Mbowe in informal meeting with JK

yote heri lakini terms za makubaliano zizingatie kile kilichoipa CDM na kupunguzia CCM kura,otherwise hapatakalika.
 
Mkuu watu wanaweza wakakubeza kwa hilo kwa sababu eti tu ni hisia zako na wakifanya hivyo nao watakuwa wamekubeza kwa mujibu wa hisia zao! mimi naona JK na Mbowe watakuwa walikuwa wanajadiliana kuhusu watu watakaokuwemo kwenye tume ya kukusanya maoni ya kuandika katiba mpya.
 
Katiba inasema waziri awe mbunge, haisemi lazima atoke chama cha rais, hivyo katiba tuliyonayo inaruhusu mseto. Ila tu Waziri Mkuu ndio lazima atoke chama chenye wabunge wengi
 
Sasa hivi utasikia wazee wa "copy and paste" CUF nao wanataka kiongozi wao naye aitwe na JK waongee ingawa hawajui nini kilichoongelewa kati ya Mbowe na JK. Subirini muone...
 
CCM bingwa wa siasa, tatizo lenu mnawaamini sana wanasiasa badala ya kujengea wananchi uwezo wa kuhoji wanasiasa..
 
JK na Mbowe ni marafiki wa siku nyingi na ninadhani JK hawai kurudisha kadi ya CDM aliyoichukuwa 1995 na kuilipia hadi 2005! Hata hivyo hao wote wawili ni Watanzania huru wenye haki yao kikatiba kukutana na hata kunywa kahawa pamoja, jambo lolote linaloongelewa kati ya wawili hawa bila kutumwa na vikao vya vyama vyao ni mambo yao binafsi hata kama yanahusu vyama vyao.

Kama hawataki kutwambia ni sawa kabisa, lakini nasisitiza kuwa kama tunataka maendeleo ya kweli lazima tusiwe mashabiki wa watu, hasa wanasiasa bila kuweka vigezo na vipimo vya nani tunataka atutawale na kwa staili gani na mwendo kasi upi.

Ni kweli Jakaya alichukuaga kadi ya Chadema kwa lengo la kuomba uteuzi ....Kama asingechaguliwa kugombea urais ........ukweli ni kuwa Jakaya Ana dhati ya kweli ya kuwatetea watanzania lakini .....watu waliomsaidia kuingia alipo walimgeuza naye anaanza Kupenda pesa na Mali.......mitizamo ya Jakaya wa kale na ya Chadema ilikuwa inaendana.....

Urafiki wa Jakaya nje ya siasa ni wa siku nyingi hata kabla Jakaya hajawa maarufu .....inafahamika kuwa mbowe ni Kati ya watoto wa mjini wa mwanzo.....ukizingatia utajiri wa baba Yake .....na kumiiliki biashara katika umri mdogo....wameshirikiana na Jakaya mambo mengi ya vijana Kama vijana wa zamani...yote!

Ila ni wazi mitizamo Yao kisiasa kwa sasa ni tofauti.....na ieleweke wazi katika anayewezA kudanganyika kwa pesa kubadili mtazamo mbowe si mmoja wao....
 
CHADEMA haihitaji serikali ya mseto, inataka kuchukua dora ili ionyeshe mfano mzuri wa kuongoza nchi na kuleta maisha bora kwa watanzania. kama ingetaka mseto wangekubali kule Arusha ambako magamba walisha warubuni madiwani wenye harufu ya ufisadi wale waliotimuliwa
 
Baada ya kumuoa maalim sasa 'mr love' anamnyemelea dj wa billz amvishe kitu cha Engagement!
 
Mbona waTZ mnaviherehere namna hii, kama jamaa kweli amekutana na Rais na amesema ataeleza yaliyo jadiliwa baada ya mazishi sasa nyie mnaharaka gani? Hapa JF kila mmoja anakuja na stori yake na Nyie wanaCDM humu JF kwanini hamna imani na viongozi wenu?

Subirini mazishi yaishe halafu ndio mje hapa kurusha madongo.

Nadhani watu wanajaribu kutoa yale wanayofikiria na matokeo yake, hivyo waache tu waendelee kufurahisha roho zao. Mbowe ndiye anayejua na atasema yeye mwenyewe kilichompeleka ikulu
 
Sasa hivi utasikia wazee wa "copy and paste" CUF nao wanataka kiongozi wao naye aitwe na JK waongee ingawa hawajui nini kilichoongelewa kati ya Mbowe na JK. Subirini muone...

