Mawakili wa Gwajima wamwandikia Kova barua

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,684
8,833
kova1.jpg

WAKILI wa Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, Peter Kibatala, ameliandikia barua Jeshi la Polisi nchini akiomba vifungu vya sheria vilivyotumika kuomba nyaraka za umiliki wa vitu mbalimbali vya Askofu huyo.

Pamoja na hilo, Kibatala aliomba mteja wake huyo kuambiwa kwa maandishi juu ya vitu vinavyotakiwa kuwasilishwa kwa Jeshi hilo.

Barua hiyo ambayo Kibatala ameielekeza kwa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, pia nakala yake ameituma kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu na kwa mteja wake huyo.

"Kwa barua hii tunaomba Jeshi la Polisi kwa niaba ya mteja wetu kumwandikia rasmi kwa maandishi mteja wetu mkiainisha nyaraka mnazohitaji na vifungu vya sheria vinavyotumika na Jeshi la Polisi kutaka nyaraka hizo.

"Tutashukuru kupata hati hiyo, ambayo bado hatujaipa jina, kwani tunategemea jeshi hilo litafahamu jina la kisheria la nyaraka husika inayotumika kutaka mteja wetu alete nyaraka tajwa na mara tu mteja wetu akipata maandishi tuliyoomba atatimiza wito au kuchukua hatua stahiki za kisheria," ilisomeka sehemu ya barua hiyo.

Juzi wakili mwingine wa Gwajima, John Mallya, alilalamikia hatua ya polisi akisema mahojiano yalichukua mambo binafsi badala ya kile alichoitiwa na kutakiwa kuwasilisha vitu 10.

Wakili huyo alitaja mambo yanayotakiwa kuwasilishwa polisi kuwa ni hati ya usajili wa kanisa, namba ya usajili, majina ya Baraza la Wadhamini (Baraza la Kiroho), idadi ya makanisa (matawi) anayohudumia, nyaraka za helikopta ya kanisa na muundo wa uongozi wa kanisa.

Vitu vingine ni waraka wa maaskofu uliosomwa makanisa yote, nyaraka za nyumba na mali za kanisa, nyaraka kuonyesha taarifa za hesabu kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Hiari na kuambatana na mtu anayepiga picha za video kanisani hapo.

Hata hivyo, katika barua ya wakili huyo wa Gwajima, Kibatala, ilieleza kwa mshangao kwamba Askofu huyo, ambaye anatuhumiwa au anapelelezwa kuhusiana na tuhuma za kutoa lugha ya matusi wakati wa mahojiano, hakutaarifiwa kama tuhuma hizo ziko chini ya kifungu gani cha sheria.

Gwajima alitakiwa kurejea katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam Aprili 16, mwaka huu, akiwa na vitu hivyo 10, hatua ambayo imekuja kinyume na matarajio ya wengi kuwa kiongozi huyo angekuwa anahojiwa tu kuhusu matamshi yake ya kashfa dhidi ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Kutokana na matamshi hayo yaliyosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii kwa njia ya video na sauti, Gwajima alitakiwa kuripoti polisi kuhojiwa Machi 27, mwaka huu, ambapo kabla ya kukamilika kwa mahojiano aliishiwa nguvu na kupelekwa hospitalini alikolazwa kwa siku nne, huku taarifa zikieleza kuwa alishtushwa na kuhojiwa taarifa binafsi badala ya tuhuma alizoitiwa polisi.

Baada ya kutoka hospitalini, Gwajima aliendelea kutembea akiwa kwenye kiti chenye magurudumu, alichotumia hadi Aprili 6, alipohubiri katika Ibada ya Pasaka ambako alionekana kusimama kutokana na kudai kuombewa na wachungaji wageni waliofika kanisani hapo kutoka Japan.

Kamishina Kova hakupatikana kuzungumzia kupokea barua hiyo kutokana na simu yake kuita bila majibu.


Chanzo: Mtanzania
 
Watu wanapenda kushughulika sana! yeye kama anavyo si apeleke kuwazodoa......anapoteza mda na pesa na mawakili wake wakati ni kitendo cha saa1 tu!!!
Au anaelewa ataumbuka???
 
