MBA evening programme UDSM

Haya kaka. Mimi nasoma pale tena MBA Evening na ninamalizia mwaka wa kwanza. Leo hii saa 11 jioni tuna mtihani wa Business Research Methodology.

Evening MBA kila mwaka inaanza katikati ya mwezi July, mfano sisi tulianza 15 July 2008. Ziko Semester/Mihula 7 na imegawanywa mihula 6 kwaajili ya darasani na 1 kwaajili ya Dissertation. Kila mmula una masomo 3 na mwisho wa muhula tunayafanyia mtihani, na baada ya mtihani tunapumzika wiki 1.5-2, mara tu baada ya likizo tunaanza mhula mwingine. Kwa hiyo 6*3=18, course/masomo 18 baada ya muhula wa sita. Muhula wa saba ni research paper.

Vipindi ni saa 11 jioni hadi saa mbili usiku kwa siku tatu kwa wiki. Muundo kunakua na assignment/presentation 1, term paper 1 na test 1 (Course work ni 50%) na mtihani wa mwisho ni 50%. Pass mark ni 50% or above. Suplimentary ukipata <50% ya jumla ya marks (Course work+Final Exams)

Unapoingia unatakiwa kufanya usajili na kila muhula mmoja fee ni TShs 900,000.Kwa hiyo unaweza kulipa kwa muhula. Ila wapo wengi walilipa muhula wa kwanza na hawajalipia mihula mingine na bado wanasoma kwa kwenda mbele. Jumla ya fee ili utunukiwe MBA ni 7*900,000=6,300,000.

Course yote huchukua miaka miwili kuimaliza ila dissertation itategemea ushapu wako, wapo wengine huchukua hata zaidi ya mwaka kuandika research paper.

Ni kweli vyuo viko vingi ila mtu unaangalia bei, ubora, credibility, value n.k


mkuu nashukuru saana kwa hii information japo ni yazamani but imenipa mwanga wakujua pakuanzia na nimekua admited n by 22 ya mwez huu ndo twaanza classes!!
 
Back
Top Bottom