Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,150
- 18,810
Kuna wingu zito linalozidi kutanda juu ya suala zima la afya ya Prof. Mwandosya, ambaye aliugua ghafla wakati wa kikao cha Bunge cha hivi karibuni na kukimbizwa Muhimbili na hatimaye India kwa matibabu. Bila shaka wengi tumeona posts juu ya ziara za mkuu wa dola katika wizara, na waraka unaosemwa kutumwa kwa Nape, kuwa inaonekana huyu Prof. bado ni tishio kwa baadhi ya kambi ndani ya CCM katika suala zima la nani atashika hatamu za kugombea uraisi kwa ticket ya CCM. Katika posts nyingi kwenye JF wengi wamekiri kwamba Prof Mwandosya ana kichwa makini, na kwamba katika kipindi chote cha uwaziri wake amejidhihirisha kuwa mtu makini na mchapa kazi, anayeheshimika ndani na nje ya mipaka ya TZ. Hata kuna post iliwekwa kwamba mkuu wa dola anamuogopa Prof Mwandosya na hawezi hata kuthubutu kumbwabwajia kama anavyowafanyia mawaziri wengine. Wengine hata wameripoti kwamba ngamia alishachinjwa jangwani ili kumfanyizia na ikagonga mwamba!
Habari zinazompamba na kumweka katika duru ya wagombea wa uraisi (kama una habari tofauti tafadhari tueleze) ni pamoja habari kwamba Mwandosya alijitoa Wizara ya Nishati wakati mkuu wa dola akiwa waziri pale kwa kuwa alimwona mkuu wa dola kuwa "mtupu" mno na akasema hawezi kufanya kazi naye. Na pia kuna taarifa rasmi kwamba Mwandosya ndiye aliyem-groom Patrick Rutabanzibwa baada ya kuona utendaji wake makini. Hii inamfanya aonekane kama siku nyingi aliona weakness za mkuu wa dola ingawa wengi hawakuona hili.
Pia kuna taarifa zinazosema Prof alijipatia sifa kubwa katika duru ya mijadala ya "climate change" wakati wa mjadala wa Makubaliano ya Kyoto, kiasi kwamba Makamu wa Raisi wa Marekani wakati huo Al Gore alimtaja kuwa mmoja wapo wa waafrika wenye akili sana, na Bill Clinton wakati wa ziara yake Tanzania alimshauri Mkapa amtumie katika baraza lake la mawaziri. Hii ilikuwa ni baada ya Prof Mwandosya kutumikia katika mazungumzo hayo kama Spokesman wa G77 and China. Kutokana na umakini wake inasemekana Marekani walimwalika Washington kama mgeni rasmi wa "State Department" na kumwalika kutoa hotuba katika vyuo vikuu kadhaa.
Kulikuwa na jitihada za kumhusisha na kashfa ya unununzi wa rada, na inasemekana ziligonga mwamba kwa kuwa hakuhusika, japo yeye ndiye aliyetumiwa na serikali kuwashawishi wawakilishi wa Uingereza kwamba ni kweli Tanzania ilihitaji rada hii japo unnuzi wake ulikuwa na mushkeli.
Wengi wa mawaziri ukiwauliza juu ya Prof Mwandosya wanasema ni mtu asiye na mzaha, na ukifanya kazi chini yake lazima utamheshimu na kumwogopa kwa namna fulani kwa jinsi alivyo serious na issue za kazi.
Sasa kuna wasiwasi kwamba suala zima la kuugua kwake ghafla linahusiana na mbio za uraisi 2015 na lilikuwa na mkono wa watu! Kama kuna taarifa juu ya hili tafadhali tuelezane zaidi.