Mbu wa Malaria kutoka Asia ahamia Afrika

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Sep 16, 2009
15,203
16,327
20221102_192339.jpg

Wanasayansi wanasema kwamba aina vamizi ya mbu anayeeneza malaria kutoka Asia imeenea hadi Afrika, ambako ni tishio hasa kwa wakazi wa mijini.

Barani Afrika, ambapo vifo vingi vya Malaria duniani hutokea, ugonjwa huu huenezwa zaidi na mbu maalumu kwa maeneo ya vijijini.

Lakini aina ya mbu wa Anopheles stephensi, ambaye ndiye anayehusika na visa vingi vinavyoonekana katika miji ya India na Iran, huzaliana katika vyanzo vya maji mijini - na ni sugu kwa dawa nyingi za wadudu zinazotumika kawaida.

Mbu huyo tayari amesababisha visa vya ugonjwa huo kuongezeka nchini Djibouti na Ethiopia, na hivyo kutatiza juhudi za kutokomeza ugonjwa huo.

Watafiti wanasema iwapo atasambaa kwa wingi barani Afrika anaweza kuwaweka karibu watu milioni 130 hatarini.

BBC
 
View attachment 2405249

Vimelea alivyo vibeba ni vipi??mana mbu ni vector tu anayebeba wadudu wa malaria.

Vimelea vipi hivyo ambavyo ni sugu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kaja na mabegi yake? ifike mahali wazungu wajue mfumo wao wa kuchuma kupitia maradhi tengenezi umepitwa na wakati toka mwendazake alipowakazia kwenye.covinda
 
Back
Top Bottom