Mwisho wa gwajima umetimia. Hata angetetewa na wakili gani ukianza kupambana na dola ujue kushnei. Frola atajuta, bora angekaa kwa mbasha
 
Watu wanapenda kushughulika sana! yeye kama anavyo si apeleke kuwazodoa......anapoteza mda na pesa na mawakili wake wakati ni kitendo cha saa1 tu!!!
Au anaelewa ataumbuka???

Akipeleka hizo nyaraka ataambiwa apeleke tena nyaraka zinazohusu mahari aliyotoa wakati anaoa! Ni afadhali waseme wanahitaji nyaraka hizo kwa mujibu wa Sheria gani ili tuhuma zieleweke! Pia awe anaitwa kwa barua na sio kujipeleka tu kwa kusikia tu kwenye vyombo vya habari!
 
Yeye SIO DOLA, that is why baada ya kutukanwa amekaa kimya. Gwajima kwa mdomo wake alisema haogopi DOLA: haogopi Polisi, haogopi mahakama na wala haogopi Bunge...That is what he said, kumbe wakili wa nini ?

...yupo sawa hupaswi kuogopa taasisi zilizowekwa kwaajili ya kutenda haki. Kwanini ziogopwe kwani zimekuwa magaidi ? Kimsingi hata rais anapaswa kuheshimiwa na sio kuogopwa...
 
Ngoja tusubiri. Au hana nyaraka nn. Si apekeke yaishe....

...sheria lazima ifuatwe,we ukiombwa hati ya nyumba unampa mtu bila maandishi ?akikuruka utakimbilia wapi kwa ushahidi gani ? Pale polisi mahabusu anashikwa na laki tano mfukoni anaandikisha kwenye jalada wakati anavua nguo na kukabidhi kwa polisi,wakati wa kutoka anakuta ameandikiwa aliacha elfu tano,utawaamini polisi hapo ? Zipo case za kuibiwa engine za magari yaliyokamatwa...
 
Kova na team yake uzee unawajia vibaya,nasi wawaandikie barua kina kakobe,lusekelo,mwingira,nabii flora na mwakasege wapeleke nao vielelzo hivyo.

Tehee....teehee...tihii ! hiyo itakuwa fujo, wanaanza na Gwajey then wengine kufuatia. Kwani unahisi hao wana shida na vielelezo vyao !?
 
...yupo sawa hupaswi kuogopa taasisi zilizowekwa kwaajili ya kutenda haki. Kwanini ziogopwe kwani zimekuwa magaidi ? Kimsingi hata rais anapaswa kuheshimiwa na sio kuogopwa...

Kwani hizo taasisi ziliwahi kumtishia !?
 
...sheria lazima ifuatwe,we ukiombwa hati ya nyumba unampa mtu bila maandishi ?akikuruka utakimbilia wapi kwa ushahidi gani ? Pale polisi mahabusu anashikwa na laki tano mfukoni anaandikisha kwenye jalada wakati anavua nguo na kukabidhi kwa polisi,wakati wa kutoka anakuta ameandikiwa aliacha elfu tano,utawaamini polisi hapo ? Zipo case za kuibiwa engine za magari yaliyokamatwa...

sina hamu na hao watu!!
wananjaa kufa, tena woooooote regardless their levels, kwa level ndo wanatofautiana aina ya njaa,
ndugu yangu aliwekwa hapo oysterbay alikuwa na cm, hela na vitu vingine!!! alikaa siku tatu tu, siku ya kutoa hahahaaaaa vituko no money wakat zimeandikwa, simu zilibadilishwa,

tukaamua kuitresi cm lengo tumjue tu aliyenayo tukaikuta kwa mke wa askar mmoja wa palepale, tukwambia hatuitaki cm ila tulitaka tujue mchezo ulikuwaje! enjoy your life!!
 
Policcm wameshindikana. Kwa matendo ya polisi kwa watz ambayo nimaagizo ya ccm basi ccm inazidi kutumbukia shimoni.
Watz tukatae uonevu huu. WAHENGA WALISEMA, LEO KWANGU KESHO KWAKO CHUKUA HATUA
 
Yule ajaye,amekuja tayari.Yule aliye na cheo serikalini na kufanya uovu wazi au kwa siri dhidi ya wanadamu juu ya nchi wakati unakuja atashushwa chini na mwisho wake utakua mbaya.
 
Back
Top Bottom