Mbunge Salim Alaudin: Kuna Haja ya Kuharakisha Mchakato wa Mikopo ya 10%

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MBUNGE ULANGA (SALIM ALAUDIN): KUNA HAJA YA KUHARAKISHA MCHAKATO WA MIKOPO YA 10%

Wananchi wa Kijiji cha Minepa Wilaya ya Ulanga mkoani wa Morogoro wamesema uwepo wa baadhi ya vifungu vya fedha kumekwamisha kupata mikopo inayotolewa na serikali kwa lengo la kuwainua kiuchumi.

Wakizungumza mbele ya Mbunge wa Jimbo la Ulanga Salim Alaudin Hasham katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Minepa wilayani humo wamesema kuwa kukosekana kwa fedha za mikopo kumekuwa kukiwakosesha mitaji ili kuweza kujiari na kuacha kuwa tegemezi katika familia

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ulanga Salim Alaudin Hasham amesema kuna haja ya Serikali kupitia mamlaka zinazohusika na utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa vijana wanawake na wenye ulemavu kuharakisha mchakato ili kuweza kuwasaidia wananchi kujikwamua kiuchumi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga Saida Mahugu amesema, kutokana na vikundi vingi kushindwa kurejesha mikopo kwa wakati serikali ilisitisha zoezi la utoaji wa mikopo
 

Attachments

  • F93xbeRXAAAk04V.jpg
    F93xbeRXAAAk04V.jpg
    101.2 KB · Views: 7
  • F93xcMfWIAA0Qlq.jpg
    F93xcMfWIAA0Qlq.jpg
    101.4 KB · Views: 7
  • F93xconXUAA_Ac6.jpg
    F93xconXUAA_Ac6.jpg
    135.6 KB · Views: 5
Back
Top Bottom