan Mwinyi.

“Nilipofika maeneo ya Daraja la Salenda Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, ghafla gari yangu ilipata hitilafu katika upande wa tairi, ndipo nikashuka pamoja na dereva wangu ili kukagua.

“Kabla ya kushuka, nilimwambia dereva wangu anayeitwa Baraka, apaki pembeni kidogo ili asisababishe foleni. Tulipolikagua gari, tukakuta kuna kasoro zilizosababisha tairi zisiweze kuzunguka vizuri.

“Dereva wangu alichukua jeki na kuanza kutengeneza gari, wakati huo mimi nikawa nazungumza na mtu kwenye simu yangu, pembeni ya ukuta wa daraja. Ghafla mbele yangu wakatokea vijana kama nane hivi, wakawa wananisogelea, mimi nikaamini wale labda wamekuja kunisaidia kumbe sio.

“Waliponikaribia, nikawauliza wanataka nini, wakaniambia kaa kimya, kwa kuwa mimi ni mbishi, nikaendelea kuzungumza na simu, lakini mmoja wao akaanza kuninyang’anya ile simu nikawa naing’ang’ania, kwa sababu najua ina namba nyingi za watu.

“Nilipozidi kuonyesha ubishi walizidi kunikaba, wakati huo baadhi yao waliendelea kumminya dereva wangu ambaye tayari alikuwa kule chini ya gari akilitengeneza.

“Lakini mimi nikapambana na wawili niliokuwa nao nikawa nakaribia kuwashinda, hata hivyo wakaongezeka tena, ndipo wakafanikiwa kunidhibiti na kuninyang’anya simu yangu na nyingine zilikuwa kwenye gari, wakachukua pia na fedha taslimu Sh 400,000 na baadhi ya vitu vidogo vidogo vilivyokuwa kwenye gari, isipokuwa Ipad hawakufanikiwa kuiona kwa sababu ilikuwa kwenye kioo cha mbele cha gari.

“Kusema kweli walinipiga kisawasawa, wakaniumiza mguu kidogo na jicho, wakaniharibia na meno yangu mawili ya bandia.

“Wakati wananikaba, wengine walimkamata dereva wangu na kumtupa baharini, lakini nashukuru hakudhurika. Baadaye tukapata msaada kwa askari polisi waliofika eneo la tukio, ingawa walichelewa kufika.

“Hata hivyo, sasa hali yangu inaendelea vizuri kwa sababu hapo awali nilikuwa na tatizo la mguu, ambao mwezi uliopita nilikwenda Ujerumani nikaanguka na kufanyiwa uchunguzi, lakini niliporudi nchini Oktoba tisa, nilifanyiwa upasuaji na sasa naendelea vizuri kwa sababu nategemea kutoa hili hogo kesho,” alisema Mchungaji Msigwa.

Akizungumzia eneo hilo jinsi lilivyo, alisema limekuwa na historia ya watu kukabwa na kuibiwa fedha na vitu mbalimbali.

“Kwanza ni aibu sana kwa sababu ni eneo ambalo lipo karibu na Kituo cha Polisi, lakini ukiwauliza askari wanadai eti wakitaka kuwakamata hao vibaka huwa wanakimbilia baharini.

“Wapo pia wabunge mbalimbali nimesikia walishawahi kukabwa hapo na kuibiwa Sh milioni moja, ingawa hawakutaka kusema, mimi ni msema kweli nimesema kwamba walinikaba.

“Vivyo hivyo, nilishawahi kusikia huyu Kigogo wa JWTZ anayeitwa Shimbo, naye alishawahi kukabwa baada ya kufika eneo hilo baada ya kushuka kwenye gari na kuanza kujisadia haja ndogo,” alisema.

Kwa mujibu wa habari iliyochapishwa na gazeti moja linalochapishwa kila siku toleo la jana (siyo MTANZANIA), Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Komba, alisema vibaka wawili wameshakamatwa na leo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani.


 
Kuna kipindi walikuwa wanaweka mawe makubwa usiku ili ajali itokee waibe hali ilipozidi kutisha matukio yakapungua sasa wameanza kuiba mchana kweupe maeneo yenyewe full security hii ni aibu sana tuna wavaa magwanda ya polisi lakini polisi wenyewe hatuna wanakula mshahara na rushwa tu... na kwa hali hii hakuna atakayewajibika
 
tatizo wahehe ni wabishi sana, shauri yako siku nyingine wangeku barlow, muwe wapole mkikutana na vibaka
 
Hii nayo ni aibu. A lieutenant general is a high ranking official in the army halafu anaporwa na vibaka kizembe ambao wana visu tu.Kama ni kweli kwanini Shimbo hakurudi na vijana wake pale kutoa angalao discipline
 
MSigwa naye asiwe kama haijui Tanzania, anapambanaje na vibaka salenda??? wangemuua tungesema ni siasa pia???

wale vijana wakija ni kuwapa wanachotaka au kunegotiate wakuachie japo buku ya chai, wanakuelewa kabisa

hiyo ya kujitutumia na watu wana viwembe, bis-bis na visu ni kutafutia watu lawama tu

she should think of his life first!!!
 
jeshi la polisi ni kichaka cha uharifu huwa siwaamni hata siku moja maana wanajifanya wanafanya kazi kumbe uhuni mtupu na ndio wanashirikiana na wezi
 
Back
Top Bottom