Mbunge Kuchauka: Waziri akichaguliwa leo anakuta wizarani kuna watu ni 'mama wa wizara', ili aweze kudumu kwenye wizara anaungana nao!

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Mbunge Kachauka anasema anaona Wakurugenzi wanatumbukizwa kwenye bwawa lenye mamba kwasababu kuna mhasibu, mkaguzi wa ndani, afisa masuuli kwenye halmashauri ambao wana uzoefu mkubwa kuliko yeye.

Kumpeleka mtu aliyekuwa mwalimu akagombea ubunge na kupelekwa pale kama Mkurugenzi je salama yake kwenye mamba hao ni nini? Ni kuungana nao!

Akiendelea kusema je Mkurugenzi huyo anayewekwa hapo na utaalamu wowote wa uhasibu, anajua mambo ya mipango, ununuzi na ukaguzi? Kama hajui na hao ndio wakongwe - akodokeza na hilo kufanyika hadi upande wa Wizara akisema,

Wewe Waziri unachaguliwa leo, unaingia kwenye wizara unakuta watu kwenye wizara ile ndio mama wa wizara, 'mwenzake na yeye' ili aweze kudumu kwenye wizara ile atafanyaje? Ataungana nao!

 
Back
Top Bottom