Mavazi ya Nyerere na kuiga kutoka China

Safi sana Kichuguu kwa kutoa taarifa inayoendana na utafiti murua.
 
Mjengwa ni mzuri sana kwa hadithi za Sungura na Paka. Kuna makala za Mjengwa ukiona heading tu unajua itakuwa na bias. Makala yake ikiisha, hebu tupatie uchambuzi wako tupate kuelimika. Inasikitisha kwamba mambo mengi kumhusu Nyerere baadhi ya watu wanelezea kama hadithi wakati facts zipo na hili kuhusu mavazi yake ni moja kati ya mengi ambalo Mjengwa ameliweka bila kufanya utafiti. Nyerere alikuwa mwanazuoni (scholar), mambo mengi sana ameyaandikia vitabu na machapisho mbalimbali (zaidi ya 200), sasa kama unataka kumkosoa ni vizuri ukaja na hoja za kisomi sio hadithi za fulani alisema hivi ambazo haziwezi kuthibitishwa. Hongera ndugu Kichuguu.
 
Shukrani sana Bwana Kichuguu
hapa ndipo JF inaporudi enzi zake, zile henzi za kuleta Hoja yenye Ushahidi na walasio adhithi za vijiwe vya Kahawa, na hoja/Thread kama hizi huwa zinawafukua wakongwe wengi ambao mara nyingi huwa wapo pembeni wanaangalia vioja
 
good job mkuu,tumepata utirio safi kabisa.Kuiga kupo na sidhani kama leo hii utaweza sema neno lolote hapa duniani ambalo halijawahi kutumika kabla.Cha msingi ni kuweka na ya kwako na siyo ku copy na ku paste vitu kama vilivyo.Yesu mwenyewe aliiga misemo ya watu,itakuwa Nyerere?
 
ndugu yangu kichuguu shukrani sana kwa thread hii, pia ndugu yangu Kiranga pongezi zako kwa mchango/ufafanuzi zaidi. JF noma
 
Kwani hayo mavazi yana tatizo gani?
Hayana matatizo yoyote, ila tunataka kuweka rekodi sahihi. Siyo kweli kuwa Nyerere aliiga mavazi hayo kutoka kwa Mao baada ya kutembelea China. Rekodi zilizopo zinaonyesha kuwa alianza kuyavaa mara tu baada ya Muungano, kabla hata hajatangaza Azimio la Arusha 1967.
 
Maneno mengine ya kuiga ya nyerere ni haya: Tanzania haitakuwa huru mpaka Africa nzima iwe huru. Haya ni maneno ya Raisi wa marekani mwaka 1963 JF Kened alipokuwa nawatetea haki za wamarekani weusi. American can not be free not until all black people are free. Halafu maneno kama Nitaona haya kumuonea haya mzebe na mzululaji. Haya aliyakopi kutoka mao Tsedong wakati alipokuwa nawakama kamata wazururaji mijini na kuwafunga mashambani kama watumwa. Jamani mano mtetea nYerer tuambieni ni mafanikio gani kiuchumi katuletea ambayo kamshinda hata kenyatta? utaona hakuna ila yeyey ni jina kubwa Non alignmnet na South South commissio, au siyo?

Soma vizuri post hiyo tena; haina lengo la kumtetea au kumsifia Nyerere, ila inaweka rekodi sahihi kuhusu mavazi yake ya neckless. Uzuri au ubaya wa Nyerere siyo mada ya thread hii, inalenga kuimarisha umuhimu wa watu kutumia rekodi sahihi za matukio mbalimbali bila kuyageuza kwa nia ya ama kumsifia au kumdhalilisha mtu yeyote kwa namna yoyote ile.

Ingawa si vibaya mtu kutumia statement iliyowahi kutolewa na mtu mwingine iwapo statement hiyo inarahisisha kufikisha ujumbe wake, hata hivyo siyo kweli kuwa statement iliyo niliyo bold ilitolewa na Kennedy mwaka huo 1963. Hiyo ilikuwa ni motto ya mkutano wa Pan-African Congress ulioitishwa na Kwame Nkurumah mwaka 1958 huko Ghana ukijulikana kama The All-African People's Conference. Agenda kubwa ya mkutano huo iliitwa HANDS OFF AFRICA! AFRICA MUST BE FREE!, ambapo walisistiza umuhimu wa kuikomboa afrika yote na uwezekano wa kuinganisha na kuwa kitu kama US of Africa. Ni kutokana na makubalianao ya mkutano huo ndiyo maana Nyerere alianza kujihusisha na harakati za ASP katika kugombea wa uhuru wa Zanzibar ingawa Tanganyika nayo ilikuwa bado haijapata uhuru wakati huo.

