Mauaji ya Kiongozi wa CHADEMA Arusha: Watuhumiwa watoroka mahakamani mbele ya polisi!

Last edited by a moderator:
Mahabusu wawili kati ya sita ambao ni watuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa CDM tawi la USA Arusha wametoroka leo mchana mahamani.

Mahabusu hao wawili ni watuhumiwa wakuu wa mauaji maana katika maelezo yao ya awali walikiri jinsi walivyojishirikisha na mauaji ya marehemu. Itakumbukwa kuna uzi ulishahi kuanzishwa juu ya watuhumiwa wa mauaji ya mwenyekiti CDM wa USA kukamatwa kwa mganga wa kienyeji Sindiga, sasa baadhi ya watuhumiwa hao ndiyo waliotoroka.

Taarifa za awali zinasema walifanikiwa kupora na bunduki moja ambayo baadae waliitelekeza.

MoDs usfute uzi huu, taarifa hizi hazina shaka kabisa kwa mujibu wa chanzo changu makini kilichopo huko Arusha.

Majina mkuu
 
Mkuu Matola unataka kumfundisha jamaa awe na id nyingine ya kuanzisha tetesi hahaaaaaaa!
anyway, nilikuwa pale central police nikawa nasikia stori za namna hiyo, ila sikutilia maanani sikujua imetokea wapi maana nilikuwa nimeconcentrate kwenye mambo yangu.
kama ni kweli huu ni unyama wa hali ya juu, na msishangae na muuaji wa Daudi Mwangosi naye akatoroka kwa staili hiyo hiyo kupoteza ushahidi!
Mkuu wangu wote tunaijenga Chadema katika maandalizi ya kuchukuwa dola 2015 na hawa kwa taaluma zao ndio katika mganyo wa majukumu watakuwa wasemaji wa ngazi au idara au Wizara mbalimbali, sasa ni lazima tuanze kuwakosoa mapema kwamba hatuhitaji ubabaishaji, na ndio maana mimi hapa JF hakuna asiyejuwa kwamba namkosoa Zitto Kabwe kwa sababu ninazo sababu za kumkosoa.

Hivi Imagine leo umkute Tumaini Makene naye yupo MMU anashiriki mada ya jinsi ya kumfikisha mwanamke kileleni u think you will take him serious anymore?
 
Mbona kazi ndogo tu ...... kamata hao askari weka ndani washughulikieni mpaka waseme walikowaelekeza kukimbilia na hiyo kesi imefikia hatua gani jamani? Au ndo kusema upelelezi bado wakati mauaji yalishafanyika.... bongo ni bongo tu
 
Inabidi Polisi watuambie upelelezi wa kesi hii ulifikia hatua gani? Kutoroka kwa watuhumiwa hao kutaathiri vipi maendeleo ya upelelezi na kesi yenyewe?
Haya matukio ya kashfa ambazo zinalihusisha Jeshi la Polisi yananifanya nianze kuamini kuwa there is something seriously wrong kwenye jeshi hili
 
How long will the CITIZENS on TANZANIA watch from the sidelines while some 'thugs' (CCM) decide our future??? if we don't do nothing-then we must just forget it and take a ride to 'Africa'
 
Hivi unafahamu kwamba wewe ni msemaji wa Chama? sasa haya mambo ya tetesi na nafasi yako wapi na wapi? Najuwa fika hili swala linaweza kuwa limetokea ila huoni kuwa kama mseamaji rasmi wa Chama unapaswa kuongea fact?

Hivi Salva Rweyemamu naye atuletee thread ya tetesi hapa JF unategemea tutamnyamazia kimya? No way thread zingine waache waanzishe watu wengine na siyo wewe, ninapoona jina lako nategemea fact tu na siyo tetesi.

Matola

Nimeipenda constructive criticism yako. Nimekuelewa. Pole kwa usumbufu.
 
Yaani askari wamuone mwenzao ananyang'anywa silaha na mtuhumiwa wa mauaji lakini wakae kimya? Haingiii akilini hata chembe! Vipi kama huyo mtuhumiwa angetumia hiyo silaha papo hapo na kuwamaliza? Ule ujasiri wa kupiga watu wasio na hatia wala silaha umeenda wapi?
 
huyu kaandika kama member wa jf. Lingekuwa tamko la chama angeitisha vyombo vya habari. au kwa kuwa ni msemaji wa chama hamtaki aenjoy jf? acheni hizo bana. Mia
 
Hawa ccm wamesahau nassari aliwatuliza wameru ........ Sasa wanahatarisha familia zao pamoja na ccm yenyewe sasa watu watakumbuka na kutake action na watu wa usa - river ni watu wanaoweza kutake action very fast
 
Mkuu ruttashobolwa, it is confirmed. Lakini pia ukinisoma between words unaweza kuona tayari ilikuwa confirmed. Ukiangalia kwa makini matumizi ya maneno niliyokuwa nayatumia utaona confirmation. But pole kwa usumbufu kamanda. I love constructive criticsim.
Huo ndo moyo unaotakiwa wa kukubali kukosolewa..sasa kwa kuwa wewe ndo muanzisha thread..nenda ka-edit post na uondoe hilo neno tetesi linalowachanganya watu..
 
NAAMINI WAMETOROKA ILI KUPOTEZA USHAHID NA KUTAKUA NA USHIRIKI MKUBWA WALIOWAAGIZA KUTEKELEZA MAUAJI HAYO/CCM.:hatari:
 
Mkuu ruttashobolwa, it is confirmed. Lakini pia ukinisoma between words unaweza kuona tayari ilikuwa confirmed. Ukiangalia kwa makini matumizi ya maneno niliyokuwa nayatumia utaona confirmation. But pole kwa usumbufu kamanda. I love constructive criticsim.
Sasa kuanzia hapa hii ni habari rasmi kwangu, wajurishe mods waondoe neno tetesi waweke Confirmed then sasa tuanze mjadala rasmi.
Ila Nakushukuru kwa kuwa muelewa, umeonesha tofauti yako na Magamba. Kudos!
 
  • Thanks
Reactions: ral
Back
Top Bottom