MBATIA UMESEMA KWELI kuhusu CDM

Kweli ukipenda, chongo utasema kengeza.

Mbatia kashusha Mianzi, wengine wanaona kawashushia Nondo.

Sasa Maisha magumu yanahusishwaje na Chadema?

Mwambie katika nondo zake basi aongeze kuwa Ukame na kukosa umeme, kumeletwa na Dr. Slaa.

Mwambie hata wanae wakifeli au akikosana na mkewe (hivi ana mke) basi ajue ni Chadema.

Udini pia umeletwa na Chadema vilevile.
 
ni pumba kweli kweli kama hata habari leo na uhuru na jambo leo hawakuandika, amechokwa sana ndio maana anaona dili kufungua kesi za visingizio baada ya kupigwa kisigino na Mtotot mdogo H.M
 
Mbatia ni mufilisi kiasa (I guess in all wise)! Kama angekuwa na agenda ya maana angepaswa kuzungumzia habari za chama chake na si vyama vingine. Ni mwenyekiti wa kwanza wa chama cha siasa ni recent TZ history aliyegombea ubunge (sio uraisi) na kushindwa je huyo ni kiongozi wa aina gani? No wonder anawashambulia CDM.
Hapo kwenye red, namshauri ajiandae 2015 agombee udiwani kata ya mchafukoge
 
yani hadi Uhuru wamechunia hiyo?
basi amekwisha,niliona kwenye Al-nuru kawekwa front page wapongeze

Hahahaaaa! Hata huyo mwana uhuru hajafurahishwa na chombo chake. Mbatia ni nani? Hana mvuto kwenye vyombo vya habari hadi vya CCM. Labda akiandikwa kwenye magazeti ya udaku, ndio watauza.
 
kama amesema pumba pia zirushwe hewani?nazani hajaongea lolote la maana yeye na hao wenzake ndo maana haijarushwa kwenye kituo chochote
Pumba?? Unataka kutuambia CDM wao huongea busara? Ona mtu kama Tundu Lisu anavyochemka hadharani bungeni, walikwenda Mwanza jamaa hawakujua wanaongea nini. Topiki ni JK tu, hawana jipya. Mbatia, Lipumba wako makiini zaidi linapokuja suala la kushuka nondo. CDM wao wanategemea kuwasakizia watu waandamane tu.
 
Vyombo vya habari vya bongo ni vibovu sana. Pale manzese bakharesa palifanyika mkutano wa CUF na mionghoni mwa waalikwa ni mwenyekiti wa NCCR bwana Mbatia. Jamaa alishuka nondo sana na kuibeza chadema kuwa sio chama makini na hakistahili kupewa nchi. Pia aligusia udini uliyofanyika wakati wa uchaguzi na kutahadharisha kuhusu amani ya nchi.
Mbona vyombo vya habari havikutoa hii habari? Bila shaka vyombo vyetu sio professional bali ni politically manipularted and oriented. Sina imani navyo.

Mkuu Heshima

Ingekuwa vyema na wewe ukaweka in Summary alichoongea Mbatia, Lini Aliongea na Alisema nini hasa ambacho wewe unaona ni kwa Mustakabali wa Taifa. Vinginevyo utaonekana unaendekeza majungu tu
 
Vyombo vya habari vya bongo ni vibovu sana. Pale manzese bakharesa palifanyika mkutano wa CUF na mionghoni mwa waalikwa ni mwenyekiti wa NCCR bwana Mbatia. Jamaa alishuka nondo sana na kuibeza chadema kuwa sio chama makini na hakistahili kupewa nchi. Pia aligusia udini uliyofanyika wakati wa uchaguzi na kutahadharisha kuhusu amani ya nchi.
Mbona vyombo vya habari havikutoa hii habari? Bila shaka vyombo vyetu sio professional bali ni politically manipularted and oriented. Sina imani navyo.

Njaa inamsumbua huyu! Ni chama kipi kina viti vingi Bungeni? Ni chama kipi kinakitikisa chama cha majambazi/mafisadi? Waandishi kwa nini wapoteze muda wao kuandika longolongo za Mbatia wakati wanajua anatumiwa na CCM? Angekuwa kweli ana mapenzi na Tanzania basi kamwe asingeishambulia CHADEMA bali CCM. Hana jipya huyu kapitwa na wakati.
 
Mbatia hana lolote la kutueleza watu wenye akili. Wengine tumesoma naye tunamjua vizuri kabisa. Hawezi kuongoza hata nyumba kumi. To hell with him.
 
Pumba?? Unataka kutuambia CDM wao huongea busara? Ona mtu kama Tundu Lisu anavyochemka hadharani bungeni, walikwenda Mwanza jamaa hawakujua wanaongea nini. Topiki ni JK tu, hawana jipya. Mbatia, Lipumba wako makiini zaidi linapokuja suala la kushuka nondo. CDM wao wanategemea kuwasakizia watu waandamane tu.

