Mbowe, Dr Slaa kulitikisa Jiji la Dar Jumamosi Ijayo

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Viongozi wakuu wa CDM wakiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa Jumamosi ijayo tarehe 26/05/2012 watalitikisa jiji kuu la Dar kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya Jangwani.

Mkutano huo utakuwa ni maalum kuzungumza na kuwaelimisha wananchi kuhusiana na Katiba mpya. Pia viongozi hao wanatarajiwa kulaani uamuzi wa halmashauri kuu ya CCM kutenga mambo kadhaa na kuwaamuru wananchi kutoyajadili kwani yanapaswa kubaki kwenye katiba kama yalivyo.

Mkutano huo pia utahudhuriwa na Naibu katibu mkuu Zitto Kabwe, Mnadhimu mkuu wa upinzani Tundu Lissu, Mwanasheria maarufu Mabere Marando,wabunge wote wa chama hicho na wajumbe wote wa kamati kuu.

Itakumbukwa mara ya mwisho CDM kufanya mkutano mkubwa kama huo Dar ni siku ya uzinduzi wa kampeni za mgombea urais wa chama hicho mwezi Agosti mwaka juzi.

Mkutano huo unatarajiwa kulitikisa jiji la Dar na Taifa kwa ujumla kwani Maelfu ya wana-CCM wanatarajiwa kuvua Gamba na kuvaa Gwanda.

Source: John Mnyika-CDM
 
Tumesubiri muda mrefu sana kupata hii fursa adhimu kusikiliza wanamageuzi, tunaomba Mnyika mtupe taarifa za kina kama mkutano utaanza saa ngapi, wapi tukanunue magwanda, bendera nk,
 
posho posho posho mbowe na slaa kila wakiishiwa pesa lazima waandae mikutam na maandamano ili walipane
 
posho posho posho mbowe na padri slaa kila wakiishiwa pesa lazima waandae mikutam na maandamano ili walipane

Huna jipya zaid ya kuona tabu na mkutano huo.posho unalipa wewe?Wakijilipa kuna tabu gani kama wanatoa somo kwa wananchi?Toa pumba zako.
 
Dar ni wastaarabu hatutaki fujo na wala hatutaki kupigania ukombozi wa watu wa kaskazini, watajaa wachaga ndio maana wameweka jpili wachaga watakuwa wamefunga maduka.
Ohooo chama! chama gani chama cha wananchi Cuf! - X 2....mapanga shaa shaa!
Sasa hakuna cha ngangali wala jino kwa jino mmebaki mavi matupu. RIP CUF!
 
Redio ya Arusha mambo mtarusha matangazo live ili wa mikoani tupate matangazo live? Wahusika naomba mtujuze ili kam hayatarushwa live na sisi tujisogeze dar. Tafadhali wahusika tunaomba majibu
 
Dar ni wastaarabu hatutaki fujo na wala hatutaki kupigania ukombozi wa watu wa kaskazini, watajaa wachaga ndio maana wameweka jpili wachaga watakuwa wamefunga maduka.

Ukabila, Ukanda ndo unavyo viwaza katika kichwa chako hata kutizama kalenda tu kufahamu Tar. 26/05 ni siku ya Jmosi umeshindwa! Acha kukurupuka
 
Viongozi wakuu wa CDM wakiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa Jumamosi ijayo tarehe 26/05/2012 watalitikisa jiji kuu la Dar kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya Jangwani.

Mkutano huo utakuwa ni maalum kuzungumza na kuwaelimisha wananchi kuhusiana na Katiba mpya. Pia viongozi hao wanatarajiwa kulaani uamuzi wa halmashauri kuu ya CCM kutenga mambo kadhaa na kuwaamuru wananchi kutoyajadili kwani yanapaswa kubaki kwenye katiba kama yalivyo.

Mkutano huo pia utahudhuriwa na Naibu katibu mkuu Zitto Kabwe, Mnadhimu mkuu wa upinzani Tundu Lissu, Mwanasheria maarufu Mabere Marando,wabunge wote wa chama hicho na wajumbe wote wa kamati kuu.

Itakumbukwa mara ya mwisho CDM kufanya mkutano mkubwa kama huo Dar ni siku ya uzinduzi wa kampeni za mgombea urais wa chama hicho mwezi Agosti mwaka juzi.

Mkutano huo unatarajiwa kulitikisa jiji la Dar na Taifa kwa ujumla kwani Maelfu ya wana-CCM wanatarajiwa kuvua Gamba na kuvaa Gwanda.

Source: John Mnyika-CDM

Tedo like this.
 
Back
Top Bottom