Matumizi Bora ya Ardhi Yapangwe ili Kuondoa Migogoro ya Ardhi Nchini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

MBUNGE JAFARI WAMBURA ATAKA MATUMIZI BORA YA ARDHI YAPANGWE ILI KUONDOA MIGOGORO YA ARDHI NCHINI

"Chanzo cha migogoro ya Ardhi nchini mojawapo ni kupitwa kwa Sera ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi ambayo ni ya Mwaka 1995 haiendani na kasi ya uzalishaji na shughuli za kiuchumi za wananchi wanazofanya" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Population (Ongezeko la watu) iliyokuwepo wakati Sera inatungwa mwaka 1995 haiwezi kuwa sawa na sasa kwa namna shughuli za uzalishaji zinavyofanyika. Lazima kutakuwa na muingiliano" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Sababu nyingine ya migogoro ya Ardhi nchini ni Mpango wa Matumizi bora ya Ardhi, kukosekana kwa Mpango wa Matumizi bora ya Ardhi kwenye ngazi za Vijiji. Hili nalo linaweza kuwa linachangia kwa kiasi kikubwa" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Sababu nyingine ya migogoro ya Ardhi nchini ni muingiliano wa Wizara za kisekta, Wizara ya Ardhi, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya TAMISEMI. Yanatokana na Sera iliyopitwa na wakati. Sera ya Ardhi ndiyo chimbuko la migogoro ya Ardhi nchini" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Migogoro ya Ardhi inatugombanisha Wananchi na Wabunge, Inagombanisha Serikali na wananchi, Inagombanisha Chama na wananchi, Jamii moja na Jamii, Wabunge, Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Rorya kuna sintofahamu ya eneo la Uteki, Kata ya Kitongoji cha Kiwandani na Begi. Katika Vijiji 975 vilivyoainishwa kuwa n migogoro nchini ambapo Mawaziri wanapita hivi vitongoji havimo. Sasa hivi tumetengeneza taharuki tunawaambia wananchi zaidi ya Kaya 300 zaidi ya wananchi 1200 wahame na hawalipwi fidia wanalipwa uwezeshaji pekee yake. Tunataka kutengeneza mgogoro ambao hauna tija" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Wananchi wanasema kabla hatujafika huko kwanza tusimamie sheria ya kushirikishwa kwenye mikutano waambiwe dhumuni ni nini la wananchi kuondolewa eneo lile. Na hii ndiyo sheria ya uthamini inavyotaka" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Wananchi wasingependa waendelee kuitwa kuwa wao ni wavamizi. Wana miaka zaidi ya 60 na 70. Shule ya Msingi pale imejengwa tangu mwaka 1959, tukiwaita wavamizi waondoke bila kuwalipa tunakwenda kutengeneza mgogoro mwingine" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Ikibainika wanatakiwa kuhama walipwe fidia stahiki kwa mujibu wa Sheria. Wananchi hawajagoma ila wanachogoma ni ushirikishwaji. Mpaka sasa hakuna Kiongozi aliyekwenda kuzungumza na wananchi na kuwaambia ABC" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Ilani ya CCM 2020-2025 ukurasa wa 20 Ibara ya 74 inasema kwa miaka 5 Vijiji vinavyotakiwa kupanga Matumizi bora ya Ardhi nchini ni 4431. Mpango wa tatu wa maendeleo unasema ifikapo mwaka 2025-2026 tuwe tumepanga Matumizi bora ya Ardhi 50%" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Vijiji tulivyonavyo sasa ni 12,318. Tulivyopanga toka Uhuru ni Vijiji 2810+ (23%). Kwa miaka 3 ili kuendana na Ilani, Mpango na Maelekezo ya Rais tumepanga Vijiji 681. Yote haya yamekuwepo kwa sababu ya ukosefu wa fedha" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Tumepata Mkopo wa Bilioni 345. Tutenge Bilioni 60 ili kutekeleza Ilani ya CCM kwa kupanga Vijiji 4131, Mpango wa tatu wa uchaguzi, kutekeleza maagizo ya Rais na kuweka historia nzuri ya tangu Uhuru kupanga Vijiji vingi kuliko wakati wowote" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya
 
Attachments

  • WhatsApp Image 2023-05-29 at 16.29.36.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-29 at 16.29.36.jpeg
    44.4 KB · Views: 3

Upimaji wa Ardhi (Land Surveying) siyo kipaumbele kwa Serikali ya nchi yetu, kipaumbele kikuu cha utawala wa nchi yetu ni masuala ya Siasa
 
Back
Top Bottom