Mbowe: Lissu amefanyiwa upasuaji mara 14

the deadline

Member
Sep 26, 2013
62
106
Babati. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amefanywa upasuaji mara 14 na ataendelea kufanyiwa upasuaji mwingine ndani ya wiki mbili zijazo.

Mbowe amesema hayo jana kwenye mazishi ya marehemu Philip Gekul, baba mzazi wa Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul yaliyofanyika kata ya Dareda.

Alisema hali ya Lissu inaendelea kuimarika lakini aliumizwa sana kama walivyokuwa wanaeleza mara zote lakini na jambo la kumshukuru Mungu kwamba ameendelea kuimarika.

"Ameendelea kupata afya, akili zake ni timamu, madaktari kule wanafanya kazi kubwa kwelikweli kuendelea kumuudumia na ni matumaini yetu kuwa baada ya muda Mungu atamrejesha katika wajibu wake wa kulitumikia Taifa,"

Mbowe alizungumza hayo baada ya kueleza kuwa alitokea Nairobi kuangalia afya ya mbunge huyo ambaye alipigwa risasi Septemba 7 mwaka huu akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma.
 
May he get well soo and come back

Ni matumaini yangu waliotaka kumuuwa, watajutia kumkosakosa uhai wake mara atakaporudi ulingoni...
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Babati. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amefanywa upasuaji mara 14 na ataendelea kufanyiwa upasuaji mwingine ndani ya wiki mbili zijazo.

Mbowe amesema hayo jana kwenye mazishi ya marehemu Philip Gekul, baba mzazi wa Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul yaliyofanyika kata ya Dareda.

Alisema hali ya Lissu inaendelea kuimarika lakini aliumizwa sana kama walivyokuwa wanaeleza mara zote lakini na jambo la kumshukuru Mungu kwamba ameendelea kuimarika.

"Ameendelea kupata afya, akili zake ni timamu, madaktari kule wanafanya kazi kubwa kwelikweli kuendelea kumuudumia na ni matumaini yetu kuwa baada ya muda Mungu atamrejesha katika wajibu wake wa kulitumikia Taifa,"

Mbowe alizungumza hayo baada ya kueleza kuwa alitokea Nairobi kuangalia afya ya mbunge huyo ambaye alipigwa risasi Septemba 7 mwaka huu akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma.
Mungu Azidi Kushusha Nguvu za Uponyaji juu ya kamanda Tundu Lissu! Tuna kila sababu za kumshukuru Mungu kwa hilo!
 
Haki yamungu tutangaze madhara makubwa iwapo lissu atatishiwa tena ama kuona gari litakalo mfuatilia tena !!
hatuwezi kubali tumpoteze tena hatuwezi mpata tena !!!
 
Babati. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amefanywa upasuaji mara 14 na ataendelea kufanyiwa upasuaji mwingine ndani ya wiki mbili zijazo.

Mbowe amesema hayo jana kwenye mazishi ya marehemu Philip Gekul, baba mzazi wa Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul yaliyofanyika kata ya Dareda.

Alisema hali ya Lissu inaendelea kuimarika lakini aliumizwa sana kama walivyokuwa wanaeleza mara zote lakini na jambo la kumshukuru Mungu kwamba ameendelea kuimarika.

"Ameendelea kupata afya, akili zake ni timamu, madaktari kule wanafanya kazi kubwa kwelikweli kuendelea kumuudumia na ni matumaini yetu kuwa baada ya muda Mungu atamrejesha katika wajibu wake wa kulitumikia Taifa,"

Mbowe alizungumza hayo baada ya kueleza kuwa alitokea Nairobi kuangalia afya ya mbunge huyo ambaye alipigwa risasi Septemba 7 mwaka huu akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma.
Tundulissu na Marehemu Mzee Gekul wapi na wapi? Mbunge Gekul alikuwa na majonzi ya kufiwa na baba yake, lakini badala ya kumfariji anatumbukiza mambo yasiyohusika. Inasemekana marehemu alimuwa ni Mwana CCM enzi za Edward Sokoine lakini kwa ubinafsi wso kikanda, Sokoine na watu kama Gekul walitupwa.
 
Wana mtesa bure lisu wetu.kulikuwa na umuhimu wowote Wa kumpiga risasi.?kwa nini lakini?
 
Haki yamungu tutangaze madhara makubwa iwapo lissu atatishiwa tena ama kuona gari litakalo mfuatilia tena !!
hatuwezi kubali tumpoteze tena hatuwezi mpata tena !!!
Pambana na hali yako kwanza.
 
Mbowe asione sifa kutamka idadi ya operation. Wingi wa operation unaonesha inefficiency ya hiyo hospitali. Tena wanamchosha kwa dawa za usingizi. Ingekuwa hospitali nzuri nina uhakika operation zisingefikia hayo makumi. Mbowe anatakiwa atujibu sababu zilizomfanya amzuie Nyalandu kumpeleka Tundu marekani.
 
Haki yamungu tutangaze madhara makubwa iwapo lissu atatishiwa tena ama kuona gari litakalo mfuatilia tena !!
hatuwezi kubali tumpoteze tena hatuwezi mpata tena !!!
Ungewapenda wazazi wako kiasi hiki.....peponi ungekaa na Yesu kristo!
 
Back
Top Bottom