Mbeya: Yadaiwa kuna wanaowatumia wenye ulemavu wa akili kutupa taka mitaani kisha kuwalipa Tsh. 500

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Baadhi ya Wakazi wa Bonde la Uyole Jijini Mbeya, wanadaiwa kuwatumia watu wenye ulemavu wa akili 'vichaa' kutupa taka kwenye makazi ya watu na mitaro huku wakiwalipa ujira wa Tsh. 500.

Hatua hiyo inatajwa kukwamisha juhudi za usafi wa mazingira kwenye bonde hilo.

Hayo yameelezwa na Diwani wa Kata ya Uyole, Daniel Njango wakati wa zoezi la kampeni ya usafi wa mazingira lililoandaliwa na Kituo cha Radio ya Kijamii, Highlands FM, wakishirikiana na Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Desemba 2, 2023.

Njango amesema baadhi ya watu wamekuwa wakitumia mbinu ya kuwatumia 'vichaa' kutupa taka ili kuepuka kukamatwa na mamlaka za serikali za mitaa hatua aliyoitaja kuwa ni kikwazo cha usafi wa mazingira kwenye eneo hilo.
mb2.JPG

mb1.JPG

"Lakini huwa tunawakamata na kuwataka watupeleke sehemu waliyotumwa, baada ya kuwabaini wanaowabebesha mizigo huwa tunawatoza faini kulingana na Sheria zetu za halmashauri," alisema.
mb.JPG

Katika hatua nyingine emesema Kampeni hiyo ya usafi itakuwa chachu ya kuhamasisha zoezi hilo kufanyika mara Kwa mara huku akieleza kuwa imekuja Kwa wakati Kwa kuwa kipindi hiki ni msimu wa mvua.

Naye, Mwenyekiti wa kamati ya usafi wa mazingira ambayo imepewa Jina la Mvua sio Janga, safisha mazingira, Lameck Charles amesema zoezi hilo litakuwa ni endelevu.
 
Halafu mtu aje hapa alalamike kwanini hatuendelei. Hivi vichwa vya kiafrika hata ufanye vitabaki hvhv..........havina akili wala uzalendo
 
Jero ni pesa nzuri sana kwa kichaa.........ataenda kwa maza ntilie kutaka ugali mkubwa na samaki(kambale) watatu pamoja na pepsi baridiii
 
Back
Top Bottom