Mshume Kiyate
JF-Expert Member
- Feb 27, 2011
- 6,766
- 894
Hivi karibuni Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kilifanya maandamano katika mikoa ya kanda ya Ziwa yaliyohudhuriwa na watu wengi.
Hata hivyo maandamano yalipokelewa kwa hisia tofauti na serikali ambayo iliyatafsiri kuwa ni hatua ya Chadema kutaka kuleta vurugu nchini. Rais Kikwete alionyesha kukerwa na maandamo hayo akisema Chadema kinawajengea hofu wananchi. Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe amesikitishwa na kauli za viongozi wa serikali kuwa Chadema wanataka kuiondoa serikali madarakani, wapi sisi Chadema tuliwataka wananchi waing'oe serikali? lengo letu ni kuiwajibisha serikali siku tisa walizotoa Chadema kutekeleza maazimio yao ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa hali ya ugumu wa maisha inaondoka. baada ya siku tisa kupita Rais Kikwete ameanza kutekeleza hoja zao. "Ndani ya siku tisa, Rais Kikwete aliagiza bei ya sukari ishuke kutoka sh 2000 hadi sh 1700 hakuishia hapo, aliagiza pia bei hiyo ishuke kutoka sh 1700 hadi sh 1500. " Rais ameanzisha ziara kwenye wizara, akaagiza pia gharama za kuunganisha umeme zipunguzwe hayo yote ni kutekeleza hoja za maandamano yetu.
Source: Mwananchi Machi 30, 2011