Nani anaye copy and paste kati ya chadema na CUF

a. CUF walianzisha maandamano ya kudai tume huru 2001; chadema wakaiga maandamano kila kukicha

b. CUF waliamua kushirikiana na serikali; Chadema naona wameanza kunywa juice ikulu..and the process is ongoing..

mtafundishwa siasa hadi lini
 
Maybe, maybe not...Lakini usisahau kuwa Marehemu ndiye aliwapa ushauri wa kwenda kumwona JK, na kweli wakaenda, so inaonyesha alikuwa mtu mwenye spirit ama mwelekeo wa kutaka serikali ishirikishe wapinzani.Wanasema kwenye misiba watu hupatana na sometimes hubadilika.Kwa jinsi JK alivyozidiwa, anaweza akafanya kwasababu ataingia kwenye historia ya nchi kwa namna ya tofauti sana!Talking bout "Nitoke vipi?" lol
j mushi huwa napenda majibu yako kiukweli huwa yanaonesha kutulia fulani hivi. Pia huwa yanaonesha si mtu wa visasi. Big up.
 
kamanda mbowe usitufanyie yale mambo ambayo seif hamad alifanya na kuwasaliti wazanzibar, chonde chonde kamanda
 
..hiyo itakuwa sawa na Shekhe kuingia ubia kwenye biashara ya minofu ya nguruwe.

..CCM ilipofikia imekuwa ni HARAMU kabisa.
 
Nani anaye copy and paste kati ya chadema na CUF

a. CUF walianzisha maandamano ya kudai tume huru 2001; chadema wakaiga maandamano kila kukicha

b. CUF waliamua kushirikiana na serikali; Chadema naona wameanza kunywa juice ikulu..and the process is ongoing..


mtafundishwa siasa hadi lini

a. Swala la maandamano sio "copy and paste". Maandamano yalikuwa yanafanywa tangu enzi za mkoloni kudai uhuru. Labda kama wamecopy huko. b. Usitegemee hata siku moja CHADEMA wakakubaliana na aina hiyo ya ndoa...CHADEMA haitaki ndoa ya wake wengi. Inataka kufunga ndoa na wananchi tu, sio kama CCM wanafunga ndoa na wananchi halafu bado wanaongeza mke wa pili CUF na bado nyumba haikaliki. Wakioa wa tatu si ndio itaungua kabisa...
 
a. Swala la maandamano sio "copy and paste". Maandamano yalikuwa yanafanywa tangu enzi za mkoloni kudai uhuru. Labda kama wamecopy huko. b. Usitegemee hata siku moja CHADEMA wakakubaliana na aina hiyo ya ndoa...CHADEMA haitaki ndoa ya wake wengi. Inataka kufunga ndoa na wananchi tu, sio kama CCM wanafunga ndoa na wananchi halafu bado wanaongeza mke wa pili CUF na bado nyumba haikaliki. Wakioa wa tatu si ndio itaungua kabisa...

Nani mke na nani mume kati ya CUF, CCM na Chadema?

Unaongelea ushabiki tu, wanasiasa wanaingia kwenye siasa kutafuta madaraka (vyeo) otherwise hakuna sababu ya siasa..

Yetu macho nakwambia soon chadema itakuwa na serikali ya mseto na ccm, sasa siku hiyo utajua nani mume na mke katika vyama hivyo..lol
 
Jumapili iliyopita (15 Jan 2015), Rais JK na Mbowe walikutana kwa siri, kilichojadiliwa pia kikawa ni siri. Gazeti la kiukweli la kimombo' The citizen' limetoa nyeti hizo ukurusa wa mbele bila chenga. Mbowe akaulizwa kwa simu, naye akikri kuwa ni kweli walikutana. Alipoulizwa mlijadili nini akapiga chenga, subiri msiba uishe. Gazeti lilipowauliza wasemaji wa ikulu nao wakatoa nje. Lilipomwuuliza Mnyika wa kueneza chama kuhusu sakata hilo naye akasema hana habari.

Maswali
Je, Dr Slaa na viongozi wakuu wa Chadema wanajua kikao hicho? Kama hapana kwanini? Kama siyo, Mbowe atujibu haraka.
Pili, kikao cha kwanza cha ikulu ilikuwa public kwanini hii ya mbowe aifanye siri peke yake?
Je, JK anamshawishi mbowe aikubali mchakato feki wa katiba?
Je, kati yao Jk anawasaliti ccm au Mbowe anasaliti Chadema?


Habari yenyewe soma hapo chini.




Dar es Salaam. President Jakaya Kikwete and Chadema national chairman Freeman Mbowe held informal talks at State House in Dar es Salaam on Sunday, sparking speculation on the agenda. Mr Mbowe, also the leader of the opposition in Parliament, confirmed yesterday that they had a three-hour meeting but said he would give the details only after the burial of Chadema MP Regia Mtema, who died in a road accident at Ruvu in Coast Region on Saturday.

He spoke with The Citizen at the Karimjee Hall grounds, where he had joined tens of hundreds of people, including government leaders and leaders of political parties, to pay last respects to the MP, who died at the age of 32.

“It’s true that I met President Jakaya Kikwete over the weekend,” Mr Mbowe said. “We discussed issues but I cannot go into the details of what transpired between us. Try to find me after the burial of Mtema.” State House officials would not confirm the meeting, with the President’s assistant press secretary, Ms Premi Kibanga, saying she had been on leave and was not aware of such a meeting.

The air of secrecy did not go down well in some quarters, with a lecturer at the University of Dar es Salaam, Mr Bashiru Ali, accusing Mr Mbowe of “privatising democracy” in withholding the details of meeting.

