Silaa za Ulimwengu wa Roho

Mwl Mwakujonga

JF-Expert Member
Jun 29, 2023
286
582
Ulimwengu wa Roho ndio uliumbwa Kwanza Kabla ya ulimwengu wa Mwili, wakati Mungu anamuumba mwanadamu aliumba Roho Kwanza Kabla ya Mwili

Wakati Mungu anaumba wanyama na miti na Vyote vinavyotambaa aliumba Roho Kwanza Kabla ya Mwili.

Vita siku zote zinafanyika kwenye ulimwengu wa kiroho , na ulimwengu wa Mwili ni uwanja wa matokeo, ziko Silaa kadhaa ambazo shetani anazitumia kuwashinda watu wa Mungu, Silaa hizo ni:-

A. Dhambi
B.Sheria
C. Damu
D. Sadaka

Silaa ya Kwanza

Dhambi

Dhambi ni Silaa kubwa Sana ambayo shetani anatumia kuwa angusha watu wa Mungu

Kwanini dhambi

Dhambi maana yake ni kutenda uhasi, kwenda kinyume na mamlaka Halali

Dhambi Kwa maana ambayo siyo rasmi ni kitendo ambacho unafanya Kwa kujua au kutokujua na kitendo hicho au matokeo ya kitendo hicho ni kukosa msaada wa Mungu aliye hai

Shetani anauwezo wa kumdhuru MTU wa Mungu , Hana huo uwezo ili aweze kupata uhalali wa kumshambulia MTU WA Mungu ni lazima atumie dhambi ili amwondoe mwanadamu katika mikono ya Mungu ili aweze kumtesa

Ndio maana shetani amekuwa anajifunza kila siku mbinu na mikakati ya kuhakikisha kwamba dhambi kuwa nzuri Sana ili mwanadamu amkose Mungu

Unaposoma habari ya pale bustani Yule mwanamke alipolitazama tunda aliliona Lina faaa Lina vutia na linapendeza

Hata Leo shetani anatumia MBINU hiyo hiyo Kile kitu ambacho Mungu alikikataza yeye anakutengenezea mazingira ya kupendeza na kuvutia kiasi kwamba unavutwa mwenyewe Kwa utashi wako

Mwanzo 3:6
[6]Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.

Dhambi ndio uwanja wa mapambano ambao shetani anautumia kuvuruga Maisha ya mwanadamu
 
Yakobo 1:13-14 Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu.

[14]Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.

Dhambi ina matokeo na matokeo ya dhambi ni mauti, neno mauti ni utengano Kati ya uhai na Kifo vinapotengwa matokeo yake ni mauti, Kwa hiyo dhambi ni utengano

Mbingu za shetani kuwashambulia wanadamu Kwa njia ya dhambi , kuna aina ya dhambi shetani ambazo anatumia

A. Uzinzi/Uasherati

Dhambi ni dhambi Tu hakuna dhambi ndogo wala dhambi kubwa , ukweli ni kwamba dhambi zina fanana Ila matokeo yake hayafanani

Nenda mahakamani fatilia au nenda magerezani kaulize kama ni gereza limekamilika wale wafungwa ambao wametenda makosa ya mauaji na wale ambao wamefanya wizi WA kuku kama wanakaa chumba kimoja?

Kwa hiyo kila dhambi Shetani anaitumia Kwa ajili ya kulenga maeneo ambayo yanahusika na Imani

Wataalamu wa afya wanakwambia mwanadamu anapoanza kufariki kitu cha Kwanza kufa ni ubongo na viungo vingine vinafatia , Kwa hiyo kama ubongo ndio unatambulisha kwamba MTU Huyu nizima au kafa ujue kuna Siri katika ubongo

Kwanini uzinzi/uasherati ni Silaa kubwa Sana katika mapambano ya ulimwengu wa kiroho ,kuna sababu kadhaa hapo chini

A. Akili
B. Ufahamu
C.Moyo/Nafsi
D.Mwili

Kitendo kimoja cha uzinzi/uasherati kina kwenda moja Kwa moja katika maeneo hayo na kila eneo Lina maana yake

Akili

Akili ya mwandamu haikk kwenye ubongo Iko kwenye nafsi , Biblia inasema pumzi ya Bwana yanipa akili na hiyo pumzi ya Bwana ilitengeneza nafsi ya mwandamu Kwa Hesabu ya moja jumlisha moja ni mbili , hivyo nafsi hiko ndani ya akili

Kazi ya akili ni kumsaidia Mwanadamu kumjua Mungu Kwa hiyo Kwa njia ya uzinzi shetani ana haribu akili za mwanadamu ili zisiweze kumsaidia kumjua Mungu

Mithali 6:32 Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.
 
Ayubu 32:8 Lakini imo roho ndani ya mwanadamu, Na pumzi za Mwenyezi huwapa akili.

Luka 24:45 Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko.

Kwa hiyo kazi ya uzinzi ni kuharibu akili za mwanadamu zisiweze kumsaidia kumjua Mungu wa kweli Nido maana Leo uzinzi uko juu kila Kona lengo kubwa ni kuhakikisha akili za watu zinaharibiwa wasiweze kumjua Mungu

Hauwezi kumjua Mungu vile unavyotakiwa kumjua kama akili zako zimeharibiwa na Uzinzi , ndio maana Leo watu ni wapishi Sana juu ya neno la Mungu kwa sababu za zinaa kuharibu akili Zao

Waefeso 4:18-19
[18]ambao; akili zao zimetiwa giza, nao wamefarikishwa na uzima wa Mungu, kwa sababu ya ujinga uliomo ndani yao, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao;
:
[19]ambao wakiisha kufa ganzi wanajitia katika mambo ya ufisadi wapate kufanyiza kila namna ya uchafu kwa kutamani. .