baada ya uhuru wa Tanganyika, mwendelezo wa siasa za Pan-Africanism ulimfanya Nyerere kuanzisha PAFMECA hapa afrika ya Mashariki, ambayo haikudumu sana, na badala yake tukabaki na EAC ambayo nayo ilikufa mwaka 1977
 
Sababu ya Nyerere kuvaa chonlai ni hii; (japo sina data kamili) Nyerere alienda Marekani na Uingereza kuwaomba msaada wa ujenzi wa reli ya TAZARA. Wazungu wale wakamzungusha mno mwalimu na kumkatisha tamaa kuwa labda miujiza itokee ndipo hiyo reli ipite huko Nyerere anakotaka. Na ni mradi wa karne. Akaachana na wazungu akaenda china (ya enzi zile). Mao akamwambia hilo linawezekana. Bajeti ikapangwa, wataalam wakatafutwa, kazi ikaanza. Ruti ile ile ambayo wazungu waliikosoa. Sikumbuki ilitumia muda gani lakini ilikamilika. Nyerere akasema kuna haja gani ya kujivika utamaduni wa hawa wakoloni na masuti yao. Akatupa suti kule akaanza kuwaenzi wachina-wajamaa wa ukweli
 
Kuna ukweli mdogo sana katika maneno yako, sehemu kubwa siyo kweli. Soma tena post yangu ya kwanza hapo juu kuonyesha kuwa hizo nguo Chou en Lai, kama zilivyokuwa zikijulikana, hazikuwa staili ya wachina, na wala Nyerere alipoanza kuzivaa alikuwa bado hajavunja uhusiano na nchi za Magharibi.

Ombi la Ujenzi wa Tazara lilitolewa na Nyerere wakati wa ziara yake ya February mwaka 1965 huko China, lakini ombi hilo halikukubaliwa mara moja mpaka mwaka 1967 ndipo China ilipojiamnisha kuwa itaweza kujenga reli ile. Nyerere alianza kuvaa nguo hizo mwaka 1964 kabla hata hajavunja uhusiano na nchi nyingi za Magharibi; hasa Ujerumani Magharibi na Marekani. Ni kweli kuwa baada ya Muungano, Nyerere alipewa push sana na Ujerumani ili kuwazuia wachina na East german wasiingie Tanzania kupitia zanzibar, lakini Nyerere aliwafukuza wajerumani wale wakaamua kubomoa baadhi ya barabara walizokuwa wameshaanza kujenga pale Dar. Kuvunjika kwa uhusiano na Marekani kulichangiwa zaidi na msimamo Marekani kuhusianina na utawala wa Ian Smith aliyetangaza UDI huko Southern Rhodesia (Zimbabwe) na kuendesha serikali ya nchi ile kwa kubagua rangi. Ingawa kuna matukio mengine ya kijasusi yaliyofanwa na CIA kupitia ofisa wa ubalozi Richard Carucci ya kutaka kuua viongozi kadhaa wa zanzibar ( hasa Babu na Karume) na hivyo kuchochea hasira za Nyerere dhidi ya Marekani baada ya rafiki yake Kennedy kuwa keshauwawa. Huyu Caruci ndiye aliyefanikisha mauaji ya Lumumba huko Kongo.

Ngua zile hazikuwa na uhusiano na China: si ujamaa wala TAZARA iliyosababisha nguo zile, ilikuwa staili iliyobuniwa hapo Magagoni tu
 
Hayana matatizo yoyote, ila tunataka kuweka rekodi sahihi. Siyo kweli kuwa Nyerere aliiga mavazi hayo kutoka kwa Mao baada ya kutembelea China. Rekodi zilizopo zinaonyesha kuwa alianza kuyavaa mara tu baada ya Muungano, kabla hata hajatangaza Azimio la Arusha 1967.
Labda aliyapenda baada ya kuwaona Makomredi wa kiukweli, akina Abrahaman Babu.
 
Maneno mengine ya kuiga ya nyerere ni haya: Tanzania haitakuwa huru mpaka Africa nzima iwe huru. Haya ni maneno ya Raisi wa marekani mwaka 1963 JF Kened alipokuwa nawatetea haki za wamarekani weusi. American can not be free not until all black people are free. Halafu maneno kama Nitaona haya kumuonea haya mzebe na mzululaji. Haya aliyakopi kutoka mao Tsedong wakati alipokuwa nawakama kamata wazururaji mijini na kuwafunga mashambani kama watumwa. Jamani mano mtetea nYerer tuambieni ni mafanikio gani kiuchumi katuletea ambayo kamshinda hata kenyatta? utaona hakuna ila yeyey ni jina kubwa Non alignmnet na South South commissio, au siyo?
Haya ndio matatizo ya waandika historia wa leo (revisionist); Nyerere ameanza kuzungumza hivyo kabla ya Kennedy kuchaguliwa kuwa Rais, ndio maana tunawaambia msomeni kidogo mtashangaa how far ahead alikuwa yeye.
 
