Mavazi ya Nyerere na kuiga kutoka China

Kaka sijasema kuwa ni Mavazi ya Kichina, nasema labda ameiga kutoka kwa Makomredi wa kiukweli i.e Abrahaman Babu.
Lets give credit where it belongs na tuache kuangalia mambo kwa kuweka mbele uzalendo:-
beatles5990.jpg
 
attachment.php

.... akiwa amezungukwa na mawaziri wenye hizo suti. By the way ni nini kinachokufanya u-conclude kuwa aliiga Uchina na siyo kwa hao mawaziri waliomzunguka?
Mada yetu hapa sio Kambona kavaa nini, au Kawawa kavaa nini. Ushahidi wa picha wa Kichuguu una mushkeli kwa maana Nyerere hajavaa suti isiyo na kola.

Tumeonyesha, na Kichuguu kakubali, kwamba hakuna picha ya Nyerere akiwa kavaa suti isiyo na kola kabla ya safari ya Uchina.

Sasa mkuu, hizo credit belongs to whom, maana hapa umeweka picha na haijulikani kama hawa ni Wa Kyuba au Wamongolia.
Mkuu The Beatles nadhani hawa ndio tunaweza kusema waliifanya collaless suit iwe fashionable na kuhusu nani aliye-invent well kuna debate kama alikuwa ni Pierre Cardin au Douglas Millings; angalia hii extract

In my research I've often come across statements like "Pierre Cardin designed the iconic suits of The Beatles" and that "The Beatles made Pierre Cardin's suit fashionable in the 1960s" but I don't believe that Cardin deserves so much credit for this accomplishment. Although Millings is well known to Beatles fans, he is often only an afterthought when it comes to analysis of Beatles fashion.
Source: The Fashion Culturist: Who Dressed The Beatles?: Pierre Cardin, Douglas Millings and the Collarless Suit of the 1960s
angalia mwenyewe Cardin design left na millings design right
car.jpg
bt.jpg
 
Nyerere was more influenced by his African upbringing and Scottish/ Fabian society Socialism while at Edinburgh than any Eastern type of communism. Why do you think he kept Joan Wickens at Ikulu for all those years ?

Lets give credit where it belongs na tuache kuangalia mambo kwa kuweka mbele uzalendo:-
beatles5990.jpg

Asante sana kwa kutuletea picha hii ya jamaa wa Beatles, na nadhani hii inaimarisha imani yangu kuwa ni vazi lililobuniwa hapo Magogoni likiwa linatumia influence za Nyerere kutokea Scotland kama Kiranga alivyosema hapo juu. Bendi hii ya Beatles ilianza kutumia vazi hilo mwaka huo huo 1964 ambao ndio pia Nyerere alipoanza kulitumia. Uamuzi wa Beatles kuvaa vazi la namna hiyo ulikuwa influenced na mavazi ya mfalme wa zamani wa uingereza King Edward wa Kwanza. Mashati ya Mfalme huyo hayakuwa na kola kama anavyoonekana hapa.

attachment.php

Gal_nations_edward_i.jpg
Kati ya mambo makubwa yaliyofanywa na mfalme huyo ni kuunganisha nchi za Scotland, Wales na England chini ya himaya moja ya UK, na alikuwa na influence sana huko Scotland. Inawezekana Nyerere na watu wake waliamua kulivaa vazi hilo kwa msingi wa historia hiyo ya kuungana, hatujui.

Kwa vyovyote vile, staili hiyo haikutokea China kama ambavyo inavyoonyesha kuwa hata bendi ya Beatles ilitumia staili hiyo. Madai ya kuwa Nyerere aliiga vazi hilo kutoka China si ya kweli, kwani alianza kulivaa tangu mwaka 1964 karibu mwaka mzima kabla hajaenda China. Na wala vazi hilo halifanani kabisa na mavazi ya wachina
 
Ndugu yangu Kichuguu,
Awali ya yote, nikushukuru kwa michango yako ya fikra. Ni kazi njema.
Pili, ulichoandika kuhusu mavazi ya Nyerere na uhusiano na safari ya Uchina yaweza pia usiwe ukweli kamili. Na tuwe kwenye lile kundi la wenye kujitahidi kujua na si wale wanaodhani wanajua. Kikubwa hapa ni lililo jema katika kiu yetu ya kuitafuta kweli, kujitahidi kujua. Binadamu hutakuwa umefanya tendo la busara endapo utaelekeza nguvu zako katika kumbeza mwanadamu mwenzako anayejitahidi kujua. Tukosoane, lakini tusibezane. Mwuungwana habezi.

