Mazingaombwe (Jugglery) ni Sayansi au Uchawi?

Salaam, Kwa muda mrefu nimekuwa nikifuatilia mambo ya mazingaombwe toka kipindi nasoma shule ya msingi maana walikuwa wanakuja shuleni hawa watu wa mazingaombwe mpaka nikashuhudia makaratasi yanabadilishwa kuwa fedha. Akina mshana, mzizi mkavu na wengine wenye uelewa wa mambo haya mchango wenu unahitajika tafadhari
 
kuna vitu huwa ni ujanja na wepesi wa matendo, lakin kuna criss angel huwa sielewi ni nguvu ya ki magic au ni ujanja ujanja, alikuta watu wanaogelea akawaambia 7 kila mmoja achukue karatasi na markpen afikirie herufi yoyote moja na aindike, akawaambia wajipange kwa mstari wakaonyesha zile karatasi, wote walikamilisha neno BELIEVE kwa zile herufi. wewe acha tu
 
kuna vitu huwa ni ujanja na wepesi wa matendo, lakin kuna criss angel huwa sielewi ni nguvu ya ki magic au ni ujanja ujanja, alikuta watu wanaogelea akawaambia 7 kila mmoja achukue karatasi na markpen afikirie herufi yoyote moja na aindike, akawaambia wajipange kwa mstari wakaonyesha zile karatasi, wote walikamilisha neno BELIEVE kwa zile herufi. wewe acha tu
 
Daaa .....nimekula sana peremende zilizotengenezwa kwenye mazingaombwe....ila sijui lengo la serikali kupromote haya mambo ilikuwa nn
 
Kuna siku nilienda kufanya mazingaombwe kule Sumbawanga. Nilikuwa na uwezo wa kumgeuza binadamu kuwa panya kisha nikamrudisha tena na kuwa binadamu.
Basi nikaenda sokoni nikawakusanya watu, nikamgeuza jamaa kuwa panya.
Kulikuwa na mama mmoja pembeni akajigeuza na kuwa paka, kisha akammeza yule panya, na baada ya hapo akarudi kwenye umbo lake la ubinadamu.
Nilijuta kuzaliwa, sitaki kukuelezea kilichotokea baada ya hapo.
Hahahaha...!
 
Enzi zile nasoma shule ya msingi kulikuwa na vijana waliokuwa wakija shule kwa ajili ya mazingombwe. Walikuwa wakifika shuleni mara kwa mara kwa ajili ya maonyesho hayo.

Walikuwa wakipewa kibali na mwl mkuu/mwl wa michezo pamoja na kupewa darasa la kufanyia mazingambwe yao kama ukumbi. Pia kulikuwa kiingilio ili kuweza kuingia ukumbini (darasani) kwa ajili ya kuangalia mazingaombwe hayo.

Ndani ya ukumbi, wanaofanyia mazingaombwe walikuwa wakifanya vituko mbalimbali ambavyo baada ya kuvikumbuka nikaamua kuleta uzi huu kwenye hili jamvi la chitchat ili tukumbushane. Nakumbuka:

  • Kuna siku walimuita mvulana mmoja wakampasua tumbo hadi utumbo ukawa unaonekana kwa nje, baadae wakaongea maneno fulani yule mtu akazinduka na hakuwa na kovu lolote lile
  • Siku nyingine wilimuita mtoto aliyekuwa mdogo kuliko wote darasani wakamuweka ndani ya gunia lililokuwa tupu mara baada ya dakika kadhaa... pipi na biskut zikajaa kwenye lile gunia...
Naombeni tukumbushane vituko vyilivyokuwa vikifanyika kwenye mazingaombwe

Vilevile nimejiuliza maswali yafuatayo:
  1. Nini kilikuwa kinasababisha tuone mtu aliyepasuliwa tumbo hana hata kovu eneo lililopasuliwa?
  2. Mazingaombwe bado yanafanyika mashuleni mpaka sasa?
  3. Je Wizara ya Elimu ilikuwa inakuridhia mazingaombwe kufanyika mashuleni?
Mtazamo wako ukoje katika haya?
UKATUBU DHAMBI KESHO MZINZI WEWE AYA FANYA UJIANDAE KESHO JUMAPILI
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom