Mbunge Eng. Aisha Ulenge ashauri uanzishwaji wa Programu kuhamasisha Wanafunzi kutumia Maktaba

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

Mbunge Eng. Aisha Ulenge Ashauri Uanzishwaji wa Programu Kuhamasisha Wanafunzi Kutumia Maktaba

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga Mhandisi Mwanaisha Ulenge amefanya ziara ya kutembelea Maktaba ya Mkoa wa Tanga na kushauri kuanzishwa program ya kuhamasisha Wanafunzi na jamii kuitumia Maktaba hiyo.

Akizungumza na Mkutubi wa Maktaba hiyo pamoja na wanafunzi waliokuwa wanajisomea, Novemba 20, 2023 amesema amesikitishwa na hali ya uchakavu wa maktaba hiyo hivyo kuahidi kutoa ushirikiano katika kusukuma suala ya kuboresha Maktaba.

Aidha, Mhandisi Ulenge amemtaka mkutubi kuanzisha program ya kuhamasisha wanafunzi na wanajamii kuitumia Maktaba hiyo.

"Mkutubi nikuahidi ushirikiano katika kuboresha Maktaba yetu, lakini pia kuhamasisha wananchi kutembelea na kujisomea katika maktaba hii" - Mhandisi Ulenge.

Pia, amewatia moyo wanafunzi aliowakuta wakijisomea ndani ya maktaba na kuwataka kusoma kwa bidii kwa manufaa ya maisha yao ya kesho.

Aidha, Mhe. Mhandisi Mwanaisha Ng'anzi Ulenge amegawa Kompyuta kwa wanafunzi ili kumuenzi Chifu Erasto Mang'enya huku akiwasisitiza wanafunzi hao kusoma kwa malengo na kuwa na ndoto kubwa. Pia, amewasihi wanafunzi Wasichana kusoma Masomo ya Sayansi.

WhatsApp Image 2023-11-27 at 12.29.21.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-27 at 12.29.22.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-27 at 12.29.22(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-27 at 12.29.22(2).jpeg
 
Maktaba inabidi ziwepo kila shule kama ambavyo vyoo ni takwa la lazima kwa kila shule kuwepo.

Na sio maktaba jengo pekee bali na vitabu vilivyo jaa vya kila maarifa muhimu.
 
Maktaba ni very old fashioned.
Kuna World Wide Web(w.w.w.)ina material isiyokwisha kwa information hapa duniani.
 
Back
Top Bottom