Na siku zote, tusikate tamaa na wala tusikatishane tamaa katika kuitafuta kweli na zaidi kujitahidi kujua. Ni jitihada hizi za kuitafuta kweli na kujitahidi kujua ndizo zitakazotupa maarifa mapya. Yatatusadia kujenga mustakabali ulio bora kwa taifa letu.

Kuna mengi tumeambiwa kwa miaka 50 sasa ya uhuru wetu; mengine ya kweli, na mengine hayana ukweli. Mjadala ulioanzisha wa vazi la Nyerere umesaidia kutupa maarifa mapya pia. Na labda hukulijua hili, kuwa safari ya Nyerere Uchina na kukutana na Mao Tse Tung mwaka 1965 haikumaanisha kuwa Nyerere hakuwahi kukutana na kiongozi yeyote wa Uchina kabla ya hapo.

Ni hivi; Waziri Mkuu wa China Zhou En Lai hapa kwetu alikuwa maarufu kama Chun Lai alizunguka Afrika mwaka 1963 katika jitihada za kutafuta marafiki na kujenga mahusiano na viongozi wapya wa Afrika. Kati ya aliokutana nao ni Julius Nyerere. Na je, siku hiyo Zhou En Lai alivaa vazi gani?

Na sie wa kizazi cha Azimio bado tunakumbuka vazi maarufu la ' Chun Lai'. Ndio, kuna watu enzi hizo waliambiwa walivaa ' Chun Lai'. Ikaja pia ' Kaunda Suti'. Hata mie utotoni niliwahi kushoneshewa ' Kaunda Suti' kama vazi la siku ya Siku Kuu!

Siku njema.
Maggid
 
Ndugu Zangu,

Haya usomayo ni majibu yangu kwenye mjadala wa mavazi ya Nyerere hapa JF.
Kwenye mjadala husika nimeandika haya;

Linkoping, Sweden
Jumapili, Julai 10, 2011
MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
 
Mkuu nijuavyo mimi vazi la nyerere lilikua linatengenezwa/linashonwa peramiho, hayo ya china unayajua mwenyewe!
 
kimuonekano suti bila ya collar za kina Nyerere zinafanana zaidi na suti za Wachina kuliko suti za Western.

Kwa hiyo labda wanaofananisha suti za kina Nyerere na za Chu Enlai ni kwa sababu ya muonekano wake bila ya kuzingatia uwepo wa collar yenyewe au la
 
Ndugu Zangu,

Tukosoane, lakini tusibezane. Mwuungwana habezi.

Na sie wa kizazi cha Azimio bado tunakumbuka vazi maarufu la ' Chun Lai'. Ndio, kuna watu enzi hizo waliambiwa walivaa ' Chun Lai'. Ikaja pia ' Kaunda Suti'. Hata mie utotoni niliwahi kushoneshewa ' Kaunda Suti' kama vazi la siku ya Siku Kuu!

Siku njema.
Maggid
Linkoping, Sweden
Jumapili, Julai 10, 2011
MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo

Mkuu ndio maana tunakusoana hapa sasa wewe kwa kutupa hiyo Chun Lai Suit bila ya kuweka picha yake hapa tukaona difference itakuwa vigumu kukubaliana na wewe anyway hata kama ikiwa identical 100% itakuwa bado ni guess work tu sababu hakuna mtu atakayesema for sure aliipata wapi, na I can argue the Beatles Suit ni more identical na sababu walikuwa famous ilikuwa rahisi kwa watu kuiona kutoka kwao, pili kuna major difference btn nyerere suit na chiniese suit na kuna similiarities kubwa zaidi btn Nyerere Suit na Beatles Suit.

