Mbona harakati za kuidai Zanzibar huru ni kama zimekufa awamu hii?

Kwa muda mrefu tangu muungano wa Tanganyika na Zanzibar hawa ndugu zetu kutoka Zanzibar wamekuwa hawaridhishwi na huu muungano, inasemakena hadi Rais wa kwanza wa Zanzibar alishawahi sema muungano ni kama koti likikubana unalivua.

Pia nakumbuka awamu ya 4, Rais akiwa Kikwete kuliibuka wimbi kubwa sana la wanaharakati kutoka Zanzibar wakiongozwa na jumuia ya UAMUSHO wakidai Zanzibar inatakiwa kuwa huru eti kisa viongozi wao wanachaguliwa kutoka Tanganyika.

Lakini jambo la ajabu awamu hii ya sita ni kama hakuna tena hizi harakati za kuvunja muungano wetu mtukufu sasa najiuliza je, shida ilikuwa nini kwa hizi harakati na imekuaje awamu hii zisisikike tena? Au ulikuwa ni unafiki tu wa wanasiasa na sasa hivi wameona huu muungano unawanufaisha na wao!

Kwa mtazamo wangu muungano huu Zanzibar ndiyo wana manufaa kuliko Watanganyika hivyo wanapaswa kuupigania ili uendelee na wao wazidi kunufaika.

Mzanzibar ana haki ya kumiliki ardhi Tanganyika wakati Mtanganyika hana hiyo haki Zanzibar. Je, nani hapo ananufaika? Nawaomba tena Wanzanzibar waache unafiki huu muungano wao ndiyo wanufaika.

MUUNGANO UDUMU MILELE.
 
Niliwahi kusimuliwa na Mzee mmoja ambaye alikuwemo kwenye Bunge la wakati wa Muungano, kisa kimoja cha utani kuhusu Mzee Abeid Amani Karume, mara tu baada ya Muungano, mwaka 1964.

Kisa hicho kinasema kuwa, mara baada ya Muungano, Mzee Karume aliulizwa na Wazee wenzake Zanzibar, kwenye Bao, kuwa imekuwaje amekubali kumezwa na Mwalimu Julius Nyerere?

Mzee Karume akawajibu Wazee wenzake, kuwa, "Yakhe, Julius nishamzidi akili. Yeye akija kwangu, (Unguja), anaishia Sebuleni, wakati miye nikienda kwake, (Tanganyika), naingia mpaka Chumbani anakolala".

Na kweli.

Mzanzibari anatutawala Watanganyika, kwa kila kitu, kama Rais wa JMT, wakati Mtanganyika hawezi kuwa Rais wa Unguja, asilani.
Huku ndio kuendeleza mawazo ya kimaskini. Bara ni kubwa sana kulinganisha na visiwa vya pwani yake.

Ni aibu kuanza kudai haki Zanzibar wakati eneo lao ni kama mkoa mmoja tu wa bara.
 
Ni wepi wenye zanzibar halisi kati ya wanaosema wamepindua na wale ambao wamepinduliwa ?
Makundi yote mawili ndio wenye Zanzibar.
Walio pinduliwa ni Wazanzibar
Sultan Jesmshid baba na babu yake wamezaliwa Zanzibar wenye asili za kiarabu .mama yake ni Mmanyema kutoka Tanganyika (Tanzania bara)
Alie kuwa Waziri mkuu Shamte ni Mpemba wa vizazi vingi.
Walio pindua kuna wazanzibar wakisaidiwa na wageni
Kina babu, Khanga ni washirazi wa Unguja kumbuka washirazi ni watu wenyeasili ya Iran 🇮🇷
Wangeni ni kina John Okello Uganda 🇺🇬 Mfaranyaki Frm Tanganyika.

Hiyo ndio biriani ya Zanzibar Revolution
 
Huku ndio kuendeleza mawazo ya kimaskini. Bara ni kubwa sana kulinganisha na visiwa vya pwani yake.

Ni aibu kuanza kudai haki Zanzibar wakati eneo lao ni kama mkoa mmoja tu wa bara.
Hoja yako ya udogo wa Zanzibar na ukubwa wa Tanganyika ina mashiko, lakini ninapata kigugumizi kuikubali.
Kwa nini Mtanganyika akataliwe kumiliki ardhi Zanzibar wakati Mnzanzibari anaruhusiwa kumiliki ardhi Tanganyika?
Hapo tunadumisha umoja?
 
Hoja yako ya udogo wa Zanzibar na ukubwa wa Tanganyika ina mashiko, lakini ninapata kigugumizi kuikubali.
Kwa nini Mtanganyika akataliwe kumiliki ardhi Zanzibar wakati Mnzanzibari anaruhusiwa kumiliki ardhi Tanganyika?
Hapo tunadumisha umoja?
Ndio udogo wenyewe wa visiwa kukataliwa kumiliki ardhi Zanzibar. Ardhi imeisha huku bara mpaka utake kuimiliki ya kule Zanzibar?.
 
Hoja yako ya udogo wa Zanzibar na ukubwa wa Tanganyika ina mashiko, lakini ninapata kigugumizi kuikubali.
Kwa nini Mtanganyika akataliwe kumiliki ardhi Zanzibar wakati Mnzanzibari anaruhusiwa kumiliki ardhi Tanganyika?
Hapo tunadumisha umoja?
Kiu harisia Mtanganyika unauziwa Ardhi wa Zanzibar Wana njaa wanauza Sana Ardhi kwa wageni kutoka ulaya Yani wamediriki kuuza mpaka maeneo ya kuzikia kwa wazungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie sioni kama zimekufa wala kufifia, kama mzanzibari msimamo wangu juu muungano uko pale pale. Sijawahi kuunga mkono wala kupenda muungano, wala sioni faida yake yoyote.

Naamini katika mashirikiano baina ya Tanganyika na Zanzibar, sawa na nchi nyengine yoyote ile kama Kenya, Uganda, Oman, Comorro n.k. Mashirikiano baina ya Zanzibar na taifa jengine lolote yasiathiri utambulisho wa mzanzibari wala utamaduni wake kama taifa huru.

Hakuna ulazima wa muungano baina ya nchi mbili hizo, zinaweza kushirikiana na kila moja ikafanya shughuli zake bila ya msuguano au muingiliano uliopo sasa ambao umekuwa kikwazo kama sio kisiki!
Nadhani Zanzibar ni uchochoro wa kutenda ualifu. Hivi CAG wakule huwa ni nani??
 
Back
Top Bottom