Mauaji ya Daudi Mwangosi: Jaji Mstaafu Ihema Kuongoza Tume Huru ya Uchunguzi!

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,146
13,216
  1. Judge...........Mwenyekiti
  2. Theophile Makunga-Tanzania Editors Forum (TEF)
  3. Pili Mtambalike-MCT
  4. Jeshi la Polisi
  5. Mtaalamu wa Mabomu
ameipa mwezi mmoja ilete taarifa, anasema kuna maswali mengi yamegubika kifo cha Mwangosi mojawapo ikiwa ni mahusiano kati ya mwandishi na jeshi la polisi na amesema hivi karibuni atachukua hatua kali dhili ya polisi wazembe

Wakuu

Hizi ndizo hadidu za Rejea za Dr Nchimbi kwa Tume yake

1.Je nini chanzo cha Kifo cha DM?
2. Je ni kweli kwamba kuna uhasama kati ya waandishi wa habari mkoani Iringa na Jeshi la Polisi?
3. Je ni kweli kwamba kuna waandishi 3 walipanga kuuawa na jeshi la Polisi mkoani Iringa?
4. Je Ukubwa wa nguvu iliyotumika ulikua sahihi?
5. Je zipo taratibu zozote za vyama vya siasa kukata rufaa visiporidhika na maamuzi ya Jeshi la Polisi?
6. Je ni kweli kuna tatizo la mahusiano baina ya jeshi la polisi na vyama vya siasa?

My take;

angalieni wenyewe, aina ya maswali, nature ya tukio, aina ya wajumbe......kuna mparaganyiko mkubwa sana, sijui kama huyu jamaa ali-consult, maswali hayajaenda shule kabisa, na kama ndio TORs basi hakuna kitu hapo.
 
Hizi tume huwa zinaniudhi sana,basi tu ngoja nisiongee mengi
 
Kuna sababu gani ya kuunda tume, kwa nini wasimwulize aliyekuwa Mkuu wa Operation ile ili atoe taarifa ya Polisi aliyemlipua marehemu au achukue zile picha aangalie. Hivi hizi tume zinatumia pesa ya nani katika uchunguzi kama huu wa kuficha ukweli ?
 
Kinachotakiwa haraka ni Nchimbi na Mwema kujiuzuru mara moja!

Kwa nini tume ipewe mwezi mmoja kuchunguza kitu ambacho kiko wazi?
IGP Mwema na RPC kamuhanda kabla ya yote watafakari kilichotokea na wachukue uamuzi wa kuwajibika kwa heshima na historia itawakumbuka kwa ilo,hizi tume hazina maana yoyote ni delaying tactics,sijawahi kuona faida ya tume zaidi ya kupoteza kodi za wananchi.
 
mh kweli tanzania wamezidi na tume zao kila kitu tume,hata njaa ikiingia mahali flan tume yaundwa,hata namna ya kupata wajumbe wa kuunda tume ,tume yaundwa,mkuu wa nch aliulizwa kwanini tanzania inaongoza kwa kuunda tume,akajibiwa itabidi tuunde tume kupata jibu la swali lako,mh!
 
Yaani mwaka huu tutapewa ban hapa kama nini taarifa zingine zinaudhi kama nini
Nchi haina uongozi wowote,wananchi viongozi waandishi wakatae kata kata kushiriki tume gani haina mwakilishi wa wananchi ,vyama vya siasa,wabunge,vyuo vikuu,NGO huu ni utumbo kabisa Nchimbi tokemea huko nawe uko kwenye list ya wauaji wananchi wanne kamhanda aliwachinja kama kuku Songea hukuenda kuwaona wala hukutoa salamu wa kukemea ukiwa mbunge wa jimbo la songea mjini
dont make us as fools
 
Dhumuni la tume sio kuleta ukweli bali ni kuvuta muda watanzania wasahau,kwani ndani ya mwezi mmoja linaweza tokea jingine la kishenzi watu wakahamia huko wakasahau hili la Mwangosi.Picha zinaonyesha lakini bado wanaunda tume!!!
 
ilitakiwa tume hiyo isihusishwe polisi wa aina yeyote yule,wala jeshi wala jkt lakini kwa kuwaweka polisi ndani ni kama kupoteza pesa ya walipa kodi,kwani kuna ulazima polisi kuwepo ama kuchunguza jambp ambalo linawahusu
 
Tulishapoteza naye imani kwenye kifo cha marehemu Ally Zona Morogoro baada ya kutoa majibu ya hovyo kabla ya TUME na kisha TUME ikaleta majibu ya hovyo hayohayo. Vilevile tunamshangaa kwa kuwashirikisha POLISI wa hapa nchini kwenye TUME hizi ambazo na wao ni walalamikiwa/wahalifu. Hatutegemei jipya, na kama mwendo ndiyo huu basi ni dhahiri SERIKALI yetu imeshindwa. Kwa ushauri wa harakaharaka ni bora yeye na wakuu wenzie wa Wizara ya Mambo ya ndani akiwemo IGP Mwema wajiuzuru haraka ili kurejesha imani kidooogo na jeshi letu la polisi pamoja na serikali.
 
Kinachotakiwa haraka ni Nchimbi na Mwema kujiuzuru mara moja!

Kwa nini tume ipewe mwezi mmoja kuchunguza kitu ambacho kiko wazi?

Mkuu hata mimi inanishangaza; wiki moja inatosha uchunguzi, hata hivyo tusifikiri anataka kujua kwa nini polisi wameua bali ni tume ya kuthibitisha kuwa Mwangosi aliuawa kihalali na tusitegemee kitu tofauti!!
 
Amewahusisha wahusika wa TFF, Mahakama, MCT na Polisi?
Inawezekana kakurupuka akawateua marafiki zake wamfanyie uchunguzi!
Marehemu alirushiwa bomu direct na picha imeonyesha, tume ya nini tena?

Mwishowe utasikia
"Rimarehemu riripigwa na rikitu kizito tumboni riutumbo rikatawanyika"

..mbavu zao hao polisi






 
Back
Top Bottom