Mbowe amkaribisha rasmi Lowassa CHADEMA

Amekidhalilisha Chama Na UKAWA.Kwa Falsafa Yake Mbovu Ya Kutegemea Makapi Ya CCM Yamsaidie Kumpeleka Ikulu.
Mbowe Anamjua Sana Lowassa Kama Ni Kiongozi Bora Kuliko CCM Iliyomlea Kwa Zaidi Ya Miaka40.

Hawaeleze Watanzania Kua Amekubali Kununuliwa Kwa Gharama Ipi Na Nani Atailipa.Pesa Ya Mafisadi Walioitumia Kuwekeza Kwake Uwa Haipotei Bure.
Napata sheeda kuelewa mpaka sasa sijawahi ona duniani mtu akahama chama usiku afu hajui misingi ya chama na asubuhi asubuhi anaaminiwa kugombea wadhifa mkubwa ndani ya chama? Hii imani imetoka wapi na tangu lini? Watz tufanye tathmini na si ushabiki usiokuwa na tija...
 
Mhe.Mbowe Jiandae Kuwajibika Katika Hili Kwa Watanzania.

Mpasuko Unaoendelea Sasa Katika UKAWA Ni Matunda Ya Maamuzi Yako Mabovu Yaliyokosa Ridhaa Ya Pamoja Ya Viongozi Wenzako.Maamuzi Yako Yaliyokua Na Lengo La Kuwaburuza Viongozi Wenzio Kifikra Na Kimaamuzi.Na Maamuzi Yako Yaliyofishwa Na Tamaa Yako Ya Uroho Wa Madaraka Na Kukubali Kununuliwa.

Kitendo Cha Kumkaribisha Fisadi Papa No.1 Mhe.Lowassa Ndani Ya UKAWA Na Kupewa Nafasi Ya Kuteuliwa Kama Mgombea Uraisi Bila Ya Maridhiano Thabiti Kutoka Kwa Viongozi Wenzio.Kumekufanya Wewe Uwe Fisadi Papa No.11(Haukuwepo Kwenye Listi Ya Awali Ila Sasa Upo).Na Watanzania Wanatakiwa Kukuogopa Kama Ukoma.Kwa Kuweka Maslahi Yako Mbele Kuliko Maslahi Ya Taifa.

Kama Bado Unaamini Kua Kuondoka Kwa Dr.Slaa Na Prof.Lipumba Ndani Ya UKAWA Hakuna Madhara Yeyote kwa UKAWA.Basi Ukae Ukijua Kua Uko Ni Kujidanganya Na Kujilisha Upepo.

Malipo Ya Usaliti Huu Kwa Viongozi Wenzio
Yatakua Ni Kuanguka Kwako Mwezi October Na Kuporomoka Kwako Kisiasa.Na Ujiandae Kwa Aibu Kubwa
Enheee hiyo list ya mafisadi papa itaja hapa we ndorrrrrrooobbboo
 
unalala sebuleni ,unaishi kwa shemeji yako,unakula mlo mmoja,hujui kesho utakula nini,wanao wanakkaa chini darasani,kumuona daktari elf 5 hospitali ya serikali,mwanao amemaliza degree anosha vyombo nyumbani,daladala unapanda huku unanusa vikwapa vya watu hakuna pa kupumulia,unalala chumba kimoja na wanao,unalima unakosa pa kuuza,umejenga nyumba kwenye kiwanja cha kata hapa na simamama pale,halafu bado unaipenda CCM iendelee kukuongoza lazima tukupime akili yako
 
ukweli mtupu umeongea

Chadema chama cha mafisadi kinaongozwa na mafisadi makubwa mawili ambayo ndiyo chimbuko la ufisadi.
 
Mwanzoni nilidhani JF ni Real Home of Great Thinkers.....Kumbe kila mtu anaweza kukaa chini na kuandika anachojisikia akijitahidi kusambaza chuki za kufikirika na kuacha kufikiri kwa kina na kukitetea anachokipenda hata kama ni kibovu. Leo asubuhi pia nimemsikiliza somebody Bana nadhani ni prof huyu ila nae amemezwa huko huko.

Natarajia wasomi wawe msaada na kuchambua mada kwa hoja na utafiti ila vimebakia vioja na ushabiki
Pole Mama Tanzania, Pole JF
Kila mtu ana mtizamo na mawazo yake kwa kadiri ya upeo wake wa kuyaona mambo mbalimbali... yawezekana upeo wako pia ni mdogo kwa mtizamo wako km angeliuona uzi wako... muda wa kuwa bendera fata upepo uishe na baadala yake tuwaze kwanini haya mambo yanatokea baadala ya kukaa na kuwatuhumu watu.... Swali rahisi la kujiuliza ni kuwa kama Prof Lipumba ni mwanzilishi na mbunifu wa jina la UKAWA katoka.... tatizo ni nini?
 
