Mawaziri bado waishi mahotelini, Hii vipi wanajamii?

HISIA KALI

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
694
108
Wale wa zamani nao wang`ang`ania makazi yao

Serikali bado inaendelea kupoteza mamilioni ya fedha kwa kuwalipia Mawaziri na Naibu Mawaziri kuishi hotelini baada ya kukosa nyumba za serikali.

Uchunguzi wa NIPASHE JUMAPILI umebaini kuwa bado mawaziri wanaendelea kuishi mahotelini kwa madai kwamba nyumba zao zinafanyiwa ukarabati.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba baadhi ya viongozi hao wamepangishiwa nyumba za gharama (apartments), kwenye hoteli kubwa jijini Dar es Salaam.

Baadhi yao wanaishi Ubungo Plaza ambako gharama ni dola za Marekani 105 kwa siku na Protea ambako kwa siku ni kati ya dola za Marekani 155 na 180.

Uchunguzi zaidi unaonyesha kwamba chakula katika hoteli ya Protea ni dola 20 wakati Ubungo Plaza, gharama ya pango inajumuisha mlo mmoja.

Hata hivyo, sababu za kukosa nyumba haziwekwi bayana wakati takwimu zinaonyesha kwamba katika baraza la Mawaziri lililopita, Naibu Mawaziri walikuwa 21 na sasa idadi ni hiyo hiyo.

Mapema Januari mwaka huu, gazeti hili lilijulishwa kuwa mawaziri hao wataondoka katika hoteli hizo mwishoni mwa mwezi huo, lakini hadi sasa wanaendelea kuishi katika hoteli hizo.

Chanzo cha kuaminika kutoka Wizara ya Ujenzi kimeliarifu gazeti hili kwamba bado kuna mawaziri wa zamani ambao hawapo kwenye baraza la sasa, bado hawajaondoka kwenye nyumba za serikali jambo linalowafanya baadhi ya mawaziri wapya kuendelea kukaa kwenye mahoteli.

Chanzo hicho kiliendelea kueleza kuwa sababu zinazotolewa bado zinautata kwa kile kinachoelezwa kuwa nyumba zinafanyiwa ukarabati.

Chanzo hicho kilifafanua kuwa majibu hayo bado ya utata kwani haijawekwa bayana ukarabati huo utamalizika lini wakati serikali inaendelea kupoteza gharama nyingi pasipo na sababu za msingi.

Ofisa mmoja wa Wizara hiyo ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini, alisema ni kweli bado mawaziri wanaendelea kuishi hotelini.

Hata hivyo, alisema kuna baadhi ya mawaziri wamegoma kuishi katika nyumba za serikali kwa madai ya kuwa zina masharti magumu.

Alifafanua kuwa masharti yaliyowakwanza ni kutoruhusiwa kujishughulisha masuala mbalimbali ikiwemo kutolima mboga wala kufuga.

"Unajua kuna baadhi ya mawaziri walikuwa wakiishi katika nyumba zao ambapo walikuwa wanajishughulisha na mifugo yao halafu leo hii waambiwe wasijushughulishe na masuala yoyote yale jambo ambalo wameona wamewekeo masharti magumu sana hiyo ndio sababu ambayo imewafanya wasije katika nyumba zao walizowekewa kwani wanajiona hawapo huru," alisema ofisa huyo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Hurbert Mrango, ili azungumzie suala, hakukanusha wala kuthibitisha lakini alisema asingweza kulizungumzia kwa maelezo kwamba alikuwa kwenye kikao.

Msemaji wa Wizara hiyo, Martin Ntemo, alipotafutwa alimtaka mwandishi kuandika maswali na kuahidi kuyapeleka kwa Balozi Mrango ili ayatolee ufafanuzi.

Hata hivyo, ni takribani wiki mbili sasa tangu maswali hayo yalipowasilishwa wizarani hapo bila kupatiwa majibu yoyote.

Ntemo alipoulizwa majibu ya maswali hayo alisema kuwa mpaka sasa bado hajapatiwa majibu hayo.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Hilo la kukatazwa kulima mboga mboga kwenye manyumba ya serikali linahusikanaje na kuendelea kuishi hotelini! Kwani huko hotelini wanaruhusiwa kulima mbogamboga?
 
Hilo la kukatazwa kulima mboga mboga kwenye manyumba ya serikali linahusikanaje na kuendelea kuishi hotelini! Kwani huko hotelini wanaruhusiwa kulima mbogamboga?