Mkuu CUF, NCCR and the co should Evaluate them selves kama kweli wanataka kuendelea kuwa katika Ramani ya Siasa za Tanzania, Siyo Mbaya kujifunza Kwa CHADEMA as nini wanafanya mpaka wanaweza kupata Mwitikio Mkubwa kwa Wananchi. Kama Unakumbuka CUF waliitisha Maandamano Dar Es Salaam, lakini watu wachache sana Walijitokeza sasa Mkiendelea kulalamikia CDM mtaachwa na Wakati
 
CDM ni mwiba! Utamchoma kila anayeiombea mabaya! Hivi Mbatia ameshakuwa rafiki wa CUF? Mmeshasahau kura za maruhani pemba? Kweli adui wa adui yako ni rafiki yako! Mbatia is consistently inconsistent and lacks cohesion in his talks-a calamity for a politician!
 
Yap, sio ushabiki ila kwa kumzungumzia mbatia ni mwanasiasa mwenye hoja(nilimsikiliza kwenye mbio za kuwania ubungo Kawe) lakini asiye na mikakati hivyo kumfanya asijue namna ya kuzisimamia hoja zake kwa mfano, huwa anakisemea mbovu sana chama twawala CCM tena kwa hoja zenye mashiko ila tatizo ni kwamba bado kama anamapenzi fulani hivi na CCM na hii inaonekana jinsi anavyoipondea CDM hivyo haiwezekani uipinge CCM alafu unawakashifu CDM kwa wanayoyatoa kuwakosoa CCM!
Hivyo huyu jamaa atakuwa na asili ya UNAFIKi
 
Ila kwa kweli Nafurahishwa sana na Approach ya CUF na NCCR! Ukipingana na CDM unapingana na Nguvu ya Uma na Matokeo yake ni Kupotea katika Ulingo wa Siasa
 
Katiba ya nchi hii ni kwamba hakuna dini hivyo mbatia na wa2 kama yeye wasijaribu kupata umaarufu kupitia cdm.
Mbatia hana lolote kaa kimya pepoooooo zzzzzzzzzzz
 
Mmmmh!.....
Inawezekana CDM siyo Makini lakini NCCR-Mageuzi wanaweza kuwa chama Maiti mahututi ICU. Mbatia ni msemaji mzuri lakini sometimes anapoteza hoja nyingi kutaka kufurahisha hadhira zaidi kuliko kusema ukweli. Angekuwa makini angejua kwamba Chadema haina udini ila CCM walitumia propaganda hiyo kuwapunguza nguvu baada ya kuona wanaungwa mkono kwa kasi kubwa na watanzania wengi. Hata CUF ilipokuwa inakua kwa kasi lugha ilikuwa hiyo hiyo, UDINI!
 
hao ndio miongoni mwa waliofilisika kisiasa, maana Mrema nae alikuwa na kituko kikubwa Chama chake kilikuwa na mgombea lakini yeye alikuwa anampigia kampeni JK

CUF wanajitahidi kutengeneza kambi ya upinzani ya kupingana na Wapinzani wa CCM, CUF wangekuwa makini na wenye nia nzuri ya kuikomboa hii nchi kutoka kwa mafisadi, wasingekubali kumwalika mtu kama MBatia ambaye misimamo yake kwa sasa inajulilkana ni kuupinga upinzani wa Chadema,
 
alishindwa na CDM jimbo la kawe tena na mwanamke Halima Mdee, sasa unadhani atasifia nini? si kila jambo ni habari. kumbuka Mbwa akimuuma mtu si habari ila mtu akimuuma mtu.

AMEFULIA NA MWENZAKE DAVID KAFULIA AU KATUNI
 
Vp kuhusu magazeti ya Rostam Aziz (Mtanzania, Rai), ya CCM (Uhuru), na ya Serikali ya CCM (Daily News, Habari Leo).
Je nayo hayakuona 'umuhimu' wa habari yake huyo Mbatia?
Kama ndivyo basi amekwisha. Huyo ndiyo Mwenyekiti wa taifa wa Chama aliyeshindwa vibaya Ubunge.
 
CDM wasipokuwa makini machoni mwa Mbatia. Inawezekana NCCR mageuzi wakawa mahututi, ICU au chama mfu kabisa. Udini gani uliopo Chadema? Ukiondoa tapatapa ya timu ya kampeni ya JK baada ya kuhisi maji ya shingo na kukimbilia kuwatisha wananchi ili kupunguza kura za chama hicho udini gani aliouona yeye?
 
Hao CUF na NCCR Mageuzi kwa wakati huu wana kitu kimoja wanachofanana (one thing in common), nacho ni kuwa hawapendezwi na kukubalika kwa Chadema kama chama kinachozidi kukubalika na kinachoweza kushika dola.
Kwa hili wanafanana pia na CCM, ndiyo naana wanaelewana, na ni kwa hili moja tu.

CUF, kutokana na kuhofia nguvu za Chadema ambayo imeipiku na kuwa chama kikuu cha upinzani, wamesahau, very conveniently kuwa mwaka 2005 ni NCCR-Magezi chini ya huyo rafiki yao wa sasa Mbatia ndiyo iliyoweka pingamizi kwa wagombea watano wa CUF huko Pemba, hivyo kusababisha wakaenguliwa na hivyo wagombea wa CCM wakashinda kiulaini ingawa walipata kura chache. Kura nyingi zihesabiwa kuwa zimeharibika, zikaitwa 'Kura za maruhani'.

Je Mbatia alitumwa na CCM? Eti leo CUF na NCCR wamekuwa washkaji?

Kwa kifupi, CUF, NCCR, na CCM wana one thing in common, that's their 'fear' of Chadema, which is becoming more and more acceptable to the people.
 
Back
Top Bottom