Mbowe ametuuza kwa vipande vya shekeli kwa tamaa ya madaraka. Hafai kabisa kiongozi wa namna hii Kama kuitafuta ikulu kaitafuta kwa fedha akiingia si watamaliza kila kitu hawa.

Naomba nikutambulishe humu ndani rasmi, wewe ni gamba la Lumumba(ccm)
 
Najaribu kutazama jinsi kenyata na ruto walivyoandamwa na kashfa kibao za matukio ya mauaji ya mwaka 2007

baadae namuangalia kenyata na kashfa yake na baba yake kwa kuwanyang'anya wakenya wengi ardhi huko kikuyu highland lakini sasa ndiye raisi

pamoja na kuwa na kashfa kibao namuona kama rais pekee aliyeipeleka puta kenya katika maendeleo zaidi ya marais wote waliotangulia huku uchumi wao ukikua maradufu

kwa mantiki ndogo kama hiyo niko radhi lowasa aingie madarakani hata kama ni fisadi ili

1) kuondoa utawala wa ccm madarakani na kisiwepo chama kinachoamini kuwa kitatawala milele kama ccm wanavyodhani

2) kubadilisha uongozi wa nchi utaifanya hata ukawa itakayoingia madarakani itende mambo kwa umakini huku ikijua baada ya miaka mitano inaweza ondolewa madarakani

nb: Nataka asiwepo mtawala wa milele kama ccm na Lizaibon wanavyoamini kuwa wao hawawezi kuanguka na hilo litafanya kila atakayepewa madaraka kufanya mambo kwa uhakika huku akijua akilegalega miaka mitano inayofata ataondolewa

kura yangu ni ukawa

kalichumbage

Hili la Kenya hulijui ni bora kujinyamazia tuu! Sasa hivi Kenya unajua kuna mjadala wa kuondoa ukomo wa Urais ili Kenyata awe rais wa Maisha kama Museveni wa Uganda na Kagame wa Rwanda!!! Kibaki kajenga uchumi Kenya, Kenyata keshafanya nini?? Usilolijua ni kama usiku wa giza!!
 
Ukiona watu wanatumia jazba badala ya kuanfika hija ujue wameshashindwa. Naona wapenzi wa ccm tunatumia jazba kana kwamba tumeshashindwa. Tukubali tusikubali hii ni dakili njema kwa UKAWA.
 
Wewe ndio unasema ila bibi yako kule kijijini hajui hayo mambo tena bado anajua kikwete anachaguliwa tena...na wewe kwa sababu ya iyo android yako bila hivyo pia ungekua CCM kama unabisha mpigie simu bibi muulize kula unampa nani uje useme hapa peupe...hamna wa kuitoa CCM kwa kuunga unga huku hata mie siwapi kura yangu hao wa kuunga unga...

Bibi yangu kule Kijijini kabisa Kirando Wilaya Nkasi anaomba Mungu amjalie angalau aishi mpaka tarehe 25 October apige kura kuiondoa CCM then ndio afe kwa madhila na taabu anazozipata chini ya utawala huu.
 
Ukiona watu wanatumia jazba badala ya kujenga hoja ujue wameshashindwa. Naona wapenzi wa ccm tunatumia jazba kana kwamba tumeshashindwa. Tukubali tusikubali hii ni dakili njema kwa UKAWA.
 
Hili la Kenya hulijui ni bora kujinyamazia tuu! Sasa hivi Kenya unajua kuna mjadala wa kuondoa ukomo wa Urais ili Kenyata awe rais wa Maisha kama Museveni wa Uganda na Kagame wa Rwanda!!! Kibaki kajenga uchumi Kenya, Kenyata keshafanya nini?? Usilolijua ni kama usiku wa giza!!
hata hivyo ni kwamba Mpaka sasa CCM imeendelea kutengeneza miswada ambayo itaihakikishia kuwa Chama cha Siasa Cha Kutawala MAisha.!! Kwa Taarifa YAko;...CCM Haina mpango wa kung"atuka Madarakani ili kuachia vyama vingine viongoze. Inatumia mabilioni kutekeleza azma hiyo. Inatunga hadi miswada mibovubovu bungeni, hatuna tume huru ya uchaguzi, inatumia jeshi kupiga wananchi, waandishi wa habari, na Kuua Upinzani, .. Ni kama hujaitazama CCm vizuri. Ifanyie tathmini Upya.

