Mbeya: Mwandishi wa Habari mbaroni kwa kujifanya afisa Usalama wa Taifa

JOHNGERVAS

JF-Expert Member
Mar 22, 2016
499
618
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Songwe, Augustino Senga amesema wanamshikilia mwandishi wa habari (41) (ambaye jina lake limehifadhiwa) kwa kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, akijitambulisha kuwa ofisa usalama wa Taifa.

Kamanda Senga ameyasema hayo leo Jumapili Mei 05, 2024 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa maelezo ya Kamanda Senga, mtuhumiwa huyo alikamatwa wilayani Momba mkoani humo kwa kujipatia fedha (kiusalama hajazitaja) akidai atawasaidia kushinda uchaguzi wa Serikali za mtaa kwa wananchi wenye nia ya kugombea.

"Alikuwa anatumia njia ya kuwakusanya baadhi ya wananchi akiwadanganya yeye ni ofisa usalama wa taifa na atawasaidia kushinda uchaguzi wa Serikali za mitaa, tumemkamata baada ya wasamaria wema kutoa taarifa kwenye vyombo vya usalama,"amesema kamanda Senga.

Kamanda Senga amesema kwa mtuhumiwa huyo alishafanya utapeli katika mikoa ya Dodoma, Njombe, Mbeya na Iringa kabla hajakamatwa Songwe ambapo pia alishafanya utapeli katika wilaya za Ileje na Momba.
 
Kwani nawajua undercover wote?
 
Hilo ni kosa la kutoa rushwa pia.

Wangelizolewa na hao watia nia katika uchaguzi wa Serikali za mtaa waliotoa hizo hela wakaswendemwa ndani.

Huyo tapeli abakie na kesi yake ya msingi, lakini na hili la rushwa asichomoke.
 
Kabisa maana hapo hakuna kesi na hata fungwa akipata wakili wa kumtetea
Ili afungwe kwa kujifanya usalama wa Taifa itawataka idara ikathibitishe kitendo ambacho huwa hawafanyi
hapo labda afungwe kwa kesi ya utapeli
Kesi hizi ni ngumu sana yani
 
Sisi huku wanaogopewa mpaka vichaa wakidhaniwa ni usalama wa taifa, wengine ni dada poa wanaogopeka sana. Kuna kichaa mmoja yeye haachi kwenda majalalani, mara paap linatokea gari likipita karibu na jalala na mtu anatupa foil ina chakula cha moto na chupa ya maji ya kunywa na gari hilo linatokomea kusikojulikana na kumuacha kichaa huyo akijinoma msosi safi hapo jalalani. Who knows kama ni usalama wa taifa? Ni assumption tu
 
hahah
 
Hata sisi wengine jinsi tulivyo tunaogopewa tukidhaniwa ni usalama wa taifa. Vijiwe vya kahawa, bodaboda, na vijiwe vya kuuzia magazeti tukifika tu tunanyenyekewa kwa heshima zote. Maofisini wafanyakazi na mabosi zetu wanatuhofia wakidhani tuko kazini kuwachunguza nyendo zao ovu na za kizembe mpaka huwa tunalazimika kuwatoa wasiwasi wawe na amani tu sisi si watu wa usalama wa taifa.
 
Back
Top Bottom