Mawaziri Watakaolalamikia OC Ndogo!, Waache Kazi!. Ni Kauli ya Kujenga Nidhamu au Udikiteta Tuu?!.

Pasco huyu ngosha amedhamiria kurudisha heshima ya nchi ila sheria zitambana Kama Ni mjanja abadilishe sheria hizo kwanza maana katika kesi zote zinazohusu jamhuri asilimia kubwa wamebwagwa Na kulipa faini kubwa , rejea meli ya samaki wa maghufuli 2008/09.
 
Sijasoma mpaka mwisho makala ya Pasco, ila kidogo nilichosoma nimeona kama kinalenga kumshutumu , kwa namna moja ama nyingine, mh jpm kwamba ni dikteta mbaya

Pass huyu huyu, amekuwa siku zote akisinzia magufuli kwamba ni dikteta mzuri, benevolent dikteta, tena kwa msisitizo

Ni kipi kilichomsibu mpaka kutengua kauli yake mapema namna hii, je ni Hilo la OC peke yake, au ana Lake chini ya kapeti
 
nchi nyingi zilizoendelea zilianza na mfumo wa kidikteta kama hivi.

Wasomi wa utawala wanakwambia dictotorship system inaruhusiwa kutumika endapo demokrasia inazuia maamuzi ya haraka na kupoteza muda.

Kama ni kuwachekea jk aliwachekea full stop hii ni awamu ya tano. Acha tuisome #
 
Wanabodi,

Nimewahi kuzungumzia baadhi ya kauli za rais wetu Mhe. Dr. John Pombe Magufuli kuwa ni kauli za vitisho, kibabe na kidikiteta, ambapo kauli ya leo ni hii ya kuwatisha baadhi ya mawaziri na makatibu watakaosika kulalamikia fedha za ndogo za OC (other charges) zinazopelekwa kwenye wizara zao ni ndogo na hazitoshi!, amewaambia wale wotewanaoona fedha wanazopewa ni ndogo na haziwatoshi, waache kazi!, amesema kuna watu wanalalamika!, anasema ametuma 'watu' wawarekodi walalamika hao, akipata tuu ushahidi, kuwa ni kweli wanalalamika, then atawatimua kazi!.

Hili limekaaje?!. Hii sio kauli ya vitisho, kuwa watendaji hawa wakuu?!, yaani kiasi chochote watakachopewa na serikali, no matter ni kidogo kiasi gani, hawaruhusiwi kucomment chochote bali wapokee na kunyamaza kimya!.

Huku si ni kuwafunga midomo mawaziri na makatibu wakuu wao?!, kitendo cha rais kesema amewatumia 'watu' wawarekodi, ni uthibitishoa usiotia shaka kuwa freedom of "expression is at crossroad!". Hii inaitwa suppressing opinion za mawaziri, makatibu wakuu na watendaji wakuu, ambazo ndizo hatua za awali za viongozi wote madikiteta duniani, hutoa kauli za kuwafanya waogopwe!. Ukiona mwenzako ananyolewa, wewe anza kutia maji tia maji, stage ya pili haiwezi kuwa ni kwenye media?!.

Tanzania yetu hii kusema ukweli madudu yalizidi, kiasi kwamba tukafika mahali nchi yetu ilihitaji kiongozi mwenye traits za udikiteta ili mambo yaende!. Mungu kasikia kilio cha Watanzania, katupatia rais Dr. John Pombe Magufuli, ambaye ni benevolent dictator, Watanzania tupewe nini tena?!.

Pasco
Hujielewi wewe ungekua China ungenyongwa!!
 
Tufanye kazi na kuwajibika hata kama umejiajiri fuata maadili na katiba ya nchi.Watalamu wa Saikolojia na Philosofia na hata walimu kama wamemwona Raisi alivyokuwa anaongea wataelewa kwamba anafanya Kile kinachopaswa kufanywa na kinatoka moyoni na ndivyo inavyotakiwa.
Uwajibikaji uanzia ngazi ya familia na kusambaa mpaka kwenye jamii.Ni kama vidole vinavyotegemeana na ndivyo maendeleo yanapokuja pale familia na jamii inapowajibika.Hivyo basi ukiwajibika ujue unachangia kusukuma maendeleo yako na ya jamii unayoishi.Mfano ukilima shamba utapata mavuno yako na ziada kwa jamii hapo ndipo ustarabu unapo anzia,ukiacha jamii nyingi za wazungu kuendelea jamii za mataifa ya Asia waliamua kujituma sana na sasa jamii nyingi za Asia zipo kwenye kipato cha kati.Hivyo ni wakati wa kila mmoja kuwajibika kama kweli tunataka tufanikiwe na umaskini uwe historia.
 