UkAWA ndiyo sera Lowasa anaenda kuitekeleza achukuapo ofisi. Ili kutupatia katiba ya wananchi itakayoleta demokrasia ya ushindani. CCM hawajaweza kutupa katiba hiyo na hawataweza, cause hawana mpango huo wala dhamira hiyo hawana.Tumekua taifa la Hofu, Tanzania Bila CCM inawezekana
 
haa haa eti dini una dini wewe? hizo za kuletewa na wageni...

Simaanishi dini hizo kwasababu kuna imani ambayo kila mtu anazaliwa anayo kwamba kuna nguvu fulani, hiyo ndo imani ..naweza kuwa nisiwe na dini fulani lakini naamini kuna nguvu fulani ..sasa amani hiyo nikizaliwa naiunganisha na dini yangu naona vinaendana na hapo ndo imani yangu inahimarika zaidi ..mwisho wa siku naamini katika dini fulani ..usiwe mwepesi wa kukariri dogo, Safisheni huko kwenye dini yake lutherani labda watakuwa wamewapa CDM uwezo wa kutakasa watu ili muisaidie kanisa kazi yake
 
hata hivyo ni kwamba Mpaka sasa CCM imeendelea kutengeneza miswada ambayo itaihakikishia kuwa Chama cha Siasa Cha Kutawala MAisha.!! Kwa Taarifa YAko;...CCM Haina mpango wa kung"atuka Madarakani ili kuachia vyama vingine viongoze. Inatumia mabilioni kutekeleza azma hiyo. Inatunga hadi miswada mibovubovu bungeni ,Hata takrima iliwekwa ili wafikie lengo.. Ni kama hujaitazama CCm vizuri. Ifanyie tathmini Upya.

UkAWA ndiyo sera Lowasa anaenda kuitekeleza achukuapo ofisi. Ili kutupatia katiba ya wananchi itakayoleta demokrasia ya ushindani. CCM hawajaweza kutupa katiba hiyo na hawataweza, cause hawana mpango huo wala dhamira hiyo hawana.Tumekua taifa la Hofu, Tanzania Bila CCM inawezekana

Hoja nzuri kuwa Ukawa watasimamia rasimu ya Warioba. Hata hivyo Lowasa hajawahi kutamka hadharani kwenye suala la Katiba yuko Upande gani na wanaomjua kwa hulka yake ya kupenda sana madaraka haielekei kuwa Lowasa ndo mtu anayefaa kusimamia hoja hiyo. Tusisahau Lowasa maisha yake yote toka ujana hadi anakuwa mzee yamekuwa ni CCM. Wiki chache kabla ya kuhama alitamka kuwa maisha yake ni CCM.

Hilo linathibitishwa na jinsi ambavyo amekuwa akiongea baada ya kuhamia Ukawa. Zaidi sana amekuwa akilalamikia uonevu aliofanyiwa akiwa CCM. Wengi wanaweza kukubaliana naye. Hata hivyo alikuwemo CCM akiwa kiongozi mwandamizi ndani ya chama hicho kwa Miaka mingi mno. Ni vigumu sana kuamini kama Lowasa anaweza akafanya mambo tofauti na alivyofanya akiwa CCM kuliko kuamini kuwa Magufuli anaweza akafanya mambo tofauti. Magufuli hakuwahi hata kuwa kiongozi wa tawi - entirely ni mtu mpya kabisa katika safu za kiutendaji za CCM na anaweza akaja na jipya kuliko Lowasa ambaye kuwepo kwake kwenye "top ranks" za CCM kwa muda mrefu kuna mfanya awe CCM zaidi kuliko hata Magufuli. Litakuja lile swali walilokuwa wakiulizana wana reformation baada ya mpasuko ndani ya Kanisa miaka ile kuwa "is Luther a Lutheran??".

Baada ya Lowasa kuingia Chadema, anaonekana kubeba hoja za ki CCM CCM zaidi kuliko hata wale waliobaki CCM. Swali litakuwa "Is Lowasa representiing Ukawa ideals??". Hapo wengi tumejikwaa na hatuoni Lowasa akisimamia hoja za Ukawa. Sana sana kuwepo kwake ukawa kunaifanya CCM iliyobaki iungane zaidi kuliko ilivyokuwa huko nyuma. Jambo hili ni baya zaidi. Mpasuko uliokuwemo ndani ya CCM ndio wengi tulitarajia kiisaidie sana Ukawa. Sasa hivi CCM wana "re-group" wakati Ukawa imepoteza nyota wake wakuu. Hili si jambo la kudharau hata kidogo. Wale wanaopiga makelele tu kuwa Ukawa itashinda si vibaya wakafanya analysis isiyo na chembe ya unafiki huko Majimboni.
 
