Mbunge Fakharia Shomari: Serikali Iliangalie Suala la Usafirishaji Haramu wa Binadamu Tanzania

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945

Mbunge Fakharia Shomari: Serikali Iliangalie Suala la Usafirishaji Haramu wa Binadamu Tanzania

Mbunge Faharia Shomari akichangia hoja ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama amesema hivi sasa nchini lipo jambo la kutisha la usafirishaji haramu wa binadamu ambapo Wanawake na Watoto wa Kitanzania wanasafirishwa kwenda Ughaibuni.

Ameongeza kuwa wapo mawakala wa Tanzania wanaosimamia na kufanikisha masuala hayo kutendeka, na kwamba ana wasiwasi na Askari wa uhamiaji kwa kuwa Wananchi hao wanaposafirishwa kwenda ughaibuni wanapata vielelezo vyote kuwawezesha kusafiri.

Amedai Wananchi hao wanarubuniwa kwa kuahidiwa kazi kwamba kuna kazi nje ya nchi japokuwa wakifika huko hufanyishwa kazi tofauti na waliyoahidiwa na pale wanapokataa kufanya kazi hizo hupitia mateso na kunyang’anywa hati zao za kusafiria na kukataliwa kurejeshwa nchini pale wanapoomba kurejeshwa.
 

Attachments

  • Untitledqwased.jpg
    Untitledqwased.jpg
    8.3 KB · Views: 1
Back
Top Bottom