Since Mr Mbowe was a follower of democratic principles of democracy, Mr Ali said, he ought to have publicly declared what was discussed. In politics, he added, there was no such thing as secret or informal talks.

“I suspect the talks centred on the process of remaking the constitution,” Mr Ali added. “Chadema leaders met the President in November last year on the issue and they principally agreed in some areas.” His colleague, Dr Azaveli Lwaitama, said every citizen was eager to know what they spoke about. But he speculated that the two leaders might have discussed the formation of the constitutional review commission that will collect views from the people.

“Basically, the President wants to appoint a constitutional review commission,” said Dr Lwaitama. “In order to avoid complaints from various quarters, he has to consult personalities such as Mbowe.”
The don speculated that President Kikwete might have met Mr Mbowe in order to avoid political barbs after he appoints the commission.

Chadema director for publicity John Mnyika said his party could not speak on administrative issues while mourning their departed colleague. “I cannot comment on anything now as the party’s attention is directed to the death of our special seats MP Mtema,” Mr Mnyika said. “Wait until we have settled down.”

His CCM counterpart, Nape Nnauye, said he had nothing to say as the meeting was between President Kikwete and Mr Mbowe. “I’m not an astrologer who can predict what transpired between the two personalities,” Mr Nnauye declared.
Chadema leaders held talks with President Kikwete in November 2011 and agreed on principle that the newly passed Constitutional Review Act 2011 bill needed major amendments.

A joint statement issued by the two sides at the end of two days of consultations said the bill should be improved so as to bring it up to the standards of building national consensus and cohesion.But President Kikwete went ahead and assented to the Bill a month later, drawing protests from Chadema and leaders of civil society organisations.

In November 2011, Chadema MPs walked out of Parliament in Dodoma as President Kikwete began delivering his speech to inaugurate the 10th Parliament. The President was forced to pause at the podium as Chadema legislators staged the walk-out, reportedly to demonstrate the opposition’s stand that it would not recognise the presidential results and the elected President.

Source:Mbowe in

My take: Maalim Seff na Karume walianza hivihivi.
JK hapendi migogoro ndio maana anakutana na viongozi wa upinzani ili Tanzania iwe mahala pema pa kuishi

Free na Jk wote ni watoto wa mjini,hawakukutana barabarani kama wengi mnavyofikiria,mambo mengi ya kimjini ya ujana wameyafanya pamoja,wanajuana,mtajisononesha bure wao wanajua wanchokifanya ndio mana nape na mnyika wote hawajui kinachoendelea!
 
Katiba inasema waziri awe mbunge, haisemi lazima atoke chama cha rais, hivyo katiba tuliyonayo inaruhusu mseto. Ila tu Waziri Mkuu ndio lazima atoke chama chenye wabunge wengi

bora yako uliyesoma katiba.
 
Muda si mrefu ntarudisha kadi yangu ya CHADEMA maana mambo haya ya vikao vya siri ndiyo yaliyoifikisha CUF hapa ilipofikia. Ole wako Mbowe na vikao kao vyako vya siri vya kutaka kutusaliti kwa kuhongwa Vyeo.
Ukirejesha kachukue ya TLP Mkuu
 
Mhe Mbowe, ndoa yoyote na CCM ni batili tangu kuanza kufikiriwa kwake hata kabla ya Rais Kikwete kulitekeleza hivyo sisi kama wenye chama tunalikataa right from the on-set of things kwa kuwa hatujawa consulted.

Letu ni kutafuta katiba mpya ya wananchi FULL STOP na wala si kutafuta vyeo vitakavyoishia kukiangamiza chama chetu.

CHADEMA kaeni mbali sana na hii CCM inayoelekea kufa kama ilivyowahi kutabiriwa na Hayati Mwalimu Nyerere; hatuna chetu mle na wazo la serikali ya mseto tukiachie KAFU; CDM we are above those petty political schemes kutafuta fedha za haraka -- strain your eyes on 2015 basi nchi tunawakabidhini hapo sisi vijana bila hiyana.

Mhe Mbowe, please stop that unholy CDM/CCM AND CUF UNIONISATION into a missionless pact.

Mseto wa Zanzibar misheni yake ilikua ni kuleta amani je hili la Bara ni kwamba tunatafuta kukamilisha nini baadaya wananchi kukashirikia ufisadi na uchakachuaji wa CCM??


Kuna uzi mmoja uliwahi andikwa humu jamvini uliokuwa ni tetesi juu ya mkuu wa wadanganywa kubadirisha BARAZA LA MAWAZIRI ifikapo mwezi wa tatu. Kutokana na kikao cha siri kilichofanyika kati ya mkuu wa wadanganywa na yule mkuu wa magwanda, nahisi walikuwa wanakubaliana kuhusu wabunge wa magwanda washirikishwe katika hilo baraza la mawa ziri. Msiniulize sosi maana sosi ni hisia zangu tu.
 
Back
Top Bottom