Hapo ndio pa kujiuliza, wanazua visababu tu na viongozi wakuu wanawaangalia!!!
 
mimi sijawahi kuelewa logic behind ya huu uamuzi wa kuuza nyumba za serikali(Mkapa na magufuli may know better). unauza nyumba ya mwalimu je unategemea mwalimu mpya akaishi wapi? tena walikarabati nyumba hizo kwa bei kubwa na kuziuza kkwa bei ya chini! ambayo haifikii hata thamani ya kiwanja chake?
Je kwa wasio waajiriwa wa serikali inakuwa kama wananyimwa haki fulani na wenye ajira mpya au new appointments wakae wapi?
gharama wanazolipa kulipia mahotel zingejenga au kukarabati nyumba ngapi? wauze basi na ikulu kwa mpangaji aliopo sasa tujue moja
 
Shamba la bibi Mkuu kila mtu huwa mvunaji. Halafu wanadai Magufuli ni mtendaji mzuri! :nimekataa :nimekataa :nimekataa
 
Kwani zile nyumba mpya za Mawaziri zilizojengwa (na Magufuli) kule Mikocheni nani anakaa huko?
 
huuu ni ufisadi hizo nyumba zilizouzwa zirudishwe na hao maminister wapya walikuwa wanakaa wapi? aaagh nchi maskini hivi mawaziri wanakaa hoteli za kifahari na bado wana mavx mapya ya mil 250, na mil 90 za kukopwa magari bungeni wamepewa hapo bado mishahara na marupurupu yanayolipwa kwa wakati. Huku wavuja jasho na wapiga kazi wa nchi hii tunateseka kudadeki siku nikiingia front na AK- 47 yangu mtu asiniulize kitu!
 
Mantiki ndogo haikubali kuhusisha suala la waziri kukaa hotelini kwa sababu ya kutokupenda nyumba za serikali eti kwa sababu kwenye nyumba za serikali huwezi kulima mboga.
 
huuu ni ufisadi hizo nyumba zilizouzwa zirudishwe na hao maminister wapya walikuwa wanakaa wapi? aaagh nchi maskini hivi mawaziri wanakaa hoteli za kifahari na bado wana mavx mapya ya mil 250, na mil 90 za kukopwa magari bungeni wamepewa hapo bado mishahara na marupurupu yanayolipwa kwa wakati. Huku wavuja jasho na wapiga kazi wa nchi hii tunateseka kudadeki siku nikiingia front na AK- 47 yangu mtu asiniulize kitu!
halafu beside those extravagancy wanasema hamna pesa za kuharibu mabomu ya zamani... yale hayasubiri uwe na pesa na hayaongei muda ukifika!! sasa fidia kwa marehemu,majeruhi,fidia za nyumba za waathirika,kujenga kambi upya na kununua mibomu mingine..hapo hata ngumbaru anajua ni ujinga! yaani hamna priority kwenye mambo nyeti,ila kwenye porojo mjengoni ni first priority if not urgent
 
mchongo wa wenye mahoteli. inawalipa ndo maana maana wanapenda hao mawaziri waendelee kukaa humo hotelini. Hela ya mtanzania nani ataipigia kelele/
 
Tanzania, Tanzania............Tanzania yetu!!!!!!!!!!!!!!!!

Alafu tunaulizana kwanini hii nchi ni maskini?
 
Katibu mkuu mzima wa wizara anaulizwa anadai hana jawabu wakati utakuta yeye ndiye au wizara yake ndio inasaini check za malipo kutoka kwenye hayo mahoteli hii ni sawa kabisa na fisadi mkulima pinda kulalamika kuhusu ununuzi wa magari ya kifahari wakati ofisi yake ndio inasaini check za kununua magari hayo. Yaani nchi hii ni unafiki mtupu.
 
Hivi kwani mawaziri hawawezi kupewa allowance ya nyumba??? Mie nahoji tu

Wapewe allowance ya nyumba ya nini bana huku mbona nchi tajiri lakini mawaziri wanajitegemea huu ni upuuzi. Mimi nasema mwaka huu kama moto haujawashwa kuanzia ngazi ndogo ndipo tumfikie mkulu huu ni upuuzi na upumbavu kupita kipimo. Ujinga huu unatoka wapi lakini mbona hivi????????????????????????
 
Kwani zile nyumba mpya za Mawaziri zilizojengwa (na Magufuli) kule Mikocheni nani anakaa huko?

Mkuu hizo hawazitaki kabisa kwani zinawafanya waishi kama vile wako kambi ya jeshi au Hostel!!!!

Tiba
 
Wapewe allowance ya nyumba ya nini bana huku mbona nchi tajiri lakini mawaziri wanajitegemea huu ni upuuzi. Mimi nasema mwaka huu kama moto haujawashwa kuanzia ngazi ndogo ndipo tumfikie mkulu huu ni upuuzi na upumbavu kupita kipimo. Ujinga huu unatoka wapi lakini mbona hivi????????????????????????

Dada sijui kaka,

Hata ulaya wanapewa allowance za nyumba kama motisha ya kazi. Ila kwanini serikali iwagharamie kuwaweka hotelini wakati hii ni kazi ya kutumikia umma. Ninapouliza allowance namaanisha serikali ina uhuru wa kupima kiasi walipwe na je hizo pesa zinakidhi mahitaji ya average politician in Tanzania. Ukitaka kukaaa vizuri basi tafuta nyumba unayodhani unaweza kumudu kama serikali imeshindwa kukulipia venginevyo ndio tunarudi pale pale tu ufisadi juu ya ufisadi.
 
Matatizo ya haka ka-nchi ni kama vile hayawezi kupata mwarobaini wa kuyatatua. Kila kitu ccm na washirika wao wanachofanya ni usanii na kuwaletea tabu wananchi wa kawaida. Usanii juu ya Usanii!
 
Back
Top Bottom