Mbunge Ntate Katika Mapokezi ya Katibu Mkuu UWT Taifa, Jokate Mwegelo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,899
944
Mbunge wa Viti Maalum (Anayewakilisha Wafanyakazi Nchini) kutoka Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Janejelly James Ntate leo tarehe 04 Oktoba, 2023 ameshiriki katika Mapokezi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa Ndugu Jokate Mwegelo yaliyofanyika katika Ofisi za CCM Mkoa wa Dar es Salaam

Katika mapokezi ya kumkaribisha Katibu Mkuu UWT Taifa, Mhe. Janejelly James Ntate kwa niaba ya Wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam alipata nafasi ya kutoa neno la shukurani na kumpongeza Ndugu Jokate Mwegelo kwa imani aliyopewa na Chama Cha Mapinduzi kuwa Katibu Mkuu UWT Taifa.

Mhe. Janejelly James Ntate akizungumza katika mapokezi ya Katibu Mkuu UWT Taifa, amesema kuwa UWT imepata mtu makini katika utendaji kazi na pia amesisitiza wana UWT wote kumpa ushirikiano ili kazi ifanyike kwa ufasaha.

Mapokezi ya Katibu Mkuu UWT Taifa, Ndugu Jokate Mwegelo yameambatana na Katibu Mkuu UWT Taifa kwenda kuchukua fomu ya Uteuzi alioaminiwa na Chama Cha Mapinduzi kuwa kama Mtendaji Mkuu wa UWT Taifa

#UWT IMARA JESHI LA MAMA
#KAZI IENDELEE


WhatsApp Image 2023-10-04 at 18.15.10.jpeg
WhatsApp Image 2023-10-04 at 18.50.25.jpeg
WhatsApp Image 2023-10-04 at 18.50.25(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-10-04 at 18.50.25(2).jpeg
 
Back
Top Bottom