Mbunge Mhandisi Mwanaisha Ng'anzi Ulenge Akichangia Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi Katika Mwaka Mpya wa Fedha 2024-2025

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,994
961

MBUNGE MHANDISI MWANAISHA NG'ANZI ULENGE Akichangia Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi Katika Mwaka Mpya wa Fedha 2024-2025

"Serikali ya Tanzania imepanga Sekta ya Bandari ichangie kwenye pato la Taifa kwa kiwango cha Asilimia Saba ifikapo mwaka 2025-2026. Mamlaka ya Bandari (TPA) Inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa kuzingatia mpango kabambe wa Mamlaka wa mwaka 2020-2045" - Mhe. Mhandisi Mwanaisha Ng'anzi Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga

"Mpango wa Mamlaka ya Bandari wa mwaka 2020-2045 ni Upanuzi wa Gati Namba 8-11, Ujenzi wa Matenki ya kupokea na kuhifadhi Mafuta na Ujenzi wa Gati Namba 3 kuhudumia Bandari ya Tanga. Utekelezaji wa miradi yote inahitaji fedha za kutosha kwani washindani wetu miundombinu (Gati) waliyokuwanayo ni mara mbili ya Gati za Bandari ya Dar es Salaam" - Mhe. Mhandisi Mwanaisha Ng'anzi Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga

"Mamlaka ya Bandari bila kuwa na vyanzo vya kutosha vya mapato kwaajili ya utekelezaji wa miradi hii, malengo tuliyojipangia kuchangia Asilimia Saba ya Pato la Taifa haiwezi kutokea. Duniani kote, mapato yatokanayo na mtumiaji wa Meli fedha huwa zinatengwa kwaajili ya kujenga na kuboresha miundombinu ya Bandari" - Mhe. Mhandisi Mwanaisha Ng'anzi Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga

"Tamko lililotolewa Agosti 2017, Bandari ilisitisha kukusanya mapato kutoka kwa Mtumiaji wa Meli (Kama chanzo cha mapato ya Mamlaka ya Bandari). Sheria iliyoundwa mwaka 2019 Na.7 ilimpa Mamlaka ya Mapato (TRA) kukusanya fedha zinazotokana na Wafeji na kuziweka katika Akaunti Maalum iliyopo Benki Kuu ya Tanzania (BoT)" - Mhe. Mhandisi Mwanaisha Ng'anzi Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga

"Fedha za Wafeji zilizopo BoT kwa mujibu wa taarifa ni kwamba hazitumiki ipasavyo. Gati zilikamilika sasa hivi zinatumika na Kampuni ya DP World, ina maana Mamlaka ya Bandari inahitaji kuongeza Gati nyingi zaidi kwa ufanisi na kuongeza Shehena. Fedha za wafeji ni asilimia 50 ya Mapato ya Bandari. Bandari inatumia asilimia 50 ya Mapato mengine yatokanayo na Bandari kuendeleza miundombinu mbalimbali" - Mhe. Mhandisi Mwanaisha Ng'anzi Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga

"Fedha za Wafeji zimewekwa kwa mujibu wa sheria kuwa mapato ya Bandari ili kuendeleza miundombinu ya Bandari ili Meli kubwa ziweze kushusha mizigo. Suala la kuboresha miundombinu ya Bandari haliepukiki. Naungana na Maoni ya Kamati ya Miundombinu kubadilishwa kwa sheria ya Mamlaka ya Bandari ili kuiwezesha Mamlaka ya Bandari kuweza kukusanya mapato yatokanayo na Wafeji" - Mhe. Mhandisi Mwanaisha Ng'anzi Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga

"Mapato yatokanayo na Wafeji kabla ya kupelekwa BoT huwa yanaingia Akaunti fulani ya biashara baadaye ndiyo hupelekwa BoT. Zinaanza kutumiwa na TRA ambapo ni kinyume na Sheria, pia huwa zinanguzwa na kupelekwa kiasi kisicho halisi katika makusanyo yake. Nashauri Serikali, Sheria hii ibadirishwe ili Mamlaka ya Bandari ikusanye fedha ili kuboresha miundombinu ya Bandari nchini" - Mhe. Mhandisi Mwanaisha Ng'anzi Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga

"Nawiwa kuishauri Serikali, kuhakikisha sheria zinabadilishwa. Passengers Service Charges irudishwe na ikusanywe na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania na Wafeji iweze kukusanywa na Mamlaka ya Bandari ili kufikia azma ya Serikali ya kuchangia kwenye pato la Taifa asilimia Saba" - Mhe. Mhandisi Mwanaisha Ng'anzi Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga


 
Mkuu unauhakika huyu Ni mhandisi aliyesomea uhandisi au Ni vyeo vya kujitangazia Kama walivyo ma dakta tulio nao wengi.
 
Uchaguzi umekaribia, wameanza kuchangia hoja, mimi nilijua ni mbunge wa zimbabwe, sijawahi kumfahamu
 
Back
Top Bottom