Sijasoma mpaka mwisho makala ya Pasco, ila kidogo nilichosoma nimeona kama kinalenga kumshutumu , kwa namna moja ama nyingine, mh jpm kwamba ni dikteta mbaya

Pass huyu huyu, amekuwa siku zote akisinzia magufuli kwamba ni dikteta mzuri, benevolent dikteta, tena kwa msisitizo

Ni kipi kilichomsibu mpaka kutengua kauli yake mapema namna hii, je ni Hilo la OC peke yake, au ana Lake chini ya kapeti
pasco alifikiri atapewa nafasi ya greyson msigwa pale ikulu sababu ni msukuma mwenzake
 
Taifa la watu milioni 50 leo linaendeshwa na akili za mtu mmoja
na wasio ridhika hawatakiwi hata kusema tu

Ndo maana wenzetu nchi zilizoendelea walishaliona hili
hatari za kuendeshwa na mtu mmoja

wakaweka mfumo wa kuhakikisha mawazo ya mtu mmoja peke yake hayaendeshi nchi
Magu ameshashindwa kama wenzake waliomtangulia walivyoshindwa.

Kiongozi ukishakuwa na madaraka mkubwa sana inafika mahali nchi inasisima
Kwa sababu kila kitu kutakuwa kinamsubiri mtu mmoja kufanya maamuzi.
 
Sijasoma mpaka mwisho makala ya Pasco, ila kidogo nilichosoma nimeona kama kinalenga kumshutumu , kwa namna moja ama nyingine, mh jpm kwamba ni dikteta mbaya

Pass huyu huyu, amekuwa siku zote akisinzia magufuli kwamba ni dikteta mzuri, benevolent dikteta, tena kwa msisitizo

Ni kipi kilichomsibu mpaka kutengua kauli yake mapema namna hii, je ni Hilo la OC peke yake, au ana Lake chini ya kapeti

soma paragraph ya mwisho utamuelewa Pasco
 
Ukiisoma makala ya Pasco kwa haraka huwezi kupata ujumbe kusudiwa.Nice article!
tatzo kubwa la pasco anataka kutufanya wote tumesoma art, na hakuna mchumi au mwanamahesabu,

nimkumbushe pasco, kulalamika si jambo baya ubaya ni aina ya malalamiko, mfn kama unamtoto anasoma halafu kila siku analalamika pesa unayompa haimtoshi, na haoneshi haimtoshi kivip... hyo anapaswa kunyimwa hata hyo unayo mpatia, hvyo mtt mzr ni yule anaelalamika kwa hoja, kwamba hii pesa haitoshi kwa sabab ya hiv na vile..

sasa hao wanaopewa pesa wasipoonesha upungufu, wakabaki kulalamika wanahaja gan ya kubaki kuwa watendaji?

jpm yupo sahihi, na amesema jambo sahihi kwa wakati sahihi.... na wasomi wamemuelewa, ila wale wenzangu na mm wazee wa kukurupuka kama JAFYA, wametoka 0...
 
Magu ameshashindwa kama wenzake waliomtangulia walivyoshindwa.

Kiongozi ukishakuwa na madaraka mkubwa sana inafika mahali nchi inasisima
Kwa sababu kila kitu kutakuwa kinamsubiri mtu mmoja kufanya maamuzi.

Angekuwa mjanja angejipunguzia madaraka haraka
badala ya kugombana na wakuu wa mikoa unaweka magavana wananchi wanawachagua na kuwatimua wenyewe
 
Angekuwa mjanja angejipunguzia madaraka haraka
badala ya kugombana na wakuu wa mikoa unaweka magavana wananchi wanawachagua na kuwatimua wenyewe
CCM hawadhubuti kwani hayo madaraka ya Rais ndo yanawafanya wawepo kwenye ulingo wa siasa mpaka leo, na magufuli an alijua vizuri maana imemsaidia kuingia madarakani.
 
Back
Top Bottom