Mbowe, Dr Slaa kulitikisa Jiji la Dar Jumamosi Ijayo

Mkuu mie Jumamosi takuwa uwanja wa taifa naangalia taifa stars...

Haina shida mkuu wangu sanasana wewe ukija Jangwani utakuwa unafanya fujo ili mkutano usisike vizuri...
 
Ukabila, Ukanda ndo unavyo viwaza katika kichwa chako hata kutizama kalenda tu kufahamu Tar. 26/05 ni siku ya Jmosi umeshindwa! Acha kukurupuka

Mkutano uko Dar, Mbowe na Slaa wanatoka Kask, Marando ni Kanda ya Ziwa, Zitto Kanda ya Magh, Lisuu kanda ya Kati,Arfi ni kutoka Nyanda za Juu,,,,na wengine wengi mchanganyiko, still unaongelea ukabila....SHAME UPON YOUR FACE
 
Viongozi wakuu wa CDM wakiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa Jumamosi ijayo tarehe 26/05/2012 watalitikisa jiji kuu la Dar kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya Jangwani.

Mkutano huo utakuwa ni maalum kuzungumza na kuwaelimisha wananchi kuhusiana na Katiba mpya. Pia viongozi hao wanatarajiwa kulaani uamuzi wa halmashauri kuu ya CCM kutenga mambo kadhaa na kuwaamuru wananchi kutoyajadili kwani yanapaswa kubaki kwenye katiba kama yalivyo.

Mkutano huo pia utahudhuriwa na Naibu katibu mkuu Zitto Kabwe, Mnadhimu mkuu wa upinzani Tundu Lissu, Mwanasheria maarufu Mabere Marando,wabunge wote wa chama hicho na wajumbe wote wa kamati kuu.

Itakumbukwa mara ya mwisho CDM kufanya mkutano mkubwa kama huo Dar ni siku ya uzinduzi wa kampeni za mgombea urais wa chama hicho mwezi Agosti mwaka juzi.

Mkutano huo unatarajiwa kulitikisa jiji la Dar na Taifa kwa ujumla kwani Maelfu ya wana-CCM wanatarajiwa kuvua Gamba na kuvaa Gwanda.

Source: John Mnyika-CDM

Kwenye Mkutano huo awepo SHIBUDA ili atangaze nia yake ya kugombea Urais 2015 siyo kwenye kamati ya CCM. Akifanya hivyo hutasikia malalamiko juu yake, mie nitahamasisha wenzangu ili tuhudhurie mkutano huo muhimu.
 
Watumiaji wa airtel kuna sms za bure na wale wa voda ni 25shs per sms vilevile na tigo wewe andika ujumbe ukiwajulisha watu kuhusu hii show na wale wazee wakufacebuuka weka weka hii habari kwenye profile/hall yako na shere na marafiki zako
Vua gamba vaa gunda
 
Tunashukuru kwa taarifa.Sio lazima mtu uchangie humu kama una point. Maana kuna watu wao kila siku ni kuzungumzia ukabila na ukanda tu wakati ukweli wanao wenyewe.
 
Niliona mwamko walionao watu wa kuangalia Star TV, wakati mkutano wa CHADEMA uliporushwa mojamoja kupitia TV hiyo wakati wa ufunguzi wa kampeni pale ARUMERU.
kwa vile tukio la JUMAMOSI ni zaidi ya lile la ARUMERU ni vema basi Uongozi ukafikiria kurusha moja kwa moja mkutano huo, ili kuweza kuwafikia watu wengi zaidi ya wale, kwa sisi tutaokuwa mikoani hiyo JUMAMOSI tunashauku kubwa ya kujua nini viongozi wetu wataongea tunataka kujua na kufuatilia kila neno litakalotolewa na viongozi wetu, kama itashindikana kurusha kwenye TV basi radio zitumike ili wananchi wote wapate fursa ya kujua nini viongozi wetu wanatuletea. Na hii itarahisisha sana kampeni hii kwa chama chama.

Wana JF nawasilisha
 
Naunga hoja mkono kwani hata sisi makamanda wa Rorya tunatamani kufuatilia ikiwezena live tukio hilo la kitaifa!
 
Naunga hoja mkono kwani hata sisi makamanda wa Rorya tunatamani kufuatilia ikiwezena live tukio hilo la kitaifa!

Ni wazo zuri,bila shaka uongozi watalifanyia kazi, pia nashauri yafanyike matangazo kwenye vyombo vya habari na magari yapite kuwatangazia watu kuhusu mkutano j.osi,kwani wengi watakuwa hawana taarifa
 
Jamani tusisahau kubeba viroba jumamosi kwa ajili ya kujaza kadi za magamba watakaokuwa wanajivua magamba!!sipati picha mpaka mwanangu mdogo atapiga kombati uhh itatisha.
 
Jamani tusisahau kubeba viroba jumamosi kwa ajili ya kujaza kadi za magamba watakaokuwa wanajivua magamba!!sipati picha mpaka mwanangu mdogo atapiga kombati uhh itatisha.

Kutakuwa na mapipa Jangwani mkuu....
 
Back
Top Bottom