Mbunge Kainja aendelea Kugusa na kuwainua kiuchumi Wanawake wa UWT Kata 46 za Wilaya ya Nzega

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora, Mhe. Jacqueline Kainja Andrew ameendelea na ziara yake katika Wilaya ya Nzega ambapo ameendelea kutoa fedha za miradi mbalimbali yenye thamani ya Shilingi Milioni 81,000,000 katika Kata zote za Mkoa wa Tabora ili kuwawezesha wanawake kiuchumi.

Vilevile, Mhe. Jacqueline Kainja katika Ziara yake Wilayani Nzega ameongozana na Mhe. Rose Busiga ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Geita ambaye amechangia Shilingi 500,000 kwa ajili ya Ujenzi wa Nyumba ya Katibu wa UWT Wilaya ya Nzega.

Mhe. Kainja amesema baada ya kukabidhi fedha za miradi kwa Wajumbe wote wa UWT katika Kata 46 za Wilaya ya Nzega kuwa Miradi ni tofauti na haifanani kutokana na uhitaji wa Kata husika kwani ilichaguliwa na wajumbe wenyewe.

Aidha, Mhe. Kainja ametoa msaada wa Godoro, Vitenge, Khanga, Mashuka, Sukari na Sabuni kwa Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kata ya Igusule Wilaya ya Nzega Ndugu Elizabeth Patric baada ya kuunguliwa na nyumba.

Mwisho, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora, Mhe. Jacqueline Kainja Andrew amewashukuru sana viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kata ya Igusule Wilaya ya Nzega na Wajumbe wote wa UWT.

WhatsApp Image 2023-07-10 at 20.50.24.jpeg
WhatsApp Image 2023-07-10 at 20.50.24(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-10 at 20.50.24(3).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-10 at 20.50.24.jpeg
WhatsApp Image 2023-07-10 at 20.50.24(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-10 at 20.50.24(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-10 at 20.50.24(3).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-10 at 20.50.24(4).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-10 at 20.50.24(5).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-10 at 20.50.24(6).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-10 at 20.50.24(7).jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom