Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,502
- 113,610
MkuuPaskali unataka kutuambia kile ambacho ulishauri kwenye bandiko lako jana kina reflect kilichotokea kwenye uchaguzi? How? Katika hoja yako jana ulikuwa ukiwashauri na kuwabeza CDM kwamba wasiende kortini baada ya kutolewa taarifa kwamba CDM hawakutimiza matakwa ya kikanuni ikiwemo suala la gender balance. Lakini kabla CDM hawajaenda kortini wakawa wameruhusiwa kushiriki uchaguzi na kura zikapigwa kwa maana ya kwamba hoja ile ya kutofuatwa kwa kanuni haikuwa na mashiko kwa mujibu wa taratibu na sheria za uchaguzi wa EALA. Hii maana yake ni kwamba hata ushauri na kubeza kwako hakukuwa na mashiko!
Sasa CDM wanasema wanataka waende kortini kupinga kilichofanyika kwenye uchaguzi naona umeibuka tena ukitumia andiko hilo hilo la jana kama reference. Kinachonishangaza ni kwamba badala ya wewe uwaunge mkono CDM kwenda kortini (hata kama madai yao na yako yatakuwa tofauti kidogo) lakini bado unaendelea kuwaponda na kuwabeza!
Kama jana uliandika andishi refu ukiunga mkono uamuzi wa CDM kuwekewa ngumu kushiriki uchaguzi huo hadi wakidhi kilichodaiwa kuwa ni matakwa ya kikanuni, lakini baadaye wakaruhusiwa huoni kwamba uchaguzi ule ulifanyika pasipo kuzingatia taratibu za kikanuni zinazosimamia uchaguzi huo?
chabusalu hoja yangu ya jana, hapa CHADEMA Chama cha Ajabu Sana!.Kwenda Mahakamani Kwa Non Issue, Serious Issue ya Katiba ni UKUTA! ilihusu Chadema kutishia kwenda mahakamani kuusimamisha uchaguzi wa EALA, kisa ni kuzuiliwa kwa ukosefu wa gender balance, nikasema hiki ni chama cha ajabu sana, katiba imevunjwa ambayo ndio wangepswa kwenda mahakamani, badala yake walihamasisha maandamano ya UKUTA, nikawaandikia kuwauliza hivi uvunjaji wa katiba unapingwa kwa maandamano?.
Issue ya EALA ni ndogo na very simple, ilihitaji tuu, gender mainstreaming na inclusion, kama wabunge wanatakiwa kuwa na 1/3 ya wanawake, then kila chama lazima kilete 1/3 ya wanawake hata kama sio lazima wachaguliwe!. Hili ni hitaji la kikanuni, halina mjadala, hivyo kama kweli jana wangekwenda kuusimamisha uchaguzi mahakamani, wangekuwa ni watu wa ajabu sana!. Nikasema tatizo kubwa kabisa la Chadema, hawana ma strategists, kama nafasi zao ni mbili, na walijijua wanamtaka Wenje na Masha, then wangepeleka watu 6, wakiwemo wanawake wawili, hao wanne wangepeleka maboya, ili Masha na Wenje ndio wawe the best!. Kitendo cha nafasi zao mbili kisha wakapeleka watu hao hao wawili, ni kulilazimisha bunge kuwa a rumber stamp ya Chadema, na kwa vile wabunge had no choice to choose from, wakaamua kupiga kura za ndio na hapana!.
Kiukweli kilichofanyika kwenye selection ya Chadema ni madudu!, sasa kama wapenzi wa dhati wa Chadema mnaogopa kukiambia chama chenu, kuwa it got to do things right, hamkisaidii, nani anajua hao Masha na Wenje wamepatikanaje?, sasa kwenye issues ndogo ndogo kama hizi wanashindwa, wangekabidhiwa ikulu si ingekuwa chaos?. Kila nikilisoma bandiko hili la mwaka 2014 CHADEMA Ikipewa Nchi, October 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala wa Kidikteta? Nauliza Tuu!
nimejikuta niko right, sasa watu kama hawa kwenye issue ndogo kama hii, wanashindwa, halafu ndio watujie ile 2020 kuwaomba Watanzania wawakabidhi nchi?!.
Hoja ambayo ni valid na ina hold water ni double standard ya CUF A na B!. NB, viti wiwili vya Chadema bado vipo, wanatakiwa kuleta watu wengine wakiwemo wanawake, then bunge litawachagua hao wawili na sii lazima achaguliwe mwanamke. Wampeleke Salum Mwalimu na Kafulila, wawatafutie maboya 4 ya kuwasindikiza, hili jambo liishe, kama ni kesi, wakamshitaki mvunja katiba.
Paskali