Unajua without facts its mere speculations, na mimi naweza kusema nyerere aliiga kubeba fimbo kutoka kwangu!!, Just sababu nilikutana nae kabla hajaanza kubeba fimbo!!, lakini was I the first ku-invent the fimbo
 
Ndugu yangu Kichuguu,
Awali ya yote, nikushukuru kwa michango yako ya fikra. Ni kazi njema.
Pili, ulichoandika kuhusu mavazi ya Nyerere na uhusiano na safari ya Uchina yaweza pia usiwe ukweli kamili. Na tuwe kwenye lile kundi la wenye kujitahidi kujua na si wale wanaodhani wanajua. Kikubwa hapa ni lililo jema katika kiu yetu ya kuitafuta kweli, kujitahidi kujua. Binadamu hutakuwa umefanya tendo la busara endapo utaelekeza nguvu zako katika kumbeza mwanadamu mwenzako anayejitahidi kujua. Tukosoane, lakini tusibezane. Mwuungwana habezi.

Na siku zote, tusikate tamaa na wala tusikatishane tamaa katika kuitafuta kweli na zaidi kujitahidi kujua. Ni jitihada hizi za kuitafuta kweli na kujitahidi kujua ndizo zitakazotupa maarifa mapya. Yatatusadia kujenga mustakabali ulio bora kwa taifa letu.

Kuna mengi tumeambiwa kwa miaka 50 sasa ya uhuru wetu; mengine ya kweli, na mengine hayana ukweli. Mjadala ulioanzisha wa vazi la Nyerere umesaidia kutupa maarifa mapya pia. Na labda hukulijua hili, kuwa safari ya Nyerere Uchina na kukutana na Mao Tse Tung mwaka 1965 haikumaanisha kuwa Nyerere hakuwahi kukutana na kiongozi yeyote wa Uchina kabla ya hapo.

Ni hivi; Waziri Mkuu wa China Zhou En Lai hapa kwetu alikuwa maarufu kama Chun Lai alizunguka Afrika mwaka 1963 katika jitihada za kutafuta marafiki na kujenga mahusiano na viongozi wapya wa Afrika. Kati ya aliokutana nao ni Julius Nyerere. Na je, siku hiyo Zhou En Lai alivaa vazi gani?

Na sie wa kizazi cha Azimio bado tunakumbuka vazi maarufu la ' Chun Lai'. Ndio, kuna watu enzi hizo waliambiwa walivaa ' Chun Lai'. Ikaja pia ' Kaunda Suti'. Hata mie utotoni niliwahi kushoneshewa ' Kaunda Suti' kama vazi la siku ya Siku Kuu!

Siku njema.
Maggid

Nimesikia ushauri wako na sikuwa na maana ya kubeza kazi yako bali nilikuwa nasahihisha ile statement moja tu uliyoandika kule. Uliposema kuwa baada ya kurudi kutoka China (yaani Februari mwak 1965), pamoja na mambo mengine Nyerere alibadilisha nguo zake ziwe kama za Mao. Sikutaka kuileta post hii hapa JF ila ni kwa sababu kule kwenye blogu yako singeweza kupost picha za kusupport record niliyokuwa nataka kuonyesha, na najua kuwa JF ni uwanja wetu sote. Nyerere hakuanza kuvaa nguo zile baada ya kutoka China, bali wanasiasa wote wa Tanzania walianza kuzivaa mara tu baada ya Muungano. Baraza la kwanza la Muungano unawaona kuwa mawaziri wote walikuwa wamevaa namna ile. Pia nguo za wachina zilikuwa na kola, tofauti na hizo za Nyerere ambazo zinafanana zaidi na zile za Bendi ya Beatles kama mtu mwingine alivyoonyesha hapo juu.