Napata sheeda kuelewa mpaka sasa sijawahi ona duniani mtu akahama chama usiku afu hajui misingi ya chama na asubuhi asubuhi anaaminiwa kugombea wadhifa mkubwa ndani ya chama? Hii imani imetoka wapi na tangu lini? Watz tufanye tathmini na si ushabiki usiokuwa na tija...

Hata Kanisani Mchungaji Mgeni Akija Hupewa Kindi Cha Kuendesha Ibada
 
Mhe.Mbowe Jiandae Kuwajibika Katika Hili Kwa Watanzania.

Mpasuko Unaoendelea Sasa Katika UKAWA Ni Matunda Ya Maamuzi Yako Mabovu Yaliyokosa Ridhaa Ya Pamoja Ya Viongozi Wenzako.Maamuzi Yako Yaliyokua Na Lengo La Kuwaburuza Viongozi Wenzio Kifikra Na Kimaamuzi.Na Maamuzi Yako Yaliyofishwa Na Tamaa Yako Ya Uroho Wa Madaraka Na Kukubali Kununuliwa.

Kitendo Cha Kumkaribisha Fisadi Papa No.1 Mhe.Lowassa Ndani Ya UKAWA Na Kupewa Nafasi Ya Kuteuliwa Kama Mgombea Uraisi Bila Ya Maridhiano Thabiti Kutoka Kwa Viongozi Wenzio.Kumekufanya Wewe Uwe Fisadi Papa No.11(Haukuwepo Kwenye Listi Ya Awali Ila Sasa Upo).Na Watanzania Wanatakiwa Kukuogopa Kama Ukoma.Kwa Kuweka Maslahi Yako Mbele Kuliko Maslahi Ya Taifa.

Kama Bado Unaamini Kua Kuondoka Kwa Dr.Slaa Na Prof.Lipumba Ndani Ya UKAWA Hakuna Madhara Yeyote kwa UKAWA.Basi Ukae Ukijua Kua Uko Ni Kujidanganya Na Kujilisha Upepo.

Malipo Ya Usaliti Huu Kwa Viongozi Wenzio
Yatakua Ni Kuanguka Kwako Mwezi October Na Kuporomoka Kwako Kisiasa.Na Ujiandae Kwa Aibu Kubwa

Ndugu yangu unavyoongea ni kama mtu uliye ndani ya chupa na ukafungiwa huko.Jiulize kwanini Lipumba ameondoka ghafla bila hata ya kuaga?Hujiulizi kesi yake imekwisha lini au imeshafutwa?Kaondoka na ndege gani?

Kwa sasa VIJANA wameshaichoka sana CCM ,kiasi kwamba wako tayari kumpigia hata SHETANI kama ataiondoa CHICHIEM madarakani!!!!!!!!Ukishaona hivyo ujue hata Lipumba alijua kitakachomkuta endapo ataendeleakukaa bongo..

Kama Mbowe ni fisadi tueletee evidnce na facts!!!!!11Halafu utuambie na Nape aliyehongo ili kupita kwenye kura za maoni za CCM anatofauti gani na huyu mnayemnanga kila siku eti MROHO wa MADARAKA?Sasa kama Lowassa ananunua MADARAKA na NAPE amefanya nini?

Ukitaka kutoa Kibanzi kwenye jicho la mwenzako,basi toa kwanza boriti kwenye jicho lako.Na ndivyo ilivyo CCM ilitakakuona UCHAFU wa UKAWA basi ianze kusafisha UCHAFU wake ambao nina uhakika hawawezi kufanya
 
unalala sebuleni ,unaishi kwa shemeji yako,unakula mlo mmoja,hujui kesho utakula nini,wanao wanakkaa chini darasani,kumuona daktari elf 5 hospitali ya serikali,mwanao amemaliza degree anosha vyombo nyumbani,daladala unapanda huku unanusa vikwapa vya watu hakuna pa kupumulia,unalala chumba kimoja na wanao,unalima unakosa pa kuuza,umejenga nyumba kwenye kiwanja cha kata hapa na simamama pale,halafu bado unaipenda CCM iendelee kukuongoza lazima tukupime akili yako

Na hao wenye good life wanaongozwa na chama gani. Acha kusingizia ccm kufeli kwako kimaisha. Unafikiri utaletewa maisha kwenye silver plate?
Kazi kushinda jf.
 
Back
Top Bottom