Jambo la pili

Moyo wa Mwanadamu , neno linatumika kama ishara ya MTU wa ndani Kwa sababu kama vile kazi ya Moyo kusambaza Damu eneo lote la mwili na kuhakikisha kila kiungi katika mwili wawandamu kinafikiwa ni kama engineer ya mwili WA mwandamu kadharika MTU wandani pia anaitwa Moyo

Mathayo 5:28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.

Kazi ya zinaa ni kushambulia Moyo wa Mwanadamu , ndani ya Moyo WA mwandamu ndimo kuna nafsi ya mwandamu na Roho ya mwandamu

Kwa hiyo shetani akiushinda Moyo wa Mwanadamu Kwa njia ya zinaa maana yake amepata uhalali wa kumiliki Moyo wa Mwanadamu na Mungu anakosa uhalali wa kumiliki Moyo wa mwandamu

Kwa lugha rahisi zinaa inamwondoa Mungu ndani ya mwandamu , Mungu anakaa kwenye Moyo WA Mwanadamu kupitia neno lake Kwa hiyo kama zinaa inakaa ndani ya Moyo WA Mwanadamu Mungu haupati nafasi ndani ya Moyo WA Mwanadamu

Ulishawai kujiuliza kwanini watu ambao Wana maagano na shetani kitu ambacho hawatakiwa kuacha ni zinaa, Kwa sababu kadiri wanavyozini ndivyo wanakuwa mbali na Msaada wa Mungu na shetani anapata uhalali wa kumiliki Maisha Yao

Ndio maana ukiona MTU anafanya zinaa kila siku sio mchana sio usiku ujue Huyo ana agano na kuzimu ni Mali ya shetani

Warumi 10:9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.

Waefeso 3:17 Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo;

Mathayo 15:19 Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano;
 
Ubarikiwe
 
Mwl Mwakujonga:
Jambo la Tatu
Shetani anapotumia zinaa kama Silaa lengo lake ni kuharibu chem chem ya uzima, neno la Mungu linasema uzinzi uko ndani ya Moyo kwa hiyo kupitia Moyo ambao ndio chem chem ya uzima shetani anapata uhalali wa kuondoa uzima maana yeye hakuna uzima

Mithali 4:23 Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo;
Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.

Yohana 1:4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.

Jambo la Nne
Shetani anapotumia zinaa kama Silaa ni kushambulia mawazo ya MTU, mawazo ndiyo yanayoleta ubunifu , Kwa hiyo shetani anaposhambulia mawazo anaharibu mfumo wako wa kufikiri

Ushawai kujiuliza kuwa watu ukikaa nao tangu asubuhi Hadi jioni mazungumzo Yao ni uzinzi , unajiuliza Huyu MTU anawaza nini?

Mawazo yanamsaidia mwanadamu kupata msaada wa Mungu lakini pia mawazo yanamsaidia mwanadamu kutawaliwa na shetani , kuna watu story Zao ni zinaa mwanzo mwisho na ukiendelea kuwasikiliza utajikuta umenaswa

Kwa sababu mawazo ya zinaa Yana ambatana na Roho ya zinaa, Kwa hiyo MTU anayezungumza Mambo ya zinaa anaambukiza roho ya zinaa Kwa watu unajikuta Tu unatamani kujaribu ndio maana Leo zinaa imesambaa kila Kona

Kwa hiyo MTU anapotenda zinaa maana yake anajiungamanisha na Roho ya uzinzi , Kwa hiyo kazi ya roho ni kumiliki na kutawala maana yake anakuwa amejiungamanisha na utawala wa Roho ya uhasherati

Kwanini sio rahisi MTU kuacha zinaa, ulishawai kujiuliza kwamba kuingia kwenye zinaa ni Raisi Ila kutoka sio Raisi ,kwa sababu unakuwa unajiungamanisha na Roho ya uzinzi ambayo inakuwa na umiliki wa mwili wako, nafsi yako na roho wako

1 Wakorintho 6:15-16 Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!

[16]Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.

Ni dhambi ya uzinzi pekee inayouwezo wa kumwondoa MTU wa Mungu ambaye anamahusiano na Mungu na kumwingiza kwenye utawala wa shetani kwakitendo kimoja Tu

Ni dhambi ya uzinzi ambayo inauwezo wa kumzuia MTU hata kama anakwenda kanisani kila jumapili kumjua Mungu, unaweza kuwa unakwenda kanisa kila jumapili na bado ukaishia motoni

Ni dhambi ya uzinzi pekee inayoweza kuharibu Maisha ya Mtumishi wa Mungu yakawa Maisha

Kwanini shetani anatumia dhambi hii, ni Kwa sababu inavutia ,inatamanisha ,inashawishi akili za watu na kuwavutia kidogo kidogo na mwishoe MTU anapotega

Kwa hiyo mtu akikwambia shetani anamapembe anatisha ni kweli lakini hata siku moja hata kuja kwako katika namna hiyo ukimwona hivyo ujue kaja kupigana vita lakini akija kukushawishi anakuja na kile unachotaka Linda Sana Moyo wako hepuka tamaa za kidunia na Mungu atakusaidia
 
Kweli Mia kwa mia
 
wamesusia uzi lkn ujumbe umewkolea..
ubarikiwe sana mtumishi wa Bwana...
 
Back
Top Bottom