Kama uko katika harakati za kutafuta maarifa basi uwe unatoa mawazo yako ukiwa unaweka bayana kuwa hayo ni maoni yako ingawa huna uhakika kamili. Lakini badala yake unazitoa kwa authority fulani kama vile una uhakika kabisa. Hata mimi sijui ni wapi Nyerere alipotoa suti hizo za Collarless, lakini nina uhakika kuwa hakuzitoa China mwaka 1965. Na wasomaji wangu wameelewa kuna sina uhakika alizitoa wapi.

Vinginevyo, critique yangu isikukatishe tamaa ya kutafuta maarifa na kubadilishana na wengine, na wala usiichukulie kuwa personal kwa sababu hatujuani kabisa ingawa nimeshona picha zako nyingi kwenye blogu yako.

NYONGEZA: Statement yako niliyokosoa haikuwa imesema kuwa Nyerere aliiga kwa Chou en-Lai, ilisema kuwa baada ya Nyerere kurudi alianza kuvaa suti zile aonekane kama Mao. Ninajua kuwa Chou En-lai (kama alivyokuwa akijulikana wakati huo alipotembelea nchi kadhaa za Afrika katika kupiga kampeini ya kusaidia China ipate nafasi ya kudumu kwenya umoja wa Mataifa). Yule jamaa alikuwa akivaa nguo sawa kabisa na Mao au za wachina wengine wakati huo ambazo zina kola fupi na zinafungwa vifungo mpaka shingoni kama nilivyoonyesha hapo juu. Ingawa tuliziita nguo zile Chou En Lai, hilo lilikuwa jina la mitaani na wala halikuwa na maana kuwa zilitoka China. Unfortunately, wewe unachukulia hilo la mitaani na kulifanya kuwa linaashiria asili ya nguo zile. Tanzania tumewahi kuwa na na nguo tukiziita Pecos lakini hazikuwa na uhusiano wowote na yule cowboy maarufu Pecos Bill bali jina tu.
 
Kichunguu

Hivi huyu Chu En-Lai ilikuwaje akawa mashuhuri sana Tanzania? Naamini safari yake Africa na Tanzania ilisaidia kumfanya ajuulikane kwa watu wengi, lakini nashangaa kuwa hata wanwake watuwazima, wasiokuwa na elimu rasmi, vijijini ambao hawakukutana nae, wala kumuona zaidi ya kumsikia kwenye taarifa ya habari wanamjua (sort of) habari zake.

Nakumbuka kuna nyimbo moja kwenye ngoma moja ya kijadi inaimbwa hivi ...

Ashakum

"Chu En-Lai, wee, Chu En-Lai, apasua mshipa hajau-try
Mchina, wee, Mchina, apasua mshipa hajaupima"
 
Kuiga ama kuchukua mambo mazuri ya mwingine sidhani kama ni kosa, na kusema Nyerere kaiga hiki ama kile pia si kosa, ila cha muhimu ni kuweka habari sahihi kuwa hiki kimeigwa sehemu fulani, Nadhani Maggid ameshindwa kumuelewa mtoa Mada (Kichuguu), Kichuguu anachosema ni kuwa Nyerere anaweza asiwe mbunifu wa hilo vazi (collarless suit) labda kaiga sehemu, lakini hakubaliani na wewe Mjengwa la kusema Nyerere kaiga hiyo suit kutoka kwa Mao na alianza kulivaa mara tu alipotoka kwa Mao 1965 na kwa msisitizo hilo vazi la bila kosa halina uasili wa Uchina

Kwa Nyerere Kuiga si Tatizo kabisa, hasa akiona ni kitu cha kizalendo na kinaelekea na miosimamo waliyokuwa nayo wakati huo, WIMBO WA TAIFA NI ZAO LA KUIGA KUTOKA AFRIKA KUSINI
 
0UuWl+sZjQAAAAASUVORK5CYII=

KIJANA WETU NAYE AMEKULA GWANDA LA KIAFANDE!!!!! JANA HIYO WANANCHI
 
Back
Top Bottom