Mbunge kuwasilisha hoja kuzuia waziri mkuu kuhojiwa

MAGAMBA MATATU

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
646
1,174
Habel Chidawali,Dodoma
MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia tiketi ya CCM, Ritta Kabati,anatarajia kuwasilisha bungeni, hoja binafsi ya kutaka kuondolewa kwa utaratibu wa sasa wa maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.Mbunge huyo alitoa kauli hiyo juzi, alipokuwa akichangia hotuba kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu, katika mwaka wa fedha wa 2011/12.

Kabati alisema haoni mantiki ya kuwapo kwa kipindi hicho ambacho alisema kimekuwa kikitumiwa vibaya na kumdhalilisha Waziri Mkuu.Maswali ya papo kwa hapo bungeni yanaulizwa mara baada ya kuanza kwa shughuli za Bunge, kila siku ya Alhamisi.

Katika mchango wake, mbunge huyo alisema kipindi hicho kinapaswa kiondolewe mara moja na kwamba kaama hakitaondolewa, vizuri kwa Spika au mtu yeyote anayeongoza kiti cha uspika kuundiwa utaratibu maalumu wa kuzuia baadhi ya maswali kwa Waziri Mkuu.

"Nitaleta hoja binafsi hapa bungeni ili kipindi hiki kiondolewe maana kina mdhalilisha Waziri Mkuu, ikimbukwe kuwa katika mkutano wa tatu Mbunge wa Arusha Godbless Lema, alisema Waziri Mkuu amesema uwongo je huo si udhalilishaji kwa Waziri Mkuu," alihoji Kabati.

Mbunge huyo alilenga moja kwa moja katika hoja ya Lema ambaye wakati huo aliomba mwongozo wa spika na aliposimama alieleza kuwa Waziri Mkuu alikuwa amelidanganya Bunge kuhusu chanzo cha mauaji ya watu watatu katika maandamano ya Arusha.Alisema kutokana na spika kutoshindwa kumchukulia hatua za kinidhamu mbunge huyo, kuna uwezekano wa wabunge wengi kutumia njia hiyo kumdhalilisha kiongozi huyo na serikali kwa jumla.

Alisema utaratibu huo ulinukuliwa kutoka Bunge la Uingereza ambako hata hivyo, wabunge wanamuuliza Waziri
Mkuu maswali yanayomlenga.

"Mheshimiwa mwenyekiti, kule Uingereza wenzetu wanauliza maswali hayo kwa kuwa Waziri Mkuu wao ni kiongozi mkubwa tofauti na sisi ambapo huyu wa kwetu yuko chini ya rais, sasa mizigo mingine tunayomtwisha ni mikubwa kuliko uwezo wake," alisema.

Hata hivyo wakati Kabati akihoji juu ya kauli ya Lema, mbunge huyo jana alinukuliwa na vyombo vya habari kuwa spika Makinda hamtei haki."Kitendo cha Spika kutoruhusu niwasilishe ushahidi wangu kuhusu uongo wa Waziri Mkuu kimeniweka katika wakati mgumu sana kwani ninaonekana kuwa mimi ndiyo mwongo,"alisema Lema.

Mbunge huyo alisema kuwa kitendo cha Makinda cha kumtaka Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe awasilishe ushahidi wake baada ya kulituhumu Baraza la mawaziri kabla yake ni upendeleo wa wazi,

MASWALI NI MENGI SANA KWA WATANZANIA KWANINI AAMUE KUZUIA WAZIRI MKUU KUHOJIWA???
 
Inawezekana maswali ya wapinzani ni magumu sana au huyu mbunge kaona siku 1 nae atakuwa waziri mkuu alafu ashindwe kujibu maswali,
 
Namsikitikia sana huyu Kabati kwa sababu hajajipa kazi ya kujifunza kwa nini mfumo huu ulianzishwa
 
Back
Top Bottom