Katika hotuba ya Tangazo la Vita dhidi ya Iddi Amin pale Diamond Jubilee Hall kwa mfano, sehemu inayokumbukwa sana ni pale aliposema "Nia tunayo, uwezo tunao, sababu tunayo" etc. Watu wengi wanafikiri haya ni maneno ya Nyerere originally, actually haya ni maneno ya bendi moja ya Kiingereza wakati wa vuguvugu la Uingereza kutaka kuingia vitani dhidi ya Hitler.
Hapa kwa kweli hata mimi umenigusa, nilikuwa naamini tangu enzi zile hayo ni maneno originally ya Nyerere. Umejuaje kama Nyerere aliyakopi kutoka kwenye bendi hiyo?
 
Haya ndio matatizo ya waandika historia wa leo (revisionist); Nyerere ameanza kuzungumza hivyo kabla ya Kennedy kuchaguliwa kuwa Rais, ndio maana tunawaambia msomeni kidogo mtashangaa how far ahead alikuwa yeye.

Hicho ndicho kinachoniudhi sana katika waandishi wengi wa kitanzania leo ambao hawataki kutafuta rekodi sahihi, hata kama haziwafurahishi, ili watoe ukweli kama ulivyo. Kila siku wanataka kupindisha ukweli. Ninalaumu sana Ikulu yetu kwa kutotunza rekodi sahihi za maraisi waliopita. Nimefurahishwa sana na ofisi ya waziri mkuu na Bunge kwa vile ingawa rekodi zao zina mapungufu, bado zinasaidia sana kujibu maswali mengi kuliko Ikulu.
 
.....
Ukisoma habari zote za "Siasa Ni Kilimo" (how many read these?) halafu ukaangalia "The Great Leap Forward" (that laughingstock of the Chinese) unaona mzee anafuata nyayo zile zile za Mao. But to take this as an example that Nyerere was in the pocket of the Chinese would be a mistake. Nyerere was much more complex than that.
Mimi nilisoma vitabu hivyo pamoja na vile vya kikomunist kutoka China, Korea na Urusi ikiwa ni sehemu ya ya DS100 na DS200 hapo UDSM miaka ya themanini. Ninakuhakikishia kuwa Siasa ni Kilimo siyo kopi ya The Great Leap Forward.

Katika hotuba ya Tangazo la Vita dhidi ya Iddi Amin pale Diamond Jubilee Hall kwa mfano, sehemu inayokumbukwa sana ni pale aliposema "Nia tunayo, uwezo tunao, sababu tunayo" etc. Watu wengi wanafikiri haya ni maneno ya Nyerere originally, actually haya ni maneno ya bendi moja ya Kiingereza wakati wa vuguvugu la Uingereza kutaka kuingia vitani dhidi ya Hitler.
...............

Hapo umenifundisha na nitakapokuwa na nafasi nitatafuta stori hiyo kikamilifu. Hata hivyo kama nilivyomjibu mtu mmja hapo juu, si vibaya kutumia maneno ya mtu mwingine kama maneno yale yanakurahishia kufikisha ujumbe wako. Lugha ni kitu ambacho kimekuwapo miaka nenda rudi, kwa hiyo reusability ya baadhi ya statements kaqma vile methali si jambo la kushangaza.
 
Imebidi nipitie hotuba ya Nyerere akitangaza vita. Baada ya kuzungumza kwa kirefu kuelezea kilichojiri muda wote huo alienda na kusema "Watanzania tunayo kazi moja tu; Watanzania tunayo kazi moja tu ni kumpiga (makofi). Uwezo wa kumpiga tunao(pause), uwezo wa kumpiga tunao(pause) na nia(msisitizo) ya kumpiga tunayo. Na sasa tutampiga..tunataka dunia ituelewe hivyo" Ningependa kuyapata maneno hayo ya hiyo bendi kulinganisha isije kuwa watu wanaokabiliwa na tishio la aina moja wameweza kuwa na mwitiko wa aina moja.
 
Kwa hiyo, ingawa hatujui ni lini Nyerere na viongozi wenzake wa Tanzania walianza kuvaa hizo nguo za neckless, ni wazi kuwa alianza kuzitumia kabla au mara tu baada ya Muungano, April 1964 lakini ikiwa kabla hajasafiri kwenda China mwaka 1965.
Kuna picha ya Nyerere akiwa na suti isiyo na kola kabla ya February 1965?
 
Back
Top Bottom