Mbunge Lusinde atangazwe shujaa Afrika kama kijana mtaka mabadiliko

Shotocan

JF-Expert Member
Nov 21, 2023
2,231
4,650
Mbunge Lusinde atangazwe shujaa Afrika kama kijana mtaka mabadiliko ya wabunge kumpiga chini Waziri Mkuu Malecela mwenye Cv kibao na Pesa Malecela

Livingstone Lusinde darasa la saba alimbwaga aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania mwenye wasifu mkubwa na madigrii kibao

Vijana wakiamua wanaweza

Record ya vijana Afrika ya Lusinde imevunjwa na Rais wa Senegal ndugu Faye kutoa Serikali ya vikongwe

Vijana 2025 msiogope yeyote bila kujali CV yake vyama vyote iwe CCM au

Livingstone Lusinde awe role model wenu msiogope kabisa hao wakongwe majimboni
 
Neno shujaa wa afrika haliko reserved kwa vibwengo, hiyo title iko reserved kwa exceptional individuals waliofanyia afrika makubwa. punguza sifa kwa watu wa kawaida
 
Alitolewa Tarime alikokuwa anahudumu kwenye chama akapewa pesa na kundi fulani ili akamtoe mzee Malecela, Hii ilikiwa maandalizi ya 2015.

UKipenda mtangaze tu shujaa wa familia yako, inaonekana kwenu neno shujaa halina maana kabisa
 
Wakati mwingine wananchi wanakosa "wide choice" kutokana na aina ya watu wanaojitokeza kugombea na hivyo kuchagua tu bora liende. Utakuta mbunge aliyepo madarakani wamekwishamchoka, kwa hiyo basi yule ambaye anajitokeza kushindana naye hata kama hana sifa nzuri wala hawamwelewi vizuri inabidi wamuunge tu mkono ili tu kumkomoa yule waliyemchoka.

Ukitaka kutambua ukweli huu basi liangalie kwa jicho la kidadisi jimbo la uchaguzi Mtera. Angalia uwezo binafsi wa mbunge katika kuwaunganisha watu katika kuchochea na kuchangia maendeleo ya jimbo.
Licha ya fedha kiduchu zinazotengwa na serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya eneo husika, lakini bado ni jukumu la mbunge na viongozi wengine kuwachochea wadau hasa waliopo sekta binafsi katika kufanya mageuzi.

Sifa za mtu kum "replace" mwingine katika nafasi fulani ya uongozi eti tu kwa kigezo cha umri wala haina mashiko ya kumtambuñisha kama shujaa wa Afrika. Bali nini ambacho anakifanya ili kuchochea na kuleta maendeleo chanya katika jimbo lake ndiyo suala linalopaswa kufanyiwa mjadala.
 
Alitolewa Tarime alikokuwa anahudumu kwenye chama akapewa pesa na kundi fulani ili akamtoe mzee Malecela, Hii ilikiwa maandalizi ya 2015.
UKipenda mtangaze tu shujaa wa familia yako, inaonekana kwenu neno shujaa halina maana kabisa
Umemaliza yote kiongozi..ni kama uone KOBE mtini
 
Kushinda uchaguzi ni majibu ya kero za maendeleo?
Tuwekee merits zake hapa kama kijana mpenda mabadiliko ameleta mabadiliko gani kisekta, kielimu, na utawala bora?
 
Mbunge Lusinde atangazwe shujaa Africa kama kijana mtaka mabadiliko ya wabunge kumpiga chini waziri mkuu kikongwe Malechela mwenye Cv kibao na Pesa Malecela
Ungekaa kimya ingekusaidia kuficha upumbavu wako!
Hivi huoni aibu kutaka mtu wa elimu ya ngumbaro eti awe shujaa?
Ni kama vile wewe ni 'mteja' hapo mirembe Hosp! meza dawa!
 
Back
Top Bottom