Mawazo haya ya mende

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,916
Mende asili yake ni uchafu japo yeye mwenyewe hupenda sana kujiweka msafi hata kama yuko kwenye mazingira machafu.. Yaani anajijali yeye tu mwili wake na si sehemu nyingine yoyote! Hata kitanda chake

Tuna ndugu yetu humu anajiita mendemsafi .. Pengine hili jina lina connection na hayo maisha ya mende
Kuna binadamu pia huitwa mende kutokana na tabia zao fulani fulani .. Ni wasafi wa mwili lakini kiroho ni wachafu kabisa!
Mende anapenda usiri na kujificha sehemu asiyoonekana kwa wepesi.. Mende hutoka mafichoni kukiwa na utulivu hapo huamini wanadamu wamelala!
Pamoja na usafi wake wote lakini mende huishi sehemu chafu.. Sehemu safi iliyopangwa vizuri mende hakai

Penye utulivu mende hujitokeza toka mafichoni na kupanga mipango ya kulivamia kabati lenye vyakula, vyombo na vitu vingine! Pale utaona kabisa anavyopiga hesabu namna atakavyolisukuma kabati lianguke vyakula vimwagike ale asibe asaze.. Ishu ya uharibifu wa vyombo na kabati hilo halimhusu kabisa

Hizi ndio akili za watendaji wetu katika kaya yetu tukuka! Mawazo yao hayatofautiani kabisa na mawazo ya mende! Pangu pakavu tia mchuzi! Vipi pa wengine!? Wanachowazidi mende ni matendo, mende huishia kuwaza wao hufanya na matendo kabisa

Ukiwaona kwenye suit na makeups utasema watu si ndio hawa sasa...ukija kwenye matendo yao.. Ni afadhali mende aishiye chooni kuliko wao.. Wote wana sera moja tuu CHUKUA CHAKO MAPEMA kwakuwa kila mbuzi mee hula kwa urefu wa kamba yake!

Jamani kaya inaliwa
Jamani kaya inatafunwa
Jamani kaya inafujwa
Watu wanapindua makabati ili wapate kitu kimoja kinachowafaa bila kujali uharibifu wanaosababisha kwa ulafi na ubinafsi wao.. Kwenye hii kaya hakuna palipopona.. Makabati yamepinduliwa kila kona

Kwenye yote haya kiti kimekaa kimya tu kinaangalia mamende yanavyopindua makabati na kuharibu vitu.. Mpaka inafika mahali unajiuliza kwani hiki ni kiti ama ni jamvi la wageni?

Inafikirisha sana!
f8ba28c8a616538ee418adb32b871485.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inafikirisha sana!View attachment 2751876

Sent using Jamii Forums mobile app
Inafikirisha kwa kweli Mkuu.
mshana uishi milele Mkuu
 
Back
Top Bottom