SoC03 Matumizi bora ya elimu

Stories of Change - 2023 Competition
Jun 8, 2023
4
1
Katika kizazi cha Sasa hasa katika nchi za dunia ya tatu,neno elimu limekuwa likichukuliwa katika upande hasi kwa sababu ya kuwepo kwa wasomi wengi ambao wameweza kupata elimu lakini maisha yao yapo chini ukilingana na watu ambao hawana elimu.

Katika nchi hizi za dunia ya tatu au zinazoendelea asilimia kubwa ya watu walioendelea ni wale walio pata elimu ya mtaani kuliko watu waliopata elimu ya darasani na kitu cha kushangaza na cha kusikitisha katika nchi hizi zinazoendelea watu wenye uwezo mkubwa shuleni wengi wao huwa huingiza kipato kidogo au huw na hali ya chini ya kimaisha ukilinganisha na wale wengi wao walioishia darasa la saba na kianz shughuli zao mbalimbali,

Asilimia kubwa ya wasomi wengi kwenye hizi nchi wengi wao ndio hutumia mda wao mwingi kwenye mitandao ya kijamii kwa kufanya mambo ambayo hayasaidii katika kujenga nchi na asilimia kubwa ya wasomi wengi ambao ndio wanatambua kuwa Afrika ndio bara ambalo nchi nyingi ni ni za dunia ya tatu au zinazoendelea,nchi nyingi huwa zinategemea misaada kutoka nchizilizoendelea.

Na ndio wasomi hao hao ambao huwa Kila siku wanalalamika kuwa serikali yetu haifai kwa sababu haijatupa ajira,Pia wasomi haohao ambao wanatambua dhairi shairi kwamba moja ya vitu ambavyo vinatufanya tuitwe nchi zinazoendelea mpaka hivi sasa ni kutegemea kutoka kwa nchi zilizoendelea kisiasa,kijamii,kiuchumi ndio hao hao Kila siku iitwapo leo ambao huwa mstari wa mbele katika kudai maslai yao ya kuikosoa aerikali kuwa inakopa sana,huku wakitaka mishahara yao iongezwe

Pia wasomi haohao wanaotambua kuwa moja ya vitu vinavyotifanya tusiendelee mpaka Sasa ni kutegemea katika sekta moja ya uzalishaji ndio hao hao ambao asilimia kubwa huyaendesha maisha yao kwa kutegemea mshahara kutoka serikalini.

Kwa namna hiyo basi,Je ni kweli elimu inayotolewa katika nchi za dunia ya tatu haina manufaa na faida katika jamii hii tu ayoishi?

Na kama ni kweli,kwanini baadhi ya wanafunzi ambao wamepata elimu hiyo hiyo baadhi yao hupata nafasi za kusoma katika nchi zilizoendelea na kuweza kufanya vizuri katika nchi hizo.

Kwa namna hiyo basi elimu inayotolewa Tanzania ni sahihi kabisa kwa kizazi cha Sasa bali watu ambao tunapata ndio tumekubali kuishi katika mfumo ambao kwa msomi lazima aanze shule za awali,shule ya msingi sekondari,chuo na baadae uajiriwe hatuna akiri ile ya kujiongez kwa mfano, sawa nimeweza kupata elimu hadi ya kidato cha sita je nawezaje kuitumia mtaani ili niweze kunufaika kupitia elimu yangu na kuweza kuisaidia jamii yangu kupitia elimu yangu

Sawa serikali imeweka mtihani kama kupima uwezo wako, pia wewe kama msomi jaribu Sasa na wewe unapokuwa mtaani kuweza kuitumia elimu uliyoipata sasa kutatua changamoto zinazoikabiri jamii yako ili jamii nayo iweze Sasa kutambua kwa uwezo Sasa ulio nao wa kielimu.

Asilimia kubwa ya wasomi wengi katika nchi ya Tanzania wanapomaliza masomo baada ya kurudi mtaani sasa huwa wanaanza kufanya shughuri ambazo haziendani na elimu uliyoipat.kwa mfano asilimia kubwa ya wasomi kazi zao nyingi ni zile ambazo zina tumia akili sana kuliko nguvu lakini wasomi hao wanaporudi mtaani hufanya shughuri ambazo zinatumia nguvu sana kuliko akili.

Kwakumalizia ni kwamba kwa sasa ni muda sahihi wa mtanzania mwenzangu wa kubadirisha mitazamo yetu na mifumo ya maisha tunayoishi,tusiishi katika mifumo turiyorithishwa na wakolonibali tuishi maisha sisi kama waafrika tusifuate miongozo na sheria za elimu ambayo tuliyowekewa kwamba mtu ili aitwe msomi ni yule ambaye amesoma na mwisho wa siku ameajiriwa na serikali tujaribu kubadilisha mitazamo tuliyokuwa nayo ukipata elimu hadi ya kidato cha sita lazima utakuwa na kitu ambacho unaweza ukakifanya nakuweza kuisaidia jamii jaribu kukumbuka kwamba kabla ya kuja elimu hii ya mfumo wa kikoloni kuna elimu ambayo tulikuwa nayo sisi kam waafrika,pia ukiondoa na elimu tunayoipata pia sisi kama binadamu tunao uwezo na maarifa asilia ambao tumejariwa na mwenyezi mungu hivyo basi tusiishi katika maisha ya kutegemea tusiishi maisha ya kuilaumu serikali Kila kuitwapo Leo sisi kama wasomi tunatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuisaidia serikali katika kutengeneza ajira na sio kutegemea ajira kutoka kwao,

Ili nchi yetu iweze kupata mafanikio sisi kama wasomi tuna mchango mkubwa sana katika kujenga hii nchi na vitu vyote hivi tutaweza kufanikiwa pale ambapo sisi sote kama wasomi haijalishi umeishia sehemu gani tukikubari kubadirika katika mfumo tunaouishi na kukubali kubadirika, ni muda wetu wa kuisaidia jamii kuondoa umaskini kwa kufumbua ajira mbalimbali kupitia sisi wasomi,ni muda wetu wakutatua suala la utegemezi katika nchi zilizoendelea,tambua ukiondoa elimu uliyonayo wewe ni binadamu wa kipekee sana unayeweza kuisaidia nchi yako iondokane na hili janga la umaskini

Natamani siku moja kizazi kinachokuja kifurahie matunda tuliyoyatengeza sisi natamani kupitia sisi tutimize ndoto aliyokuwa anayoiota babu yetu Martin Luther King Junior kwamba waafrika nao watambuliwe kwa uwezo tulio nao na imani kwamba kuna siku tutafanikiwa kwa sababu sisi kama waafrika tumeumbwa kuwa wakipekee sana na hiki tutatambua uwezo tuliokuwa nao,Asante
 
Back
Top Bottom