kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 268
Kanisa la Westboro Baptist Church la Kansas City, Marekani limeandaa maandamano kupinga mazishi ya msanii maarufu nyota wa kundi la Jackass, Ryan Dunn ambaye alifariki wiki hii kwa ajali ya gari, kanisa hilo linasema kuwa Ryan Dunn alikuwa ni mtenda dhambi na baada ya kufariki hivi sasa yuko motonKanisa la Westboro Baptist Church lenye makazi yake Kansas City nchini Marekani linajulikana sana kwa maandamano yake ya wazi ya kupinga mashoga duniani.
Kanisa hilo lilitoa taarifa kwa vyombo vya habari likisema kuwa Ryan Dunn yuko motoni.
Ryan Dunn alikuwa msanii maarufu wa kundi la Jackass la Marekani ambalo limekuwa likifanya shoo za michezo ya hatari na vituko mbali mbali ambapo shoo zao huonyeshwa na televisheni maarufu duniani ya MTV.
Kanisa hilo lilisema kuwa kifo cha Dunn kwa ajali ya gari ni matokeo ya vitendo vyake viovu ambapo mara nyingi huonekana akifanya vitendo vya kipuuzi na wakati mwingine akifanya vitendo vinavyohusisha ngono.
"Kwa rehema za Mungu, maisha yake duniani yamekatishwa kwasababu alikuwa akifanya maovu na akiwafundisha watu kufanya maovu mbele ya mungu", ilisema taarifa ya kanisa hilo.
Dunn alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 34 baada ya kupata ajali wakati akiliendesha gari lake aina ya Porsche kwa spidi ya kilomita 225 kwa saa.
Wakati huo huo, Dunn alikuwa amelewa na damu yake ilipopimwa ilionyesha kuwa na kiwango cha alcohol mara dufu ya kiwango kinachokubalika kisheria.
Familia ya Dunn iko kwenye maandalizi ya kufanya mazishi makubwa kwaajili ya Dunn na polisi wameishapewa taarifa kuhusiana na maandamano ya kanisa la Westboro Baptist Church.i.