Mbaroni kwa kumuua mpenzi wa Mama yake

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,116
Jeshi la Polisi Mkoani Arusha linamshikilia Kijana anayefahamika kwa jina la Rasuli Abdalah kwa tuhuma za kumuua Mwanaume anayefahamika kwa jina la Aniskari Maembe baaada ya kumkuta akiwa amelala na Mama yake mzazi.

Noris Kivuyo ambaye ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Makao mapya ambako tukio limetokea amesema Mtoto huyo alimkuta Mama nyumbani kwa Mwanaume huyo na kumtaka atoke nje na alipogoma alimtoa kwa hasira akiwa uchi na baadaye akanza kumshambulia Mwanaume kwa marungu hadi kufariki.

“Nilipouliza nikaambiwa ni Mtoto amekuja kumtoa Mama yake kwenye chumba ndani kwa Mwanaume, Mama alivyogoma alimtoa akiwa uchi na Mama alipiga kelele sana, nitoe ushauri ukiona Baba yako anatoka na taulo kwenye chumba cha Mama yako huyo ni Baba yako”

Mwanamke huyo alishaachana na Mumewe na akawa kwenye mahusiano na Mwanaume aliyeuawa, bado hajajulikana chanzo cha Mtoto kuchukua maamuzi hayo.
 
Kiasili sisi watoto wa kiume huwa hatupendi kuwaona mama zetu wakiwa na wanaume wengine zaidi ya Baba zetu, kibaya zaidi hawa mama zetu knachotuuzi zaidi kumwona mama yako akitembea na kijana wa umri wako inauma kweli kweli, wamama mnapoamua kufanya ujinga wenu fanyieni pengine mikoa mingine ujinga wenu.
 
Sasa akafie jela ili maza aendelee kujiachia kwa raha. Vitu vingine ni kuaachana navyo tu. Unakaa mbali na mama.
Hata watoto wa kiume hutembea na wanawake wakubwa size ya bibi zao lakini mama zao hawawadhuru zaidi ya kuongea tu.
 
Hata watoto wa kiume hutembea na wanawake wakubwa size ya bibi zao lakini mama zao hawawadhuru zaidi ya kuongea tu.
Maumivu ya Mtoto wa kiume kwa Mama mdangaji ni zaidi ya unavyofikiri, nawaonea huruma wadangaji wenye watoto wa kiume siku akigundua kua huyu Mama anadanga na Baba yangu yupo Vita inaanzia hapo utaburuzwa na mtoto wako uliemzaa maana anaona unamuaibisha

404: Page Not Found
 
Sidhani kama hii issue ina suala la udangaji. Kama walishaachana na baba yako unakuwaje na chuki hadi kufikia kuua?
Ni jambo la kusononesha ndio lakini hadi ufikie suala la kuua inafikirisha. Wivu gani huo wa kipumbavu...ukute alikuwa analala na mama yake.
 
Back
Top Bottom