Mauaji ya polisi wannne Dar, Mh. Magufuli amweke Mwigulu Nchemba pembeni na kufanya uchunguzi

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,807
Miaka ya Nyuma Yameshafanyika Mauaji kadhaa na Ulipuaji Mabomu, Ambapo watu Waliumizwa na Kwa haraka haraka Chama Fulani cha Siasa Kikashutumiwa, (Chadema) Na aliyewashutumu sio Mwingine Bali Ni ambaye sasa Ni Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba.

Cha Kushangaza Juzi Tu yamejirudia Tena Kwa Polisi Wanne Kuuwawa kwa Jinsi ya Kutatanisa sana, Na Ajabu iliyoje Mwigulu Nchemba anajitokeza tena safari hii, akiwa kama Waziri wa Mambo ya Ndani, Wanasingiziwa tena Ukawa na Operesheni UKUTA, Kisha Inafuatia Kamishina wa Mafunzo wa Polisi Kupiga Marufuku Mikutano ya Ndani ya Kisiasa, akidai Kuna wanaowatuma waendesha bodaboda wanunue petroli ya kuchoma maeneo, Cha ajabu huyo Mtu anayepanga Uhalifu, tena Ugaidi hawamkamati :(

Hisia Zangu Ni Kuwa Kuna Viongozi Waovu sana, Waovu Kupitiliza Waliowatoa Kafara Askari wale Kwa Lengo la Kusingizia au Kupata Kick ya Kuonea na Kusingizia Wengine. Mtu yeyote anayefikiri Kwa Kina atajua Kuna Kioja cha ajabu.
Angalia Historia ya Mwigulu,





Siamini Kama Rais naye atakaa Kimnya Katika Mashaka ya Namna Hii, Mimi Naona sio Vizuri Kumhukumu Mtu lakini Mwigulu Nchemba na Yule Aliye toa Tamko linaloonyesha Maajabu (Kamishina wa Mafunzo) Wawekwe Pembeni Kupisha Uchunguzi Mkali, Vinginevyo Lawama Itamwangukia Rais Ikitokea Kuwa Kuna Hujuma chafu zilifanywa. Inasikitisha sana, sana!


Watazame sana Machoni "yakipepesa Kushoto na Kulia" Utajua Kama anachozungumza, Hakitoki Moyoni. Na Pia Wanaonekana Wakipima sana Maneno yao.
 
Hivi utanyang'anya bunduki Mbili au hata nne kwa ajili ya siasa? Ingekuwa hivyo wakina Salva kiir wangekuwa jela wala Sudan kusini isingekuwa huru Leo.Serekali inaacha kudeal na wahalifu inaongea siasa.ujinga ulioje Chama cha siasa kikaue Askari wawili? Viongozi wetu tunaomba muanze kufikiri japo kidogo tu
 
Nadhani uhalifu huu ni kama wa staki shari.... kuna watu wanampango wa kupata silaha hapa nchini.... sioni kama kuna connection na chama chochote cha siasa wala mwigulu.... ila kuhusisha hili na ukuta ni sawa na kumsingizia jirani kwa sbb uligombana nae jana pindi unapo pata
majanga kwako.... intelegensia inatakiwa iende mbali sana kwenye hili....
 
Jana kwenye mkutano wa waandishi wa habari Tundu Lissu ameuliza maswali ya muhimu sana ambayo ukitafakari unaweza kuelewa kitu .Hakuna lenye mwanzo lisilokuwa na mwisho unaweza kufanya maovu kwa miaka 10 baada ya hapo ukaja kuumbuka.

TIME WILL TELL.
 
Nani kisheria anapaswa kufika wa kwanza eneo la tukio?.

Labda Katiba inasemaje katika hilo ili tusije kusema Rais kavunja Katiba akichukua hatua tunazopendekeza.

Maana hata kabla ya Mwigulu kufika eneo la tukio kuna wananchi ambao ni wa eneo husika je nao hawakuwahi kufika eneo la tukio ila ni Mwigulu tu? Mhhh haingii akilini...ukuta kama kawaida yenu kuchafua watu hasa wale ambao ni tishio kwenu...hamtamuweza Mwigulu na tar mosi septemba wananchi hatutawaunga mkono....
 
Kuna mahali tunalazimishwa kupafikia bila hiyari yetu. Rais achukue hatua bila kuangalia uso wa mtu kwani doa hili ni baya kwake. Na sioni ni kwanini mtuhumiwa huyu hajajiuzulu yeye na waliotangaza makatazo kwenye luninga ili kupisha uchunguzi.
 
Hao police walikuwa na umuhimu gani kisiasa hadi chama cha upinzani kiwavizie kuwaua kwanini wasife akina Dr tulia wenye ugonvi na upinzani muda sana wauliwe police ambao hata chama wanacho kipenda moyoni akijulikani .ila la kusha ngaza ni jinsi wazili alivyo jipiga picha na maiti kama tukio la sifavile na kuitupia mitandaoni
 
Back
Top Bottom