Mbunge Cherehani Akabidhi Kadi 400 za UWT Ulowa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

MBUNGE CHEREHANI AKABIDHI KADI 400 ZA UWT ULOWA

Mbunge wa jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Cherehani amekabidhi kadi 400 za Umoja wa Wanawake Tanzania katika Jukwaa la Wanawake Kata ya Ulowa ili Wajiunge na Umoja huo wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga.

Akizungumza wakati wa kukabidhi kadi hizo Cherehani amesema ametoa kadi hizo ili kuwarahisishia wanawake kujiunga na jumuiya hiyo ambapo amemuomba mwenyekiti UWT Wilaya ya Kahama Theresphora Saria kuweka utaratibu wa kuwatembelea wanawake hao mara kwa mara na kuwapa elimu mbalimbali kwa maendeleo yao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa hilo ambaye pia ni mwenyekiti wa UWT wa kata ya Ulowa Constantina Kazwika amemshukuru Mbunge kwa kutoa Kadi hizo ambapo amesema, kupitia mchango huo wataendelea kuhamasisha wanawake kujiunga na UWT hata wale ambao sio wanajukwaa
 
Attachments

  • WhatsApp Image 2024-02-25 at 00.31.09.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-25 at 00.31.09.jpeg
    45.9 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-02-25 at 00.31.09(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-25 at 00.31.09(1).jpeg
    61.4 KB · Views: 1

MBUNGE CHEREHANI AKABIDHI KADI 400 ZA UWT ULOWA

Mbunge wa jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Cherehani amekabidhi kadi 400 za Umoja wa Wanawake Tanzania katika Jukwaa la Wanawake Kata ya Ulowa ili Wajiunge na Umoja huo wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga.

Akizungumza wakati wa kukabidhi kadi hizo Cherehani amesema ametoa kadi hizo ili kuwarahisishia wanawake kujiunga na jumuiya hiyo ambapo amemuomba mwenyekiti UWT Wilaya ya Kahama Theresphora Saria kuweka utaratibu wa kuwatembelea wanawake hao mara kwa mara na kuwapa elimu mbalimbali kwa maendeleo yao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa hilo ambaye pia ni mwenyekiti wa UWT wa kata ya Ulowa Constantina Kazwika amemshukuru Mbunge kwa kutoa Kadi hizo ambapo amesema, kupitia mchango huo wataendelea kuhamasisha wanawake kujiunga na UWT hata wale ambao sio wanajukwaa
Huko ushetu kuna Umasikini wa kutisha, na huo ndio mtaji mkuu wa CCM,
 
Back
Top Bottom